15 November 2010

TETESI BARAZA LA MAWAZIRI:Lowassa atajwa kulilia Tamisemi.

*Yeye asema tuyaache hayo, ni uvumi usio na msingi.

Na Tumaini Makene.
WAKATI Watanzania wakisubiri kwa hamu Baraza la Mawaziri la Rais Jakaya Kikwete litakalomsaidia kuongoza serikali katika ngwe yake ya mwisho, habari zimevuja zikimhusisha Mbunge wa
Monduli, Bw. Edward Lowassa na mikakati ya kukwaa moja ya wizara nyeti katika serikali mpya itakayoundwa na rais siku chache zijazo.

Bw. Lowassa ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu katika serikali ya Rais Kikwete kabla hajajiuzulu kufuatia kashfa ya Richmond iliyopewa zabuni ya kuzalisha umeme kinyume cha taratibu, anatajwa katika mikakati ya kuteuliwa waziri katika wizara itakayohusika na tawala za mikoa na serikali za mitaa.

Katika Serikali zilizopita ikiwamo ile ya awamu ya kwanza ya Rais Kikwete wizara hiyo ilikuwa ikijulikana kwa ufupisho kama TAMISEMI (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), na inaelezwa kuwa ni nyeti inayompa waziri fursa ya kuwa karibu zaidi na wananchi.

Vyanzo vya habari vilivyo karibu na duru za michakato inayoendelea serikalini juu ya uteuzi wa nafasi mbalimbali hususan zile za kisiasa, vimeliambia Majira kuwa upo msukumo mkubwa kutaka Bw. Lowassa ateuliwe katika nafasi hiyo kwa mustakabali wake kisiasa, hususan katika uchaguzi mkuu wa 2015.

Pamoja na kutoa taarifa hizo, watu hao walio karibu na Bw. Lowassa waliliambia Majira kuwa huenda yeye (Lowassa) hahusiki katika mikakati ya kuzishawishi mamlaka zinazohusika na uteuzi wa mawaziri, kumteua katika nafaii hiyo nyeti, lakini upo msukumo wa wazi kutaka hivyo.

Majira lilipomtafuta Bw. Lowassa juu ya tetesi hizo, alijibu kuwa yeye hajui lolote wala hajasikia kitu kama hicho.

"Sijui lolote wala sijasikia lolote kuhusiana na hicho unachokisema, tuyaacheni kwanza hayo mambo, la sivyo tutakuwa tunazungumzia speculations (tetesi, uvumi) bila sababu yoyote.

"Nasisitiza kuwa sina taarifa zozote kutoka mamlaka za uteuzi, sijasikia kitu kama hicho, ni speculations ambazo hazina maana yoyote ile," alisema Bw. Lowassa ambaye amekuwa swaiba wa karibu wa Rais Kikwete, kikazi na kimaisha, kwa muda mrefu.

Kabla ya kupatikana kwa habari hizo zikimhusiaha Bw. Lowassa na uteuzi wa waziri wa TAMISEMI, kulikuwa na tetesi zilizokuwa zikimtaja kuwa mmoja kati ya watu ambao wangeweza kuteuliwa tena katika nafasi ya waziri mkuu, lakini wadadisi wengi wamesema kuwa itakuwa ni vigumu kutokana na ukweli kwamba Bw. Mizengo Pinda bado ana nafasi kubwa ya kuendelea na Rais Kikwete kumalizia ngwe yao ya mwisho.

Uwezekano wa Bw. Pinda kuendelea na nafasi hiyo ya uwaziri mkuu umeelezwa kuwa ni mkubwa kutokana na uadilifu wake, kutokuwa mtu wa makundi ndani ya CCM na serikalini,  akielezewa kuwa hapendi matumizi makubwa ya fedha za umma, huku pia akiwa hajawahi kukumbwa na kashfa yoyote, hali ambayo inamfanya akubalike kwa kadri upepo wa kisiasa ulivyo nchini kwa sasa.

Vyanzo vya habari vilivyo karibu kikazi na mbunge huyo wa Monduli, vimesema kuwa hali hiyo ya nafasi ya uwaziri mkuu kuonekana 'imejaa' ndiyo imeelezwa kuwa sababu ya Bw. Lowassa kutajwa katika uteuzi wa wizara nyeti ya TAMISEMI.

