19 November 2010

Ujenzi wa nyumba kwa siku moja wazinduliwa.

Na Peter Mwenda

TATIZO sugu la ukosefu wa makazi nchini limepata ufumbuzi baada ya kampuni ya Moladi Framework ya Afrika Kusini kuzindua teklonojia mpya ya ujenzi wa nyumba za
gharama nafuu na muda mfupi.

Mgunduzi wa teknolojia hiyo, Bw. Henrick Botes alisema  Dar es Salaam jana kuwa ujenzi huo ambao aliugundua mwaka 1986 nchini Afrika Kusini, unatumia gharama ndogo na muda wa siku moja kumalizika.

Akionesha ujenzi huo katika nyumba iliyojengwa eneo la Wazo Hill Dar es Salaam jana, Bw. Botes alisema wanajenga ukuta kwa kutumia saruji na mchanganyiko ya vitu vingine ambayo ukuta wake unakauka baada ya saa nne.

Bw. Botes alisema kabla ya kumimina saruji hiyo njia za umeme, mabomba ya maji, fremu za majidisha, milango zinakuwa zinawekwa na baadaye siku ya pili makasha yanayosimamia ukuta yanaondolewa na kupachika madirisha, kupiga bati na kumalizia marumaru.

Alisema ujenzi wa nyumba yenye vyumba vitatu, sebule, choo na jiko hugharimu sh. mil. 20 bila kuingiza gharama za marumaru, madirisha ya kisasa na mabati ya thamani kubwa.

Bw. Botes alisema nyumba ambayo imewekwa marumaru na vitu vingine vya kisasa inagharimu sh. mil. 40 hadi mteja kukabidhiwa nyumba yake kuishi.

Alisema Kampuni ya Moladi Framework imefanikiwa ujenzi huo katika nchi za Zambia, Ghana, Zimbabwe, Angola, Botswana, Msumbiji, Nigeria na Afrika Kusini.

Alisema kampuni yake ya Moladi imefungua tawi nchini na mkandarasi aliyeteuliwa kwa sasa ni kampuni ya Holtan ya jijini Dar es Salaam.

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Moladi Framework nchini, Bw. Abeid Abdallah alisema kampuni yake ambao ni wakala pekee imedhamiria kutoa ufumbuzi wa uhaba wa makazi kwa kutengeneza nyumba kwa kutumia muda mfupi.

13 comments:

  1. Mnaandika habari za nyumba ambayo hata picha yake hamjaiweka.
    huu ni upungufu mkubwa, hebu rekebisheni

    ReplyDelete
  2. Hamajeleza kamba zinauzwa zinakodishwa au kukopeshwa, tunaomba ufafanuzi zaidi.

    ReplyDelete
  3. pETRO eUSEBIUS mSELEWANovember 19, 2010 at 8:40 AM

    Hii teknolojia nzuri ila kwa hali yetu watanzania wengi nyumba hizo watajengewa akina fulani tu.sisi waje kutujengea sizizo na marumaru wala simenti.hizo ndo zetu.

    ReplyDelete
  4. Hizo nyumba watawajengea mafisadi CCM na wachachuaji wa kura. Mtanzania wa kawaida hatamudu hizo shiling milioni 20 au 40. Ukisoma taarifa ya UNDP ya juzi utaona jinsi watanzania walio wengi ni masikini wa kutupwa kabisa. Kwa wantanzania hawa hii habari kwao ni kama ndoto ya kimweri.

    ReplyDelete
  5. Makampuni na Mashirika ya Umma yanatakiwa kuingia mikataba na wafanyakazi wao wajengewe na kupatiwa hizo nyumba kwa kukatwa kwa miaka 10 ili maisha bora kwa kila mtanzania yatimie. Mafisadi tatizo lao watajiingiza na kuanza kuwatoza watanzania pesa nyingi. Wakati huu watanzania wameamka, ni jukumu la watanzania na wafanyakazi wanaoliingizia taifa pesa nyingi kupwa fusa ya kujengewa nyumba hizo. Wapo Waajiri wengine hawana hata habari za wafanyakazi wao, wanajilipa wao pesa nyingi za nyumba lakini wafanyakazi walio chini yao wanaaimbiwa hawana sifa za kulipwa wakati walikuwa wanalipwa enzi za Mwalimu. Ufisadi hadi Mashirika ya Umma upo sana, wao wanalipana fedha nyingi lakini wengine eti hawana sifa, je walale wapi juu ya miti au wapi? Serikali iangalie wananchi na wafanyakazi wa chini wapatiwe huduma hizo kwa mikopo.

