12 November 2010

Bundi anyemelea upinzani bungeni.

*Waunda kambi mbili tofauti, moja kuongozwa na Mbowe, nyingine Hamad Rashid

Peter Saramba na Charles Mwasyeba.
VYAMA vya upinzani vimeunda kambi mbili za upinzani katika Bunge la Jamhuri la Muungano baada Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuunda kambi yake ikijitegemea kutokana na
kuwa na idadi kubwa ya wabunge huku Chama cha Wananchi (CUF) kikiungana na NCCR-Magauzi kuunda kambi nyingine.

Kambi ya CHADEMA yenye jumla ya wabunge 45 inaongozwa na mbunge wa Jimbo la Hai na ambaye pia ni Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Bw. Freeman Mbowe akisaidiwa na mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe huku mnadhimu akiwa mbunge wa Singida Mashariki Bw. Tundu Lissu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi wa masuala ya bunge wa CHADEMA, Bw. John Mrema alisema walifikia uamzi wa kuunda kambi yao wenyewe baada ya juhudi zao za kuwashawishi wenzao wa CUF kuungana pamoja kugonga mwamba.

Alisema Bw.  Mbowe aliyefanya majadiliano na aliyekuwa kiongozi wa upinzani katika bunge liloisha, Bw. Ahamad Rashid.

Bw. Mrema alisema CHADEMA iliyoshinda viti 22 vya majimboni Tanzania bara ilitaka kunda kambi kwa kushirikiana na CUF ambayo imezoa viti vingi Tanzania visiwani na vingine viwili upande wa bara lakini wenzao waliamua kuunda kambi nyingine wakishirikiana na vama vingine vya upinzani vyenye wabunge.

Akizungumza na Majira kwa njia ya simu kutoka Dodoma jana, mbunge wa Wawi, Bw. Ahamed Rashid alisema wameamua kuunda kambi yao kwa kushirikiana na NCC-Mageuzi baada ya CHADEMA kushindwa kutimiza sharti la kushirikisha vyama vingine kwenye kambi ya upinzani.

“Kweli leo asubuhi (jana),mwenyekiti wa taifa wa CHADEMA, mheshimiwa Mbowe (Freeman) alinifuata kunieleza utayari wao wa kushirikiana nasi kuunda kambi ya upinzani lakini tuliwapa sharti la kushirikisha vyama vingine zaidi ya hivi viwili katika kambi hiyo. Wenzetu hawakuwa tayari hivyo tukaamua nasi tuunde kambi yetu kwa kushirikiana na NCC-Mageuzi,” alisema Bw. Rashid.

Alisema katika kambi hiyo ya pili yeye amechaguliwa kuwa kiongozi wa upinzani akisaidiwa na mbunge wa Gando, Bw. Halifa Suleiman Halifa pia wa CUF wakati David Kafulila, mbunge wa Kigoma Kusini akiwa mnadhimu huku akisema milango iko wazi kwa vyama vya Tanzania Labour (TLP) na United Democratic (UDP) kujiunga nao.

Bw. Rashid ambaye katika bunge liliopita aliongoza kambi ya upinzani akisaidiwa na Dkt. Willibrod Slaa aliyekuwa mbunge wa Karatu alisema katika majadiliano yake na Bw. Mbowe suala lingine lililoonekana kuhitaji maelezo ni ushiriki wa CUF katika serikali ya umoja wa kitaifa kwa upande wa Zanzibar.

“Katika hili nilimhakikishia mheshimiwa Mbowe kuwa tutatumia katiba na hali halisi ya kisiasa kwa upande muungano kwani sehemu hizi mbili za nchi yetu zote zina katiba na sheria zinazoheshimiwa na kufanya kazi kila upande. Wenzetu walikuwa na hofu kuhusu msimamo wetu juu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokana na mazingira yetu ya visiwani,” alisema Bw. Rashid.

Kuhusu nafasi ya uspika, kiongozi huyo alisema wao wanamuunga mkono mgombea wa kambi ya upinzani aliyesimamishwa na CHADEMA, Bw. Mabere Marando. Hata hivyo alisema kura ni siri ya kila mtu ingawa wao wangependa mgombea aliyesimamishwa na CCM, Bi. Anne Makinda aangushwe kwenye kinyang’anyiro hicho.