Pamoja na kuwa wengi wamekuwa wakiichukulia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, kuwa ndiyo moja ya wizara nyeti nchini, maarufu kama 'njiapanda ya ikulu', baada ya kumtoa Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa na Rais Kikwete, bado unyeti wa TAMISEMI katika utawala wa nchi haukwepeki kutokana na ukweli kuwa ndiyo wizara yenye mtandao mkubwa ndani ya nchi, ikiwa ni kiunganishi kati ya serikali kuu na serikali za mitaa.

Waziri wa wizara hiyo ambayo mara nyingi imekuwa ikiwekwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, ikiwa pamoja na ile inayohusika na maafa na utaratibu wa bunge, ameelezwa kuwa ana afasi pana zaidi ya kukutana na wananchi wa kada mbalimbali katika shughuli mbalimbali za maendeleo zinazogusa maisha ya kila siku ya Watanzania, hasa wale wapiga kura.

TAMISEMI inaonekana kuwa ni wizara mtambuka, ikielezwa kuwa ni kiungo muhimu kati ya wizara za kisekta na asasi mbalimbali za Serikali za Mitaa. ikiwa na jukumu la kuhakikisha yanajengwa mazingira mazuri ya kuwezesha ushirikishwaji wa umma katika kujiletea maendeleo, kwa kuzingatia utawala bora.

Kwa mujibu wa mkataba kwa wateja wa wizara hiyo, kulingana na mpango uliopo sasa wa uboreshaji wa huduma kwa umma, TAMISEMI inategemewa kuongoza na kuwa kiungo kati ya mpango wa uboreshaji wa mfumo wa Serikali za Mitaa na Mpango wa Uboreshaji wa Wizara za Kisekta unaofanywa na sekta mbalimbali ngazi ya Taifa.

Katika kuonesha unyeti wa wizaya hiyo, mkataba huo unaeleza kuwa TAMISEMI ina wajibu wa kuratibu na kusimamia tawala za mikoa ili ziweze kuzisaidia halmashauri katika kutekeleza wajibu na majukumu yake; kutayarisha na kusimamia sera ya maendeleo vijijini; kusimamia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo Mijini; kuendeleza programu ya uboreshaji wa mfumo wa Serikali za Mitaa nchini ili ziweze kutoa huduma bora.

Majukumu mengine yametajwa kuwa ni kuzijengea Serikali za Mitaa uwezo wa kusimamia mapato na matumizi; kuboresha miundo, hali ya watumishi na mifumo ya kazi ndani ya TAMISEMI, mikoa na halmashauri; kusimamia asasi, mashirika ya umma na miradi inayotekelezwa chini ya wizara hiyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (OWM), kuratibu utekelezaji wa shughuli za hifadhi ya mazingira katika Serikali za Mitaa na pia kuratibu vita dhidi ya rushwa na UKIMWI.

Tangu kujiuzulu kwake uwaziri mkuu kwa kashfa ya Richmond, akiwa waziri mkuu wa kwanza kufanya hivyo nchini, mapema Februari 2008, Bw. Lowassa amekuwa kimya katika masuala mengi ya kitaifa, suala ambalo limekuwa likielezewa na wachambuzi wa mambo kuwa ni mkakati wake wa kisiasa kurudi katika uringo wakati mwafaka ukiwadia.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa waliozungumza na Majira, vikiwemo vyanzo hivyo vya habari, wamesema kuwa nafasi hiyo ya uwaziri wa TAMISEMI, utampatia nafasi nzuri Bw. Lowassa kurudi katika chati ya kisiasa hata kubadili upepo wa kisiasa hasa nje ya CCM ambapo imeelezwa kuwa umekuwa haumwendei vizuri, tangu alipoondoka serikalini.

Hivi karibuni, katika uchaguzi mkuu uliopita, mbunge huyo wa Monduli, alijipatia ushindi wa kishindo na kumshinda kirahisi mgombea wa CHADEMA, Mchungaji Amani Silanga. 

