08 December 2010

Khan atamba kuinua heshima ya Uingereza

LAS Vegas, Marekani

BONDIA Amir Khan, anaamini pambano lake la Jumamosi linaweza kuinua heshima ya Waingereza baada ya ya lile lililoboa mashabiki kati ya Audley Harrison, ambaye alipigwa mapema na David Haye.Bingwa huyo wa WBA wa uzani
wa light-welter, Khan atatetea ubingwa wake mjini Las Vegas katika Ukumbi wa Mandalay Bay Hotel, dhidi ya Marcos Maidana.

Katika usiku huo, pia bondia wa uzito wa juu Dereck Chisora atakuwa akijaribu kutwaa taji la ubingwa wa uzito wa juu dhidi ya bingwa mtetezi wa mikanda ya IBF na WBO, Klitschko mjini Mannheim, Ujerumani.

Pia katika mji wa Liverpool, Echo Arena, aliyekuwa bingwa Olimpiki, James DeGale goes atacheza mechi yake ya kwanza ya kuwania ubingwa kwa kutwangana na Mwingereza, Paul Smith katika mechi ya uzani wa super middle na Nathan Cleverly atapigana kuwania nafasi ya kuja kushindania taji la WBO uzani wa light-heavy dhidi Alejandro Lakatos.

Khan mwenye miaka 24, amekerwa na uchezaji wa Harrison katika mechi ya uzito wa juu duniani ya kuwania ubingwa wa WBA, iliyochezwa mjini Manchester katika Uwanja wa MEN mwezi uliopita.

Aliwataka Waingereza wenzake watakaopanda ulingoni Jumamosi kulisafisha jina la nchi yao. "Si mabondia tu wanaohusika katika mapambao ya ubingwa wa Dunia kama mimi na Chisora, tunaotakiwa kuweka mbele utaifa," alisema.

Alisema mechi zitakazochezwa Ujerumani, Marekani na Liverpool ni muhimu kwa kuonesha ni jinsi gani Uingereza ilivyo na mabondia wazuri.
Khan atakuwa akipigana kwa mara kwanza mjini Las Vegas, pia kutakuwa na pambano kubwa Liverpool na Chisora atajaribu kutwaa ubingwa wa dunia Ujerumani.

Alisema katika mechi za Jumamosi, hatarajii kutokea kile kilichotokea Manchester, wakati wa mechi kati ya Haye na Harisson.Khan alisema anatarajia pambano lake dhidi ya Maidana, litakuwa kali kwa kuwa wote ni wapiganaji wakali na wako katika nne bora duniani.

Bondia huyo alikuwa miongoni mwa wanandondi waliokuwa wakimpa nafasi kubwa Harrison, kutoka upinzani kwa Haye katika mechi yake ya kuwania Ubingwa wa Dunia."Niliona pambano la Haye. Wapiganaji hawakuwa karibu na Haye alikuwa na kasi zaidi ya nilivyofikiri kwamba pambano angalau lingefika raundi ya tano au zaidi," alisema.

Alisema hataki kupigana na kupata matokeo kama ilivyokuwa kwa Harrison, na kwa uzoefu wake anajua kuwa ni ngumu kuwa bingwa wa Olimpiki, alipata medali ya fedha, lakini Harrison alitwaa ubingwa.

No comments:

Post a Comment