20 comments:

  1. Mbowe tafadhali fikieni makubalianoa na Hamad Rashid, sisi tupo nanyi kwa karibu sana. huyo Anna Makinda apigwe mweleka .Marando awe Spika. Makinda naye tunajua ni fisadi la kutupwa sasa hau ccm wameamua kuilipua hii nchi. Acheni mchezo kabisa kwani 79% ya watanzania imeerevuka na wanafuatilia kila mnachokifanya katika nchi hii na hata nje ya nchi.
    Tafadhali msifanye makosa.

    ReplyDelete
  2. Tafadhali tendeni haki nyie viongozi wa nchi hii Mungu hajalala usingizi anaona kila linalofanyika juu ya nchi hii yenye neema ya kila aina. Tamaa za dunia ambayo tunapita tu zisituponze na kumkosea Mungu wetu aliyetupendelea kwa kila kitu. Tumwogope Mungu jamani asije akatuchoka bureee!!!

    ReplyDelete
  3. huu ni wakati wa kujenga nchi si wa malumbano

    A S VICTOR

    ReplyDelete
  4. CUF NA CCM NI KITU KIMOJA HAO WABUNGE WA CUF WANATOKA ZANZIBAR WOTE UKIONDOA HAO WAWILI TU WA BARA, NA WAZANZIBAR WAMEAMUA KUSHIRIKIANA NA CCM, JE MNATEGEMEA KAMBI GANI YA UPINZANI ITAKAYOUNDWA NA CUF? WAKTI WAO NA CCM NI DAMU DAMU.
    NI HERI CHADEMA IJIPAMBANUE KWA KUJITENGA NA WANAFIKI WATAKAOWAANGAZIA MCHANA NA KUWACHOMA USIKU

    ReplyDelete
  5. CCM wanajulikana sana kwa kupandikiza watu wao ili kuharibu upinzani ili umma waone haufai wanataka madaraka tu. Hivyo CHADEMA kuweni macho na hao watu wanaosema mko wote katika upinzani wakati ni ngozi ya chui. Afadhali mkabaki peke yenu mkipanga mikakati tena kwa kuelewana bila migogoro watu wawe na imani na nyie. Ninachofahamu macho ya wa-tz yamewaangalia CHADEMA,wako nyuma yenu, jilinde na mapandikizi ya ccm kutaka kukiua chma na kila mwanachama mpya atakayejiunga macho naye sana. Kingunge na Makamba wako pale kwa kazi hiyo ya kuudhoofisha upinzani na kama wanavyotaka kuiua ccm yao. Huyo mama wa kulinda mafisadi bungeni asipewe kura, wanataka kuwazima midomo, ni vibaraka wao.

    ReplyDelete
  6. Mbowe hawezi kufikia makubaliano na CUF ambayo kimsingi ni CCM. Hata hiyo NCCR Mageuzi na TLP ziko huko huko.
    Kwa vile CHADEMA ipo kuleta mageuzi inaweza kusimama pekee kama wenzake hawataki na mambo yakaenda kama ilivyotokea kwenye uchaguzi uliopita.

    ReplyDelete
  7. Kutoaminiana miongoni mwa vyama vya upinzani pamoja na ubinafsi (sioni sababu kwa nini CHADEMA ikatae kuvishirikisha vyama vyengine mbali na CUF)ndio chanzo cha mfarakano baina yao. Vyovyote viwavyo, sisi letu jicho, si utawala si upinzani, madam tumeshawapa kula, endeleeni kula jasho letu.

    ReplyDelete
  8. UPINZANI NI KAZI SANA TANZANIA KWA VILE CCM INAHONGA UPINZANI NA KUWARUBUNI KWA UONGOZI HIVYO WANASALITI UPINZANI, SASA ONA HIVI KWELI MTU ALIYEKUFA MWAKA 2005 KWENYE UJO ZA UCHAGUZI AKIFUFUKA LEO AKUTE MAALIM SELFU NI MAKAMU WA RAIS ZANZIBAR CHINI YA CCM SI ATAOMBA AFE TENA!!
    HIVYO CUF KAMWE HAWATA UNGANA NA CHADEMA KWA VILE WANAMUUNGANO NA CCM! SASA CHAMA KIMOJA HAKIWEZI KWA CHAMA CHA UPINZANI BUNGENI NA NI MSHIRIKA WA CHAMA TAWALA-HUU WOTE NI UFISADI NA NJAA YA MADARAKA.
    MTU MWINGINE AMBAYE NI CCM KIVULI MBUNGE WA VUNJO BWANA MREMA, YEYE WALA SIYO NDUILA KUWILI BALI NI CCM DAMU.

