15 November 2010

Wizara ya Habari yatupiwa lawama.

Na Heri Shaaban

WIZARA ya Habari, Utamaduni na Michezo imeelezwa kuwa ndiyo chanzo cha kushuka kwa kiwango cha michezo katika shule za msingi nchini.Hayo yalisemwa
mwishoni mwa wiki na Ofisa Utamaduni na Michezo wa Manispaa ya Ilala, Shani Kitogo, wakati wa mafunzo ya siku moja kutoka kwa walimu wa michezo na sanaa wa Shule za Msingi za Kata 27 za Manispaa hiyo.

Shani alisema, awali shule hizo zilikuwa zikiandaa michezo mbalimbali, lakini kutokana na Wizara hiyo kuzisahau, ndiyo maana imesababisha kiwango cha michezo kushuka katika shule hizo.

''Naomba Serikali itukumbuke na kututengea fungu, ambalo litapitia Manispaa kwa lengo la kuinua michezo shule za msingi, ili watoto wetu wasijitumbukize katika kumbi za disko toto, kipindi cha mapumziko na sikukuu.

Amewataka walimu wa shule za msingi wakati wa mapumziko kuwandalia bonanza na kukutanisha shule mbalimbali ili watafute vipaji vya watoto.

Naye Ofisa Michezo Manipaa hiyo, Claud Mpelembwa alisema walimu wakuu wa Shule za Msingi nchini, wamekosa washauri, hali iliyosababisha michezo kushuka shule za msingi.

No comments:

Post a Comment