18 November 2010

Waandishi watakiwa kuwa na huruma.

Na Mwandishi Wetu

WAANDISHI wa Habari wameobwa kuwa na huruma na kuacha kuwanyanyapaa wanamichezo wanaoshindwa kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa kwa
kuwaita 'watalii wa Tanzania warejea na mabegi yao.'

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Idd Kipingu alisema kauli hizo za waandishi wa habari  zinawanyong'onyeza wanamichezo kwa kuwa hata wanapofanya vibaya, aibu ni ya nchi nzima na si ya wachezaji pekee.

"Ninyi waandishi msiwanyanyapae wanariadha, maana hao ndiyo mara nyingi mmekuwa mkiwaita watalii na pia wanamichezo wa michezo wengine wanapofanya vibaya, jaribuni kutafuta chanzo na sababu mnaweza hata ikawa ni msaada mkubwa kwa Serikali kupitia kalamu zenu," alisema Kipingu.

Alisema kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa ni kazi ya ujasiri kwa kuwa, mchezaji anakuwa amebeba mzigo wa nchi nzima na kwamba hata pale wanapofanya vibaya si kuwa walipenda ila ni kutokana na sababu ambazo zinasababishwa na vyama ama serikali.

Kipingu alitoa changamoto kwa waandishi wa habari kukosoa na kufichua shule, ambazo hazina michezo na si kungojea wanamichezo wanaorudi kwenye michuano ya kimataifa na kuwaita watalii.

No comments:

Post a Comment