    ReplyDelete
  9. Jamani CCM haijapandikiza mtu. Tumieni akili zenu mlizopewa na Mungu kuona nini kinaendelea. Malumbano hayo yanatokana na mwenendo wa chadema. Watu inabidi wakae chini na kusema May the real chadema stand up. Hivi nyie mnaoshabikia chadema mnawajua ni akina nani? Angalia walivyochagua wabunge wa viti maalumu. CCM tuliwaona wakipiga kura, lakini hao wa chadema walipatikanaje? Na jaribu kuangalia wangapi wanatoka wapi na wanahusiana na nani? Mkipata majibu ya maswali haya, mtapiga magoti kumshukuru Mungu kuirudisha madarakani CCM. Chadema si chama cha kuongoza nchi. Kinashikiliwa na watu wachache wenye ubinafsi. CCM walipiga kura kumchagua Makinda, Marando alichaguliwaje? WanaCCM walipiga kura wakamkataa Sitta, hiyo ndugu zangu ndiyo demokrasi. Nyie wafuasi wa chadema mchawi wenu ni viongozi wenu siyo CCM.

    ReplyDelete
  10. Mtaoa maoni namba tisa huna lolote zaidi ya kutapatapa. Kwani CCM zaidi ya kushikiliwa na mafisadi watatu wa nne wa kihindi ambao nao ni wachache sana inashikiliwa na nani?
    Chadema ikilinganishwa na CCM na CUF ni chama chenye mwelekeo na sera vinavyokipa sifa ya kuongoza nchi. Rejea kupata wabunge wengi toka sehemu mbali tofauti tofauti na CUF ambayo ni chama cha wapemba. Nadhani kwa nondo hii huenda utatia akilini ingawa umeficha jina lako kuonyesha ulivyo mwoga na mzushi.

    ReplyDelete
  11. Mimi naitwa Hafidh kutoka Visiwa vya amani- Zanzibar. Mimi napenda kumjibu ndugu yangu NNMHANGO- kuwa unaposema chama cha CUF ni chama cha wapemba !! hii sio logic kwa mtu mwenye muono ila kama una macho lakini huoni hapo ni suala jengine , ok by the way nataka nimuambie kua hoja yake sio ya msingi kwa sababu hizi:- 1) CUF ina wabunge kutoka Tanzania nzima, kina wabunge kutoka Pemba, kina wabunge kutoka Unguja na kina wabunge kutoka Tza Bara. Jee chadema Kinacho wabunge kutoka sehemu zote hizi ??
    2) M/Kiti wa CUF ni Mnyamwezi,K/Mkuu ni mpemba na Naibu Katibu mkuu ni kutoka Unguja. hawa ni viongozi wajuu kutoka front Line ya CUF, Hebu nitajie Front Line ya Chadema ?? imeweka uwiano kama hii??
    3) CUF ilipokua inaongoza kambi ya upinzani iliweka uwiano na chadema na UPDP,Hamad Rashid alikua kiongozi na akisaidiwa na Slaa na vile vile Cheo alikua yumo ndani ya kambi hii, jee kwa nini Chadema wanajivutia upande wao tuu ?! ndio mana Slogan ya Cuf inasema haki sawa kwa wote. Naomba ujibu Hoja na usigawe watu. epeka ukabila jenga hoja za msingi.thanks

    ReplyDelete
  12. mimi SADIKI from lushoto.nilikuwa nataka kumuunga mkono hafidh wa znz kwa points alizotoa kwa kumuelimisha huyo mshabiki wa chadema asiyejua siasa bali amekalia umbumbumbu.akumbuke hayati baba wa taifa alisema chama kitakachoweza kuiondoa ccm madarakani ni kile kitakachokuwa na nguvu znz na Tz bara.je kati ya cuf na chadema kipi chenye wabunge(nguvu)znz na bara?Jibu unalo.