32 comments:

  1. LOWASA NI MCHAPAKAZI TATIZO NI ZILE KASHFA ZA RICHMOND ILA ANAFAA KABISA KUWA KIONGOZI. ANACHOTAKIWA KUFANYA NI KUTUBU KWELI NA KUOMBA RADHI KWA WANANCHI ILI TUMSAMEE NA ARUDISHE MALI KAMA ALIZURUMU. NI MFATILIAJI MZURI WA MALALAMIKO YA WANANCHI NA MTATUZI WA MIGOGORO NA ANAPENDA MAENDELEO ZA WIZARA ANAZO ONGOZA. LAKINI KINACHO MKWAZA NI HASIZA ZA ARAKA NA KUWA NA MARAFIKI WANAOMPOTOSHA KAMA ROSTAM AZIZ.

    ReplyDelete
  2. Hivi ni kweli watanzania mnaamini kuwa bila Lowasa serkali haiwezi kuwepo au Kikwete hawezi kuongoza? Lowasa ataishi milele? Kikwete aache kabisa kuunda baraza la mawaziri la kishikaji namshauri ajari taaluma na utendaji bora wa mteuliwa. Mambo ya kulipana fadhila yatamfanya adharauliwe hata na hao atakao wateua kwa mizengwe.

    ReplyDelete
  3. Petro Eusebius MselewaNovember 15, 2010 at 10:25 AM

    Lowassa acha sifa.Sisi bado tunatafakari adhabu ya kukupa siku yoyote ile.Yaweza kuwa nzuri kuliko hicho cheo.Kama wataka cheo,subiri tusahau kwanza basi kama kawaida yetu.Ukitukumbusha...utaishia na Ubunge wa Monduli hadi unakufa.Kosa kubwa kwa sasa ni kupata cheo za kuteuliwa sehemu yoyote ile isipokuwa Umasaini.

    ReplyDelete
  4. Akipewa Lowasa Kikwete atakua hajautendea haki umma kutokana na tuhuma zilizomkabili! Mwache ampe Pinda lakini kwetu sisi wazanzibari Pinda bado hatuingii akilini tangu aliposhika kusema Zanzibar si nchi na juzi uwanja wa amani kakiona wananchi walimwimbia kua Zanzibar ni Nchi, asikie vizuri masikioni mwake!

    ReplyDelete
  5. UCHAPA KAZI HAUNA TIJA KAMA EL SIO MWADILIFU TUNATAKA JK AWATEUE WATU WACHAPA KAZI, MAKINI NA WAADILIFU KATIKA UTENDA KAZI

    ReplyDelete
  6. Ni mzee wa biashara. Biashara na uongozi wa kusimamia mali za umma vinakinzana.

    ReplyDelete
  7. Ni wazi Lowassa alipata ajali ya kisiasa kama JK alivyosema wakati fulani. Naamini tunahitaji viongozi wenye kuthubutu kama Lowassa. Tatizo la baadhi ya Watz wanafata mkumbo na kutaka viongozi wanaosinzia sinzia, wasiothubutu ili wasiwaudhi watanzania, hatudanganyiki Lowassa anatosha. Hata Mzee Mwinyi alipata ajali ya kisiasa na akaja akawa kiongozi. Mnyonge Mnyongeni lakini haki yake mpeni. JK akiona inafaa ampe wizara, jamani tuache ushabiki usiotusaidia.

    ReplyDelete
  8. Kama wangejua Yesu ni MUNGU,wasingemsulubu...naona sijaeleweka,I mean,wasiopenda Lowassa awepo serikalini wanasumbuliwa na madhambi yao na wanajawa hofu sana kila wakisikia jina lake!!!

    ReplyDelete
  9. LOWASA WA NINI HUYO AMESHACHUJA TUSIPENDE KUTUMIA MAJIBU YA ZAMANI KWA MASWALI MAPYA YAANI HAKUNA WANACCM WENGINE WANAOWEZA KUWA MAWAZIRI HADI LOWASA UKISHINDWA WACHUKUE WAUPINZANI UWAPE NAFASI HIYO SIYO FISADI LOWASA,URAFIKI KATIKA KUJENGA NCHI HAUFAI.

