22 November 2010

Wakala amtabiria Lukaku kukipiga England.

BRUSSELS, Ubelgji

WAKALA wa mchezaji, Romelu Lukaku anaamini klabu za England ndizo zitakazoshinda katika mbio za kumwania kinda huyo wa timu ya  Anderlecht.Kwa sasa mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka 17, ambaye anachezea timu ya taifa ya Ubelgji anawindwa na klabu nyingi kubwa za Ulaya, huku Juventus na AC Milan zikitajwa kukabana koo katika mawindo ya mshambuliaji huyo.

Hata hivyo wakala wa Lukaku, Christophe Henrotay alisema kuwa klabu za England, ndizo zimekuwa zikifanya jitihada kubwa za kunasa saini ya kinda huyo huku, Chelsea ikitajwa kuongoza katika mbio hizo.

Henrotay aliiambia tovuti ya calciomercatoweb: "Nafahamu Juventus na Milan zinamtaka mchezaji huyo, lakini si moja kwa moja na kwa sasa sijaona dalili zozote za kutaka kumalaiza suala hilo."

"Badala yake nchini England, nimekuwa nikipokea mawasiliano ya moja kwa moja na klabu kadhaa ambazo zimeonesha nia ya dhati kwa ajili ya kumtaka mchezaji huyu, lakini hata hivyo bado hatujafikia hatua ya mwisho ya majadiliano na timu yake ya sasa ya Anderlecht," aliongeza.

Alisema kumekuwepo na nia kwa baadhi ya klabu, lakini akasema itakuwa vigumu kumnyakua katika usajili wa Januari, kutokana na kuwa ni kati ya wachezaji bora kwa sasa.

No comments:

Post a Comment