    ReplyDelete
  13. Hivi kweli kwa ukweli wenyewe CUF ni chama cha upinzani?? Mbona Zanzibar wameunda serikali moja na CCM,au tuseme CUF wamegawanyika kuna CUF bara na CUF visiwani??? AU kuna CCM bara na ccm visiwani,Mbona inachanganya.huku bara wawe wapinzani,au kwenye bunge la muungano wawe wapinzani na visiwani wawe serikalini.si mnaona mnatuchanganya?? ndio maana ukitafakari kwa kina utaona CUF kwa kweli si wapinzani wakweli.Mimi naona Hata TLP,mbona walikuwa wanawapigia debe wagombea wa CCM,tutafakari.

    ReplyDelete
  14. Tatizo lililopo viongozi wa chadema na wafuasi wao wamejiona kama wao ni manabii wa nchi hii.Wengine wote wasiokuwa chadema hawana maana tena,msipolirekebisha hili mtaendelea kuwa wabinafsi wakubwa.Hatimae anguko lenu litakuwa kuu.Ni Ushauri Tu.

    ReplyDelete
  15. Tatizo Chadema hakitaki kushirikiana na vyama vingine kwa sababu ni chama cha mabepari waliokubuhu! Tena mafisadi wakubwa wanaojificha nyuma ya mgongo wa vita vya ufisadi. Ukimtoa Zitto hebu waangalie viongozi waliobaki pamoja na waasisi wao. Woga unakuja wakishirikiana na wengine malengo yao yatagundulika. Hawa wako hapo kutetea maslahi ya biashara zao na kupambana na wafanyabiashara wengine basi!

    Kwako Mhango, je kati ya Chadema na CUF kipi kina ushirikiano na uhusiano wa karibu na CCM? Kwanini watu hawaoni hili la Chadema kupewa milioni 200 na kada mkubwa wa CCM Sabodo? Je nani ana uhakika hizi pesa hazitoki kwenye akaunti ya CCM?

    Mhango unawasema wafanyabiashara wa kiasia, je huyu Sabodo ni mchaga au machinga? Mbona baba yake ni mchanganyiko wa mhindi na muiran? Au ndio yale ya Mtikila kelele nyingi kisha anaenda kuchukua pesa kwa hao hao anaowatukana mpaka siku walipomuumbua?

    Bora CUF inajulikana ni chama cha wananchi na waasisi wake pamoja na viongozi wanajulikana sio mapepari/mafisadi, maana ubepari ni unyama alisema Mwalimu Nyerere!

    ReplyDelete
  16. Mimi ni yule yule Hafidh kutoka visiwa vya amani Zanzibar. mimi sipendi nimpige madongo ndugu mwana mageuzi Mhango ila nataka nimpe Hoja za msingi pale anapojaribu kutoa sababu zisizokua na msingi madhubuti - Ndugu yangu Mhango umejenga hoja ya kwamba CUF kwa mtazamo wako sio chama cha Upinzani eti kwasababu wameungana na CCM kwa Zanzibar !! Hii hoja si yamsingi kwa sababu hizi :-
    1) Kenya kuna chama kinaongozwa na Bw.Raila
    Odinga na pia kuna chama kinaongozwa na Bw. Mwai Kibaki ,kumbuka hivi ni vyama viwili tofauti na wakati huo Bw. Raila alikua kutoka chama cha upinzani na mpaka kesho akiwa hai Bw. Raila ni mpinzani wa chama cha Mwai Kibaki lakini hawa wote wanaunda serikali ya pamoja ndugu yangu. kama hiyo haitoshi hata Zimbabwe kuna serikali ya pamoja kutoka vyama viwili vyenye nguvu.
    2)Hakuna chama chochote cha siasa duniani kilichokua hakina malengo ya kuongoza dola na ukiona kipo basi ujue kina shaka hicho chama na hata Chadema nacho kina lengo la kuongoza dola na sio kuendelea kua upinzani tuu !! kwa hiyo CUF kuingia katika mamlaka ya Uongozi ni moja ya agenda za kisiasa kuweza kuingia madarakani.
    3)CUF ni wapinzani wa kweli katika Tanzania hii ndugu yangu Mhango ukiacha upenzi na ushabiki usiokua na macho!! kwa nini nikuambie CUF ni chama cha upinzani wa kweli ni sababu hizi zifuatazo - kama unakumbukumbu nzuri ni chama pekee kilichokua na msimamo bila ya kutetereka kwa sababu CUF wamehama wanachama wake ambao ni viongozi wakuu hasa na hakijatikisika kwa mfano :- Mzee Mapalala,Salum Msabah,Lwakatare,Bi Fatma Magimbi etc hawa ni baadhi tuu na ujue hawa walikua viongozi wandamizi wa chama lakini chama kama chama kipo na hakijayumba, jee hili vipi kwa NCCR cha wakati huo wa mrema ? na vipi leo akitoka Slaa na zitto kwenye chadema ?! hali haitokua tete? hili halina shaka itakua tete mana Zitto aliwahi kunukuliwa alikua anataka kugombea Uenyekiti au kujaribu kutoa makosa katika chama basi chama unahisi kinayumba kwa mtu mmoja tu?!
    4) CUF kimepambana na CCM kwa Zanzibar mpaka kimeeleweka ndugu yangu Mhango!! hili halitaki Tochi CCM kwa Zanzibar walikua hawataki kusikia wanafanya kazi pamoja na CUF katika Serikali na ndio mana kuna wahafidhina Zanzibar ! unalijua hili !! lakini kwa vile hawana budi na wamegonga mwamba wameona waweke mikono juuu - upepo bado unaendelea lengo la CUF ni kuondoa CCM kabisa katika madaraka na kumbuka ikifikia hapo jua ndio Bye bye CCM Zanzibar tunazika kabisa na hii ndio njia ya kuwaonyesha watanzania kua CCM sio chaguo lao kwa sasa.
    Ndugu yangu naona nisikuchoshe sana kuna mengi ya kukufahamisha ila nachelea kuona tabu kusoma kama makala! Jenga Hoja za msingi ili na sisi tujenge nguvu za hoja zetu.