    SAMWEL ELIAS

    ReplyDelete
  10. Najiuliza hivi wasomi Tanzania ni akina Lowasa Tu????? Kwanini Serikali haitizami wananchi wanasemaje, Ukidharau mwiba ????????? Hata Kenya KANU ilianza kufa taratibu Kama hii CCM inavyo anza kufa taratibu. Kwa upinzani bara chama kimoja kupata wabunge 53 ni mwanzo wa sisiem maarufu chukua chako mapema kufa. Inakuaje Serikali kuwa rehani (kwenye mikono ya mafisadi?? wanachotaka wao ndicho kifanyike?? kampeni mbaya kwenye majimbo wamefadhili na mambo chungu tele.

    Ole wenu watanzania munao fumbia macho mambo haya ole wenu muliomadarakani munao beba mambo haya. Sikumoja mutaikimbia nchi au kuwa akina Albashiri.

    ReplyDelete
  11. mimi naona ni mapema mno kutoa hukumu kwa jambo amabalo hakuna mwenye uhakika kuwa ni kweli amechaguliwa tena, hata iwe ni kweli yeye ni binaadamu kama ni binaadamui wengine na kitendo cha kujiuzulu kwa makosa ya watu wengine ni kitendo cha kishujaa kwani tunaona wanasiasa amabao wabaona ni bora damu kumwagika lakin wao wapewe uongozi kwake ni tofauti tumpeni nafasi

    ReplyDelete
  12. Jamani tuache utani. Lowasa alikuwa Waziri Mkuu. Leo iweje awe waziri wa TAMISEMI? Kwanza muelewe kuwa wananchi hawana tena imani naye japo mnasema ni jasiri na mchapakazi. Wapo wengi wachapakazi na wenye uwezo mkubwa kupewa wizara nyeti kama TAMISEMI. Lowasa achape mwendo na huko umasanini wanakomwabudu kwa kuwa hawana elimu ya kutosha. JK akimpa uwazir umma utamshangaa kuliko maelezo.

    Faith Mtokambali.

    ReplyDelete
  13. CCM na serikali yake inatakiwa ifungue milango yake ya fahamu na kutambua kuwa wananchi wanaona na maamuzi yao yanatokana na yale wayaonayo,kupeana vyeo kwa uswhiba kutaiharibia CCM.JK ikifanya hivyo tutajua kuwa yote anayokemea ni kiini macho.please mr President !!! WATU WANAONA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  14. Aachana na tetesi, baraza la mawaziri halijatangawa mmeanza tetesi za Lowasa, please mr President!!! kufanya kosa si kosa, lakini kurudia kosa ni dhambi kubwa sana.

    ReplyDelete
  15. Inatosha LOWASA alivyotuhudumia watanzania. tumeona uwezo wake na mwelekeo, msimamo wake kwa watanzania. Wapewe watanzania wengine wenye uwezo. ninaamini wapo. Tunataka serikali ya watu waadilifu wasio na uchu wa madaraka. President,PLZ, watu wenye sifa zaidi ya lowasa wapo, na wachapa kazi, tunataka wapenda maendeleo kwa kujali maskini, kuwawezesha watanzania sio hao waweke mali kwa ajili ya familia zao.

    ReplyDelete
  16. Jamani watanznia kweli tutafika????? Hiii balaaa, kweli itasikitisha sana kama kweli Lowasa ambeye bonge la fisadi atapewa uwaziri wa TAMISEMI mbona watanznia tutaangamia kabisa,je ccm hakuna wasomomi wengine wenye ujuzi wa nafasi hiyo.huyu Losawa muda wake wa kutufilisi umeshakwisha tunaomba aongoza jimboni kwake hicho cheo cha ubunge kina mtosha huyo fisadi, hafai kuwa waziri tena

    ReplyDelete
  17. Heri waziri mkuu awa Salma, Rahma au Ridhiwani kama upuuzi wenyewe ni huu. Kikwete amefilisika kiakili kuliko yeyote aliyewahi kukalia kiti alichokalia. Ni pigo na aibu kwa taifa kuwa na rais mwenye mawazo mfu na mipango haba kama Kikwete kaliza apendaye kuitwa Daktari wakati hana lolote.

    ReplyDelete
  18. Speculation to the fullest,speculation in its full mouth...Watanzania kwa umbea wamezaa hadi wana wambea,na wasomi wetu nao ndo sasa wanaongoza kwa umbea!!!

