17 December 2010

Ilala, Kisarwe kupata umeme Jumanne

Na Peter Mwenda

WAKAZI wa baadhi ya maeneo Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam na Kisarawe Mkoa wa Pwani wanatarajiwa kupata tena umeme, Jumanne baada ya kutengemaa kwa transifoma inayosambaza umeme katika eneo hilo.Kuharibika transifoma hiyo
  kusababisha kukosekana kwa umeme katika maeneo mengi ya wilaya hizo.

Meneja wa Mradi wa Kampuni ya National Contracting  ya Saudi Arabia inayofunga transifoma hiyo, Bw. Sadeesh John alisema kazi ya kufunga transifoma hiyo imekamilika bali bado kujaza mafuta na kukamilisha uunganishaji wa nyaya.

Alisema kumalizika kufunga transifoma hilo na kuanza kazi kutategemea kama mvua hazitanyesha kuathiri utendaji wa kazi vinginevyo hakutakuwa na mabadiliko mengine.

Bw. Sadeesh alisema kuchelewa kufunga transifoma hiyo kumetokana na sababu mbalimbali hasa kuchelewa kutoka  bandarini katika kitengo cha ushuru wa Forodha.

Alisema transifoma hiyo iliyotengenezwa nchini India yenye uwezo wa kupokea msongo wa umeme wa Voltage 45 inachukua nafasi ya ingine la Italia ambalo limeharibika.Transifoma hilo liliharibika mapema mwezi uliopita na kusababisha maeneo mengi ya Jiji la Dar es Salaam kukosa umeme kwa zaidi ya saa 16 na kusababisha huduma na uzalishaji mali kushuka.

Kati ya walioathirika zaidi ni wagonjwa katika Hospitali ya Kisarawe mkoani Pwani ambao wameshindwa kufanyiwa upasuaji kwa kukosa maji yanayozalishwa na umeme.Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Badra Masoud aliwaomba wakazi wa maeneo hayo kuvuta subira wakati kazi ya kumalisha ufungaji wa transfoma unakamilika.

1 comment:

  1. Hivi huyu meneja uhusiano anapo waomba wakazi kuvuta subra sijui anakuwa anakusudia nini?
    Hii ni jinsi gani inavyoonyesha kuwa shirika zima halina mtu mwenye jukumu au dhamana ya kuwa umeme unapo kosekana basi anawajibu wa kuiacha ofisi na kuwajibishwa.
    Tanesco kama bwana ngeleja unataka iwe na ufanisi mzuri na si kuwatia madeni watanzania ni Bora ndani ya Tanesco kuwe na Ushindani wa kiutendaji ambao Shirika tuligawe katika Sehemu mbili,Yaani Tanesco South West,na Tanesco East North,na kila shirika liwe na utawala wake kiutendaji,kimantiki ni kuwa South West Itakuwa ikimiliki nusu ya mikoa ya nchi na East North Itamiliki nusu ya mikoa iliyobaki ikiwa ni pamoja na Zanzibar.
    Hii itawezesha kuwa na ufanisi bora,kwani kutakuwa hakuna upande utakao kubali kuonekana unafanya uzembe.K
    KWA SASA TANESCO HAWAJIONI KAMA WANATIA HASARA NA MADENI KWA KILA MTANZANIA,KWANI WANAJIONA KUWA HAWANA UPINZANIA WA SEKTA YA NISHATI YA UMEME HAPO NCHINI,

    MUNGU IBARIKI TANZANIA INAZAMA MUNGU!!!!!!

    ReplyDelete