    TANZANIA YENYE NEEMA ILIOJAA MALI ASILI - BADO INAENDELEA KUA MASKINI?!! BILA YA MSAADA TANZANIA INAWEZEKANA. WE NEED CHANGE - YES WE CAN

    ReplyDelete
  17. kwa kweli bwana hafidh umetuelimisha vya kutosha,umejenga hoja na umeweza kuitetea kiuchambuzi hasa.asielewa ni mbinafsi na mwenye fikra mgando ni bora kuachana nae kwani wajinga hawaishi duniani.ni hamdan mrope nikiwa mbeya

    ReplyDelete
  18. Acheni ushamba!!!pamoja na serikali ya umoja wa kitaifa hayo ni maigizo!!!upinzani manake ni kusimama kwa miguu yao wenyewe na kama wapinzani wakishakuwa na agenda moja bila unafiki na njaa wanaweza kuungana lakini tatizo vyama vingine bado vinajali matumbo yao wenyewe!!Na kama wanaodai kuwa CUF ina uwiano wa wabunge kutoka bara hadi visiwani,je kuna wakristu wangapi katika uwiano huo?Au alimradi anayegombea ni muislam anachaguliwa hata kama
    hana qualities,angalieni ubora wa candidate!!Maneno ya wakosaji wakikosa la kusema watadai mafisadi nyuma ya vita ya ufisadi mbona hamjasimama mpeleke vielelezo mahakamani ili wakamatwe???

    ReplyDelete
  19. Wewe Sadiki kutoka lushoto ni mbumbumbu zaidi ya huyo uliyemuunga mkono!!!Baada ya kutaja wasifu wako sishangai,du sijui nani atawatoa matongotongo mjue kinachojiri

    ReplyDelete
  20. Hongereni CHADEMA!!Endelea kusimama imara kama simba!!!Kama mna uhakika wa vyama ambavyo ni MAGUGU!!Msijali,songeni mbele, chezeni kwa akili na msimame wenyewe,na gugu likipandikizwa ndani yenu kwa faida za chama kingine msisite kumtimua ili kukinusuru chama manake gharama ya kulea gugu ni kubwa na itafanya zabibu isistawi ndani ya chama chenu.
    Msikurupuke kufanya maamuzi na agenda muhimu!!
    Wote kwa pamoja shikamaneni kukipanua chama pande zote za TZ Bara na Visiwani bila kujali dini,rangi wala kabila zaidi ya kujali ubora,uaminifu na moyo wa kuleta mabadiliko ya kweli kwa Watanzania wote kwa ujumla.

    ReplyDelete