    ReplyDelete
  19. Anon wa novemba 15,2010 6:51 AM pole, tena nakupa pole mara ya 2, na ya 3. Kisha nakushauri wahi hospitali ukatibiwe haraka. Kwanini nasema hivyo, kwanza Rais haundi serikali yeye peke yake, anapelekewa cv za na proposals, pili hizo umeambiwa ni tetesi tu yaani ni speculations au redio mbao. Sasa maneno yote ya hasira na kashfa yanayoonyesha chuki na ghazabu zako yanini?

    Unahitaji msaada wa daktari kukuondoa stress na depression uliyonayo. Angalizo, wivu ukizidi ukichanganya na chuki vinaleta TB!

    ReplyDelete
  20. WOTE MLIOTOA COMMENTS I CANT HO! MLIVYOKUWA MKIWAIMBIA MAJUKWAANI WAKATI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI HAKUJUA WANGETAWALA VIPI? MLIVYOKUBAKI KUVAA ZILE NGUO ZA KIJANI NA NJANO HAMKUJUA YANGETOKEA NINI? MLIVYOWAPIGIA KWA KURA ZENU HAMKUJUA KUWA WANGEGAWANA MADARAKA? LEO MNAANZA KULALAMIKA!! MWACHENI LOWASSA AWE TENA HATA WAZIRI MKUU! HII NDIYO CCM MNALYOIPENDA!! CCME OYE!! MAFISADI OYE!!, KANDAMIZENI HII MITANZANIA ISIYOWEZA KUONA MBELE. WATANZANIA HATUNA HAKI YA KULALAMIKA WALA KUMLAUMU RAIS TULIYEMPANDIKIZA KWA KURA ZETU WENUYEWE!!
    MDAU ROMA, ITALIA.

    ReplyDelete
  21. mi nashangaa waazania weengi mnapomtupia lawama lowasa.kila kukicha LOWASA. TAFAKARINI SANA KABLA HAMJALAUMU JUU YA LOWASA.KWA WALE WASOMJI WA BIBLIA,MAFARISAYO WALIMPELEKA MWANAMKE MZINIFU KWA YESU ILI AMHUKUMU.YESU AKAWAAMBIA HAO MAFARISAYO ALIYEMSAFI AU ASIYEWAHI KUTENDA DHAMBI,AWE WA KWANZA KUMTUPIA MWANAMKE HUYU JIWE.YESU KUINAMA NA KUINUKA WALE MAFARISAYO WOTE WAMESHATAWANYIKA KWA KUWA WALIJUA FIKA KUWA WOTE WALIWAHI KUTENDA DHAMBI HIVYO HAKUNA HATA MMOJA ALIYESAFI KATI YAO.YESU ALIMWAMBIA KITU KIMOJA TU YULE MWANAMKE,NENDA ZAKO USITENDE DHAMBI TENA.NINACHOWAAMBIA WATANZANIA WOTE KUWA NI MTANZANIA YUPI ATAINUA JIWE KUMTUPIA LOWASA KWA YALE MNAYOMTUHUMU?TENA KWA MENGINE MSIYOKUWA NA UHAKIKA NAYO?KILA MTU ANA MAPUNGUFU YAKE KAMA BINADAMU.TAFAKARINI NI MANGAPI MAZURI LOWASA KAITENDEA NCHI HII.MNASAHAU ALIVYOKWENDA KUPIGANA NA WAARABU KUHUSU MAJI YA MTO NILE HADI HIVI SASA SHINYANGA WANAFAIDI KAMA WAKO PEPONI,MASAHAU ALIVYOWAFUKUZA WAHINDI WA DAWASCO?MNASAHAU LOWASA ALIVYOSIMAMIA SHULE ZA SEKONDARY MPAKA SASA HIVI WANAZIITA SHULE ZA LOWASA.
    TATIZO SISI WASWAHILI TUNAFUATA MKUMBO NA USHABIKI WA KISIASA.KAMA ANGEKUWA FISADI KIHIVYO MNAVYODAI JK ANGEMWACHA? TAKUKURU INGEMWACHA?MSICHOKIJUA MSISEMESEME. MI NASEMA LOWASA NI MCHAPA KAZI NA ANADHUBUTU KUFANYA YALE AMBAYO BAADHI YA VIONGOZI WALIO WENGI WA SASA HIVI WA TANZANIA HAWADHUBUTU. MPENI LOWASA NAFASI TENA MWONE KAZI YAKE. MMASAI HAKOPESHI HATA KAMA ANA DAMU YA KIMRERU.NI KIONGOZI IMARA ANAYEDHUBUTU NA NDIYO VIONGOZI TUNAOWATAKA KWA SASA HIVI TZ.

