01 December 2010

Weil Bugando kuwa chuo kikuu kamili

Na Jovin Mihambi, Mwanza

CHUO Kikuu Kishiriki cha Sayansi ya Tiba, Weill Bugando, kimo mbioni kuwa Chuo Kikuu kinachojitegemea endapo mazungumzo kati ya uongozi wake na serikali
yatafanikiwa.

Mkuu wa chuo hicho, Profesa William Mahalu alisema hayo wakati wakati akitoa maelezo ya maandalizi ya mahafali
ya tatu ya chuo hicho, ambayo yatafanyika Jumamosi ambapo wahitimu 138 wa fani mbalimbali watapewa vyeti vya ngazi mbalimbali.

Alisema kuwa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) limeanza mazungumzo na serikali, ambayo yatawezesha chuo hicho Chuo Kikuu Kamili kinachojitegemea badala ya kuwa Chuo Kikuu Kishiriki cha Mtakatifu Augustine (SAUT).

Mazungumzo hayo yakikamilika, SAUT itakuwa na kitivo chake kipya cha tiba, ambacho kitakuwa Mahenge wilayani
Ifakara, mkoani Morogoro.

Kwa mujibu wa Profesa Mahalu mahafali hayo yatatanguliwa na kongamano ambalo litashirikisha maprofesa bingwa kutoka vyuo mbalimbali nchini kujadili mada mbalimbali zinazohusiana na mambo ya jamii pamoja na changamoto
ambazo zinavikabili vyuo vikuu vinavyomilikiwa na Kanisa Katoliki na jinsi ya kukabiliana nazo.

Mgeni rasmi katika sherehe hizo atakuwa Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Augustine, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza, Mhashamu Thaddeus Ruwa'ichi.

5 comments:

  1. Mwandishi naona Jografia ya Morogoro-Tanzania inakupita kushoto..Ifakara haipo Mahenge ipo Kilombero.Nomba muwe mnasoma atlas..Kama hapo hauna basi tumia hata mitando kupata ramani za sehemu husika.

    ReplyDelete
  2. Aliposema Mahenge alimaniisha Jimbo la Mahenge, yaani Mahenge Diocese, si Mahenge wilaya.

    ReplyDelete
  3. inahitajika kusoma pia kwa ugalifu habari kabla ya kutoa maoni. hongera sana

    ReplyDelete
  4. mwandishi unapoongelea majimbo ya kikanisa, usiweke wilaya za kiserikali. hapo umekosea. sema kipo ifakara ktk jimbo la kikanisa la mahenge, sio tu "Mahenge wilayani
    Ifakara". sio wasemaji wote ni wakatoliki!!!

    ReplyDelete
  5. Lakini mbona Prof William Mahalu sio Mkuu wa Chuo. Mkuu wa Chuo ni Prof. Mtabaji.

    ReplyDelete