21 November 2010

'Wabunge Chadema wamekosa uungwana'.

Na Andrew Ignas

MBUNGE wa Jimbo la Temeke kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw. Abbas Zuberi Mtemvu amelaani kitendo kilichofanywa na wabunge wa Chama cha Maendeleo (CHADEMA) wakiongoza
na kiongozi wao wa upinzani ambaye ni mwenyekiti wa chama hiyo, Bw. Freeman Mbowe  kutoka nje wakati Rais alipoanza kuhutubia Bunge Alhamis wiki hii.

Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi mbunge huyo alisema kwamba kitendo hicho hakikuwa cha uungwana bali ni utovu wa nidhamu. 

"Sijui wanafikiria nini jua hilo lakini hata kama wana madai yao hawakupasa kususia bunge kwani jana haikuwa siku husika ya madai yao," alisema Mtemvu.  

Alisema Bunge ni sehenu pa kuheshimiwa lakini viongozi wengine wanapachulia kama ukumbi wa mapambano na kwamba kwa jinsi hiyo hatuwezi kujenga nchi badala yake yatajengwa  makundi katika jamii. 

Hata hivyo Mbunge huyo amewataka viongozi hao wa CHADEMA kutafakari kwa makini juu ya kitendo hicho  na hatimaye kurekebisha kasoro zilizojitokeza.

Mbunge huyo alisema kwamba CCM imestaarabika na kwamba hata kama Dkt. Slaa angeibuka mshindi katika uchaguzi uliopita na kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wabunge wa CCM wasingeonesha utovu wa nidhamu wa kiwango hicho.

Alhamis wiki hii bungeni mjini Dodoma wabunge wa CHADEMA waliamua kunyanyuka na kutoka nje ya ukumbi mara tu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete alipoanza kuhutubia wabunge hao. 

3 comments:

  1. mbowe kaza uzi, usimsikilize mrema au maalim self, hao tako zamani ni ccm damu na nia yao kubwa si kuwakomboa watanzania bali ni kulilia madaraka, rejea mrema akimkampenia kikwete badala ya mgombea wa chama chake ingawa yeye ni mwenyekiti wa chama hicho NA AKIOMBA APEWE UWAZIRI WA MAMBO YA NDANI, au maalim self yeye ameshapewa umakam na sare ya suti ya ccm, sasa anaona eti kumgomea rais kikwete ni UHAINI!!JAMANI SIASA WEWE MAALIM SELF HATA UNAKUJA DAR UNAFIKIA IKILU HATA BILA KUFIKA BUGURUNI KUONANA NA NDUGU YAKO LIPUMBA!!!UMESAHAU JINSI WANA CUF WALIVOPIGWA RISASI!!
    KATIBA MPYA, TUME HURU YA UCHAGUZI NI LAZIMA,

    ReplyDelete
  2. Ni wazi watu kadhaa hawajaelewa lengo la CHADEMA, kwamba Kikwete siyo tatizo bali tatizo ni chombo kilichomfikisha yeye katika nafasi hiyo, na sheria kwenye katiba ya mfumo wa chama kimoja, inayomkinga kutobatilishwa katika ngazi ya uraisi. Kikwete kama Kikweli ni rafiki wa kila mtu, ila katika dhamana anayoibeba kuna maswali mengi ya kuuliza. Uongozi wake umekataliwa na Watanzania wengi baada ya kuona hakufanikisha yaliyotazamiwa na Watanzania jambo alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo.

    ReplyDelete
  3. Huyu Mh. Chiligati anatakiwa asiwe katika baraza la Mawaziri lijalo. Matamshi yake eti ya kuwafukuza Ubunge Wabunge wa CHADEMA,kwa vile walimgomea Rais, inaonyesha wazi kwamba huyu jamaa hana uelewa mzuri wa demokratia.Bado anatumia utendaji wa zamani wa chama kimoja, TANU!! Hata pale alipomtangaza Mbunge mtegemewa wa Nzega eti si Mwananchi,inathibitisha kabisa CCM ina watu wa ajabu!!

    ReplyDelete