Na Agnes Mwaijega, Dar es Salaam
KAMPUNI ya mawasiliano SASATEL imeshusha viwango vya gharama huduma ya mtandao wa internet kwa wateja wake.Akizungumza Dar es Saalam juzi Mkurungenzi wa
Masoko Sasatel, Bw. Derik Byarugaba alisema wameamua kupunguza viwango vya gharama ya huduma hiyo ili kuwapatia unafuu watumiaji wake ambao wanaongezeka siku hadi siku.
"Tumepunguza gharama za matumizi ya internet ili kuwapa unafuu wateja wetu ikizingatiwa kuwa dhamira kubwa ya kampuni yetu ni kuhakikisha Watanzania wanapata huduma ya mawasiliano kwa gharama nafuu," alisema Bw. Byarugaba.
Alisema punguzo hilo pia litawawezesha mteja mmoja mmoja na kampuni binafsi kupata huduma bora ya internet na kwa gharama nafuu.
Bw. Byarugaba alisema Sasatel imetoa ofa ya punguzo la bei kwa simu za mezani zenye uwezo wa kuunganishwa huduma za internet na kutuma ujumbe mfupi wa maneno ambapo simu hiyo inauzwa sh. 39000.
Aliongeza kuwa Sasatel imefanikiwa kujiimarisha katika utoaji wa huduma bora za mawasiliano ya simu na internet kwa wateja wake wote wa Mkoa wa Dar es Saalam na ina mkakati wa kusambaza huduma hizo kwa mikoa yote nchini.
Sasatel inasambaza huduma zake na kuboresha huduma za mawasiliano kwa msaada wa mfuko wa kuendekeza miundo mbinu, PME ambao ni mbia mkubwa wa kampuni hiyo.
No comments:
Post a Comment