    ReplyDelete
  6. oya anonymous wa kwanza nakuomba tembelea blog ya michuzi www.michuzi.blogspot.com utaona picha halisi ya picha hizo.
    Mdau J.ng

    ReplyDelete
  7. hizo hata watanzania wanaweza kujenga mataprli tu,hapo kuna ulaji,halafu tunasema hakuna ajira,wakati ajira munawapa nchi kutoka njee ...pili hizo nyumba za nani ? mi nafikiri mutajenga nyumba tanzania nzima na watu haziwatoshelezi,boresheni elimu na afya,elimu ondoeni vikwazo kila mtu asome hata mlemavu nae ajue kutengeza computer...nyumba itakuja wenyewe atakapo jiajiri..

    ReplyDelete
  8. Badala ya kuleta vitu vya uhakika nchini mnataka kufunika wananchi kwa kifusi cha nyumba. Mmeona dili la mvua za mabomu limekwamba mmeona nyumba za chapchap ni dili. Hebu punguza bei ya saruji mie nijenge nyumba ya uhakika. Nyumba vimeo, simu vimeo, magari vimeo, dawa vimeo, nguo vimeo na maziwa vimeo. Tumekwisha! Nchi gani isiyokuwa na speed governer!

    ReplyDelete
  9. ANTONY

    Milioni 20 ni ngarama nafuu? Kwa akina Yusuf Manji au Mtanzania wa kawaida! Mimi ukinipa hizo mbona najenga nyumba ya block ya vyumba 8.

    ReplyDelete
  10. Jamani nafikiri tungejua kwanza uimara wa nyumba zenyewe hapo ndo tungeongea zaidi.Ninavyojua,naungana na Antony milioni 20 ni gharama ndogo sana.Ieleweke kwamba unaesema kwa kiasi hicho wawezajenga nyumba ya block ya vyumba 8,hizo labda ni block za matope mfuko mmoja wa kilo 50 kwa matofari 100.Ujenzi wa Ki-Tz hatujui kuhesabu/kuweka kumbukumbu za gharama wewe jaribu mwulize mtu yeyote aliye na nyumba nzuri umetumia kiasi gani kujenga nyumba hii?atakuambia niliacha kuandika maana gharama hizo zinaumiza sana sana utaambiwa gharama za bati na vioo na fremu za madirisha mimi mwenyewe sijui jumla ya gharama maana fundi akuibie mara leo hajaja kujenga lakini pesa kala unabadilisha fundi mwingine.Ushauri wangu SERIKALI ifuate utaratibu wa nchi zilizotajwa kujenga nyumba hizo je wananchi wamewezaje kulipa?najua ni kwa mikopo ya muda mrefu zaidi ya miaka 10 ujue hicho "Anonymous"ulisema miaka kumi kulipa 40mil.Wa-TZ tuache hofu Mungu ametuona ni ukombozi tosha,tuibane serikali iingie mkutaba na hawa jamaa.

    ReplyDelete
  11. Nadhani huo ni utani mnafanya,tunashindwa kupata picha nyumba hiyo ikoje.kwa sababu hakuna picha wala mchoro.

    ReplyDelete
  12. duuh hii nayo technology but tuangalie tusije jenga kwa siku moja then ikabomoka ndan ya mwaka mmoja

    ReplyDelete
  13. si watuonyeshe hiyo mifano na uimara wake, pia guaratee yake ni ya miaka mingapi kabla ya kuhakikisha ni imara?

    ReplyDelete