01 December 2010

Wanaume watakiwa kuchunguza afya zao

Na Mwandishi Wetu

WANAUME wametakiwa kuwa na tabia ya kwenda kuchunguza afya zao kila mara ili kuepukana na ugonjwa wa saratani ya tezi dume ambao ukigundulika mapema kuna
uwezekano mkubwa ya kutibiwa na kupona.

Wito huo umetolewa na Mratibu wa Shirika la Saratani ya Tezi Dume nchini, Mchungaji Emmanuel Kandusi wakati akipokea msaada wa vipeperushi vyenye thamani ya sh. milioni 7.5 vinavyotoa ujumbe wa ugonjwa huo kutoka Benki ya NMB.

Mchungaji Kandusi alisema kuwa kampeni ya saratani ya eezi dume inapaswa kuungwa mkono na taasisi mbalimbali nchini ili wananchi waweze kufahamu madhara ya ugonjwa huo saabu zake.

"Saratani hii inasababishwa na vitu vingi ikiwemo lishe, umeme, urithi, upungufu wa virutubisho na umri," alisema mchungaji huyo huku akifafanua kuwa watu wenye umri wa miaka 50 na kuendelea wana nafasi kubwa ya kupata ugonjwa huo," alisema.

Kulingana na takwimu za mratibu huyo, ugonjwa huo unaua watu wengi, mfano mwaka 1990 uliua watu milioni 6 idadi ambayo ni kubwa kuliko watu wanaokufa kwa magonjwa ya Kifua Kikuu (TB) na UKIMWI.

Aliongeza kuwa mwaka 2020 saratani huyo isipothibitiwa itaua watu milioni 12, kati yao asilimia 75 wanaishi katika nchi zinazoendelea.

No comments:

Post a Comment