Na Elisante Kitulo
ALIYEKUWA mgombea ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Ali Mleh ametangaza dhamira ya
kufungu akesi mahakamani kupinga matokeo ya ubunge jimboni humo, yaliyompa ushindi Bw. Peter Serukamba wa CCM.
Akizungumza na Majira kwa njia ya simu jana, Bw. Mleh alisema amepanga kufungua kesi hiyo Mahakama Kuu Kanda ya Kati Tabora jumatatu.
Bw. Mleh analalamikia mwenendo mzima wa uchaguzi jimboni humo hadi kutangazwa kwa matoko hayo.
Alisema kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa sheria na taratibu za uchaguzi kwa baadhi ya maofisa wa uchaguzi jimboni humo.
"Unajua mchakato mzima wa ukusanyaji, ujumlishaji na utangazaji wa matokeo umekiuka sheria za uchaguzi," alisema.
nenda kila la kheri , kama haki ni yako utapata tu
ReplyDelete