15 November 2010

Uchaguzi wa amani, watu wachache Mpanda.

Na Juddy Ngonyani, Mpanda

UPIGAJI wa kura katika vituo 202 vya majimbo ya Mpanda Mjini na Mpanda Vijijini mkoani Rukwa limefanyika katika hali ya utulivu huku baadhi ya vituo kukiwa na
mwitikio mdogo wa watu kujitokeza katika zoezi hilo.

Kwa upande wake karani mwongozaji wa kituo cha kupigia kura cha Paradise kilichopo katika Kata ya Kashauriri wilayani Mpanda, Bw.  Didadi Nguo amesema kuwa zoezi hili katika kituo chake linaendelea vizuri.

Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Mpanda Vijijini lenye jumla ya vituo 94 vya kupigia kura, Mhandisi Emmanuel Kalobelo alisema kuwa zoezi hilo lilitarajia kuisha kwa utulivu.

Jimbo hilo la Mpanda Vijijini lina jumla ya watu 35,911 waliosajiliwa katika daftari la kudumu la wapiga kura huku likiwa na jumla ya wagombea wawili wa ngazi ya ubunge ambao ni Bw. Moshi Seleman Kakoso wa CCM na Bw. Masanja Mussa wa CHADEMA.

Msimamaizi wa uchaguzi jimbo la Mpanda Mjini Bw. Henry Haule alisema kuwa jimbo hili lina jumla ya watu 42,215 walioandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura na likiwa na jumla ya wagombea watatu ambao ni Bw. Said Amour Alfi wa CHADEMA, Bw. Sebastian Simon Kapufi wa CCM na Bw. Aron Ndimubenya wa CUF

Hali ya ulinzi na usalama imehimarishwa katika kila kona ya majimbo hayo ya uchaguzi, kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, Bw. Isunto Mantage.

3 comments:

  1. hofu kubwa ya watu kupiga kura ni kwamba kura zao hazina maana kabisa.hapa namaanisha kuwa hata wamchague nani wampendaye,msimamizi wa uchaguzi aweza kumtangaza ampendaye.huu ndio ukweli.sa hautaki?

    ReplyDelete
  2. Petro Eusebius MselewaNovember 15, 2010 at 10:19 AM

    hiyo ni kweli.hata pale kwetu mambo yalikuwa hivyohivyo.ukisema unatafutwa.mara nyingi hujiuliza swali:hivi msimamizi wa uchaguzi ana kura zake anazopiga kwenye chumba cha kutangazia matokeo? iweje basi pawe na tofauti kati ya jumla ya kura za kituo baada ya kituo na ile jumla aotangazayo? hivi hapa ukisema kuna 'uchakachuaji' utatafutiwa nini? ndo nimeshasema sasa....nitafuteni.

    ReplyDelete
  3. kwa kweli watu wamepungua moyo sana si kwenye jimbo la mpanda tu hata urais kiujumla we jiulize wat 20m wamejiandikisha na waliopiga kura 8m hao 12m wapo wapi??? watu wamechoka maana wanajua hata wakimchagua mtu wamtakao hatakuwa....

    ReplyDelete