01 December 2010

Wapangaji NHC wadaiwa bilioni 9/-

Na Peter Mwenda

SHIRIKA la Nyumba na Taifa (NHC) limetoa siku tisini kwa wapangaji wake wanaodaiwa kodi ya nyumba zinazofikia sh. bil. 9 walipe vinginevyo watachukuliwa hatua za kisheria.Mkurugenzi wa
Usimamizi wa Matawi na Utawala wa NHC, Bw. Raymond Mndolwa alisema jana kuwa shirika limechukua hatua hiyo baada ya kuona hakuna dalili za wapangaji hao kulipa kodi zao nyumba kwa zaidi ya miezi mitano.

"Kati ya sh. bilioni  9 tunazowadai wapangaji wetu, sh. bilioni . 7 ni wapangaji wa Mkoa wa Dar es Salaam tu, hao ni taasisi binafsi, taasisi za serikali, watu binafsi na mashirika," alisema Bw. Mndolwa.

Alisema NHC imetoa miezi mitatu ili wale wenye deni kubwa wandikiane mkataba jinsi watakavyolipa deni hilo kabla ya hatua nyingine kufuata kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.

Bw. Mndolwa alisema NHC imejipanga kuboresha huduma za wateja wao ambako kuanzia Januari mwakani bili za nyumba zitalipwa kupitia mabenki mbalimbali nchini na ofisi za shirika hilo tofauti na zamani zililipwa kupitia benki chache.

Alisema mikakati ya shirika hilo katika mkakati wa miaka mitano ijayo limejipanga kuboresha huduma zake na kujenga nyumba nyingine mpya ili kukabiliana na uhaba wa nyumba za kupanga.

"Wataalamu wetu NHC hawakai ofisini wamekwenda mikoa mbalimbali kutafuta viwanja vya kujenga nyumba 15,000 katika kipindi cha miaka mitano kukabiliana na uhaba wa nyumba nchini" alisema Bw. Mndolwa.

Alisema hatua nyingine ya kuboresha huduma za NHC ni kutumiwa ankara kupitia ujumbe mfupi (sms) ili wapangaji wasipate usumbufu wa kupata taarifa zinazowahusu.

2 comments:

  1. "Wataalamu wetu NHC hawakai ofisini wamekwenda mikoa mbalimbali kutafuta viwanja vya kujenga nyumba 15,000 katika kipindi cha miaka mitano kukabiliana na uhaba wa nyumba nchini" alisema Bw. Mndolwa".

    kuna low cost ambazo hali zake zinatisha sasa sijui mnahusika na ujenzi wa nje ya majengo pekee. Ndani ya majengo hayo yanatisha nyufa, mvua ikinyesha paa zinapitisha maji, paa za nyumba hizo zilishabomoka vipande zina mashimo kwa juu. kwa ujumla hazifai nyumba hizi siku moja mgefanya savei ya kuzicheki. BADALA YAKE BOMOENI HIZI MBOVU MJENGE MPYA! WAPANGAJI WENU WA ZAMANI WAPATE MALAZI BORA MAZURI. INAWEZEKANA NDI0 MAANA HAWATAKI KULIPA HIZO KODI ZENU!

    ReplyDelete
  2. Makazi bora, malazi bora, ambayo si hatarishi kwa wananchi.Paa tu la hasha hata kuta hazifai zina manyufa kibao wakazi wamefanya kuzuilia na mapipa ili watoto wao wasidondoke na kupoteza maisha. NHC BORESHENI HUDUMA ZENU SIO MNAJINADI KWA KUJENGA MAJENGO MENGI MAPYA WAKATI MENGINE YA ZAMANI YANAWASHINDA. NA HAYO NI MAJENGO YA MWAKA 47 JE HAYA MAPYA YANA UBORA KWELI NDANI YAKE? JE, YANA KIWANGO? KILA LA HERI NHC. BOMOA YA MWAKA 47 JENGENI MAPYA.

    ReplyDelete