    ReplyDelete
  22. Lowasa Lowasa...what kind of a leader who involved himself in so many dubious scandals?????? Loliondo, aArdhi, AICC, RICHMOND,EPA, Meremeta and still there are people with courage to defend him??? Those scandals matter. Caesar's wife must be above suspicion. When the newspapers reported the rumor, perliament committee mentioned him he resigned he had failed to pay his faithfulness to us, the he resigned, remember "Caesar's wife must be above suspicion."

    ReplyDelete
  23. Wanaomfagilia Lowasa kuwa katenda mengi mazuri ni sawa lakini pia kuna makubwa sana aliyatenda vibaya hivyo kufuta sifa zote. Sasa muda wake umekwisha na imani kwa wananchi juu yake haipo. Msimpotoshe JK kuwa amuweke Lowasa mahali popote zaidi ya wananchi wake huko Umasaini wakimtaka hata atembee juu ya red or black carpet kwa kuwa anawahonga mapesa ya kifisadi ambayo hana uchungu nayo na pia kwa vile anazo fedha nyingi sana HAZITAISHA HIVI KARIBUNI! Mwache awagawie wananchi wake kwa style atakayochagua yeye lakini tusimpe nafasi nyingine. Ataangamiza taifa hili kwa vile huwa hana AIBU. Hata mseme vipi! Kiburi sana yuko na THUBUTU NYINGI SANA anayo hata kujisikia yuko juu ya Rais. MZEE ACHANA NA LOWASA. ATAKUTIA DOWA WEWE NA CHAMA CHAKO.Ushauri huu ni wa bure kwa vile tunakupenda wewe kama wewe.

    ReplyDelete
  24. Labda Lowasa apewe nafasi kwenye Chama lakini sio Serikalini. His time has expired! He has lost his chance. That's it. LOWASA NI FISADI HIVYO HAFAI. HATA BABA WA TAIFA ALILIONA HILO NA AKAONYA.Sasa Mzee JK tafadhali usiendelee kumkumbatia huyo. ISHI MANENO YA BABA WA TAIFA!LOWASA HAFAI KURUDI SERIKALINI NA HATA YEYE ANAJUA ILA ANAJARIBU KUONAKINA CHA MAJI KUTOKANA NA USWAHIBA MLIOKUWA NAO, LAKINI USIRUHUSU.

    ReplyDelete
  25. Fisadi Lowassa........UKITAJA MAFISADI TANZANIA basi LOWASSA ni nambari one, wa pili ni MRAMABA, wa tatu ni KARAMAGI wa nne ni YONA wa tano ni ROSTAM wa sita ni MKAPA wa saba ni SOFIA SIMBA wa nane ni MAHANGA wa tisa ni CHENGE wa kumi ni MAKAMBA......oroodha ni ndefu na hao ndio the best tena, ila mmoja katangulia huko wote kwenda nae ni BALALI.....sidhani kama Bwana Mungu kamuweke pema peponi bali pema jehanamu......bila kumsahau fisadi anae kula sasa dona la ukonga nae ni LIYUMBA....mshahara wa dhambi ni mauti....hatujuti hata kidogo LIYUMBA kuwa lupango maana pesa za sie walipa kodi yeye ndio za kutanua na malaya zake...............

    ReplyDelete
  26. Ni kweli CCM ni Chama Cha Mafisadi. Je kwanini wananchi tunaendelea kuwapa kura nyingi? Richmond iliiweka nchi gizani kwa muda mreefu sana. Lakini bado CCM inathubutu kuwasafisha waliohusika. Wale wa kashfa ya RADA tumefahamishwa waaazi na Waingereza juu ya Ufisadi wao, lakini TAKUKURU (CCM) imeharakisha kusheherekea uamuzi wa DPP wa Uingereza kuwa hawatafunguliwa mashtaka huko Uingereza. Na sisi je? Kwanini tusiwafungulie mashtaka KISUTU? CCM ni Mafisadi tupu.

