23 November 2010

Ujerumani kusomesha watoto masikini.

Na Andrew Ignas, Dar es Salaam.

TAASISI  isiyo ya Kiserikali ya Ujerumani   ijulikanayo kwa jina la Pamoja kwanza imetenga zaidi ya sh. bilioni 1 kwa ajili kumalizia ujenzi wa shule ya watoto wasio na uwezo unaoendelea maeneo ya
Kimara Bonyokwa, Mbezi.


Akizungumza na mwandishi wa Majira Dar es Salaam jana Msemaji wa shirika hilo, Bi. Carolina Litcher alisema shirika hilo
limetenga fedha hizo kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa shule itakayokuwa ikitumika kwa watoto wa walala hoi.


"Kwa kutambua umaskini unaoikumba familia nyingi za Watanzania ukiwepo na kutokuwa na elimu ndio maana tumeamua kukamilisha ujenzi huu kwanza ili kwa wale watoto wasio na uwezo kusoma bure," alisema Bi. Ritcher.


Alisema pia mpaka sasa wamepata jumla ya watoto 68 ambao ni wa ngazi ya sekondari mpaka chuo kikuu kutoka mikoa tofauti  ambao wanawalipia karo za shule sambamba na fedha za nauli ikiwemo na chakula.



Aidha kwa upande mwingine Mfadhili huyo amewataka wanafunzi hao kutumia muda mwingi kwa kusoma ili kuwapa moyo zaidi wahisani hao wa kuwasaidia maskini
badala ya kutupa fedha zao.

No comments:

Post a Comment