Na Adam Hussein
WIZARA ya Viwanda, Biashara na Masoko kwa kushirikiana na Serikali ya Japani wameanzisha mafunzo ya vitendo kuhusu mbinu za uendeshaji na usimamizi wa biashara za viwanda
kwa wazalishaji wa nguo nchini.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko, Kaimu katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Desystant Masawe alisema, kupitia mafunzo hayo wazalishaji wa nguo nchini watatengeneza nguo nzuri na za kisasa jambo ambalo litasaidia kuinua kipato chao.
Alisema, Serikali ya Japan kupitia Chuo K
uu cha GRIPS cha Tokyo ambao utakuwa ni ushirikiano endelevu kuhakikisha wamiliki wa viwanda nchini wanakuwa na uwezo wa kushiriki kikamilifu katika Sekta ya Viwanda ndani na nje nchi.
Bw. Masawe alisema, wazalishaji wa nguo na bidhaa zake, wanachukua sehemu muhimu ya sekta ndogo ya Viwanda vya nguo hapa nchini ambapo sekta hiyo imekuwa ikitoa mchango mkubwa kwenye uchumi wa nchi.
Alitoa mfano kuwa sekta hiyo kuwa imekuwa na mchango mkubwa katika kutoa ajira, pato la Taifa na hivyo kuchangia kupunguza umasikini miongoni mwa wazalishaji na wafanyakazi.
Alisema mojawapo ya mchango wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko ni kuifikisha nchi katika uchumi wa kati wa maendeleo ya viwanda kna kupunguza umasikini ifikapo mwaka 2025.
Bw. Masawe alisema mafunzo hayo ambayo yameanza Novemba 16 yatachukua muda wa miezi mitatu mpaka kumalizika na wataalamu kutoka Japan ambao watakuwa wakitembelea kila kiwanda kwa muda wa siku saba.
No comments:
Post a Comment