    ReplyDelete
  27. Oh! Tanzania si masikini wa Viongozi wala sijawahi kuona saa zikirudi nyuma. maana yangu ni kwamba Mheshimiwa Lowassa alitakiwa kabla ya kashfa iliyotokea awe ameshaijua na kuibaini kwani ndiye aliyekuwa mtendaji mkuu wa serikani hivyo basi kukaa kwake kimya ulionyesha madhaifu kama si mapungufu kwake, ndugu zangu, kitengo cha usalama wa taifa kilikuwepo mambo mengi hayakuwa uficho zaidi wapinzani waliwezaje kuibua hiyo kashfa huku kakalia mtungi mkuu wenye kila siri ya taifa? kama ningekuwa rais hawezi kuweko kamwe tena kwenye uongozi, hivi Hayati Julius Nyerere alikosea kauli zake kwa ndugu yetu huyu? nashauri akaa chini awashauri tu wengine kuhusu uongozi na umakini wa uongozi badala ya kutafuta tena kuingia kwenye mdundo wa uongozi wa taifa hili ambalo raia wake wameanza kuamka usingizini.

    ReplyDelete
  28. Jk akitaka kumpa yeye ampe tu chochote, lakini watanzania hawataendelea kuwa wajinga kwa miaka mingi sana ijayo. Tunajua wengi ndani ccm wameoza, so whoever atachaguliwa will just end up the same. Tunajua nchi inaendeshwa kifalme/kikoo/kifamilia, kama sio Lowassa kupewa atapewa someone else ndani ya mtandao.Solution tunayo kila baada ya miaka mitano, but hatuitumiii, so acha wafanye tu wafanyalo, ngoja tupigike haswaa, mafuta (Dizeli, Petroli) zipande mpaka lita sh 6000 ndo labda tutajua jinsi ya kutumia demokrasia yetu ya kuchagua wachapa kazi, na sio serikali zenye dalili ya kiimla.
    JJJ kwenye mgomo.

    ReplyDelete
  29. Ama kweli wakupata niwakupata tu,kama kweli JK utamrudisha Lowassa kwenye baraza la mawaziri basi hukumu mtaipata 2015 kwani watz wa sasa si wale wa enzi za mwalimu kaani mkilitambua hilo.JK nikuibie siri ndogo ni kwamba usithubutu kuweka waliojichafua wenyewe bali weka waadilifu na wenye hekima,wachapakazi na ikiwezekana muombe mh.Mkapa akusaidie in one way or another kuwapata waliowasafi ili kuzikonga mioyo ya watz waliokata tamaa na nchi hii.Anyway let us wait and see what is happening in this land of Julius K.

    ReplyDelete
  30. Je hela za watu wa MV bokoba atawalipa lini? Mbona zilitolewa zikakabidhiwa kwake akiwa ofisi ya waziri mkuu na hadi leo bukoba na mwanza ni viliyo vya wajane na yatima awajalipwa. Je kwenye hayo mashirika na halimashauri tutapona?

    ReplyDelete
  31. mi kura yangu ningempa lowasa kwani anajua kazi ,ni mwenyekuwa na maamuzi,inachokisimamia kinafanyika!hakuna aliyemkweli,sema wengi wao mambo yao mkiyajua mnaweza kumwona lowasa ni afadhari!pliz lowasa apewe nafasi!

    ReplyDelete
  32. Kuna wabunge wengi sana wasomi ndani ya chama chao cha mapinduzi sioni ni kwanini lazima baadhi tu ya wabunge ndio wateuliwe kuwa mawaziri na ukizingatia walijiuzulu kwa kashfa mbalimbali, nashauri wachaguliwe watu SAFI na WACHAPA KAZI na sio mtindo wa urafiki na kujuana hii nchi haiendelei kwa mtindo huo tutabaki kuwa masikini kwa kuwaendekeza mafisadi ambao wanatumaliza,wachaguliwe watu wenye uchungu na nchi yao na wanaopenda maendeleo kwa nchi na si kwa manufaa yao binafsi.

    ReplyDelete