23 November 2010

Uamuzi wa Zitto wazua mjadala.

Na Mwandishi Wetu.

UAMUZI wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe wa kupingana na uamuzi wa chama chake ambacho kiliamua kwa kura wabunge wake watoke nje ya bunge wakati Rais Jakaya Kikwete akihutubia
umewagawa wananchi, huku baadhi wakimuunga mkono wengine wakimponda kwa usaliti.

Bw. Zitto alipingana na uamuzi huo na kuamua kutokwenda kabisa bungeni ambapo wabunge wengine wa chama hicho wakiongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe waliingia bungeni na kuondoka wakati Rais Kikwete alipoanza kutoa hotuba yake.

Kwa mujibu wa maoni yaliyotolewa na wasomaji wa gazeti la Majira ambalo juzi liliandika ufafanuzi wa Bw. Zitto kuhusu uamuzi wake wa kutokwenda kabisa bungeni wakati Rais akihutubia, walimpongeza kwa kitendo hicho na kusema kuwa alionesha ukomavu wa kisiasa na kutokukubali kuburuzwa na viongozi wa CHADEMA.

 “Zitto ni kiongozi mkomavu na shupavu na ana busara ndio maana akachukua uamuzi wa kutokwenda kabisa, tunajua wanaweza kumzushia kuwa yeye ni mamluki na mambo mengine lakini kadri siku zinavyokwenda tutajua hata waliokwenda kwa kushinikizwa,” ilisema sehemu ya maoni ya msomaji.

Msomaji mwingine aliyeonesha kutofautina na wengine alisema kuwa kuwepo kwa Bw. Zitto na kutokuwepo ina maana kuwa wote walikubaliana kushinikiza kudai haki za watu walioibiwa kura na NEC ili kumpa ushidi Rais Kikwete, hivyo kitendo cha Bw. Zitto kinamwonesha namna alivyo mamluki wa Chama Cha Mapinduzi.

Msomaji mwingine aliwataka wabunge wa CHADEMA kudai haki kwa njia za busara na sio kutoka nje ya ukumbi wa bunge wakati Rais akihutubia kwa kuwa iko wazi kuwa rais akishatangazwa hakuna namna ya kumpinga.

“Uamuzi wa Zitto ni mzuri lakini kibaya alichokosea ni kutoa siri za kikao cha chama ambacho walikubaliana kufanya kitendo hicho, hivyo hakutakiwa kuweka wazi siri hizo,” ilisema sehemu ya maoni hayo.

Akizungumzia suala hilo, msomaji aliyejitambulisha kama mfanyabiashara na mkazi wa Jimbo la Bw. Zitto, Bw. Jackson Kumenya alisema kuwa kitendo alichokifanya cha kupingana na chama chake ni kurejesha shukrani kwa Rais Kikwete ambaye hakwenda jimboni kwake kwa kumnadi mgombea ubunge kupitia CCM.

“Yeye aseme tu kwamba alifanya hivyo kwa ajili ya kumshukuru Rais, kwani angekuja jimboni na kumnadi mgombea wa CCM yawezekana kabisa angeshinda lakini kwa kutokuja ilimrahisishia kazi Bw. Zitto,” alisema Bw. Kumenya kwa njia ya simu.

Msomaji mwingine aliandika, "Hapa zitto kama chadema kinakushinda nenda CCM, hapo hatujengi, tunabomoa. Mpaka hapa tunajua Zitto wewe ni 'papeti' (kibaraka0 wa CCM.

zitto, uamuz wa chama ni wa wanachama wote, iweje wewe upingane nao. jitahid kuzuia hisia zako binafsi, ndio maana uamuzi huu ulifikiwa kwa kura.

Naye Bw. Amani Silayo alisema, "Nina imani CHADEMA mlimchagua huyu jamaa (Zitto) mkiwa mnamwamini, ila  kiukwel mwangalieni sana. Hapo jinsi ya kumkanya, hebu tumieni busara maana Watanzania tunawaamini sasa, mkianza kugawanyika kama vyama vingine watu wataona chama hakina mwelekeo."

37 comments:

  1. Nampongeza Zito kwa kutumia uhuru wa kutoa mawazo ndani na nje ya Chama. Hao vijana wa Kichaga wasiachwe wavuruge CHADEMA. Alichofanya Zito ni kumuenzi Hayati Chacha Wangwe. Koleza zaidi Kabwe.

    ReplyDelete
  2. Amekosea sana huyu Bwana Mdogo Zitto,kutoa siri za maamuzi yaliyofikiwa ndani ya Chama chake ni sawa na kutoa siri za chumbani anakakolala na mkewe.Hata kama hakukubaliana na wenzake na ambavyo hakufika hakutakiwa kutoa siri za maamuzi waliyofikia ndani ya Chama.
    Huyu ndani ya CHADEMA sasa ni mamluki wa CCM(Chaka Chua Mapema) tangu kipindi kile alivyoingizwa kwenye Kamati ya Madini kwani baada ya pale alianza kubadilika sana na ndiyo maana Kikwete hakumpigia kampeni mgombea wa CCM kwenye jimbo lake ili kumpa nafasi ashinde.
    Kuanzia sasa nawashauri WanaCHADEMA(Na mimi nikiwepo)kuwa makini na huyu mtu kwani ana walakini ndani ya nafsi yake.

    ReplyDelete
  3. Zitto sio mwana mapinduzi,nilikuwa nasikia izi kauli nabisha sasa nime amini,sijui kapewa ahadi gani na CCM,huyu ana future kwenye mageuzi,tunamsubiri 2015 na ndoto zake za kugombea uraisi,hapati Ng'o

    ReplyDelete
  4. kweli zitto hapo umechemsha, ina maana wewe unakubaliana na katiba ya sasa, tume ya uchaguzi ya sasa na muundo wake na mfumo ulitumika kumchagua rais tofauti na chama chako! huna haya? kisa pesa za kamati ya madini. tunakosa kuna imani nawe. au wewe ni mamluki? nenda ccm. usituharibie cc wapenzi wa chadema. wewe kutokewnda bungeni cku hiyo ilikuwa makosa mkubwa, mbaya zaidi ukaja tena kuweka adharani sababu zako binafsi za kutokewnda kinyume na msimamo wa chama chako hapo tena ukakosea zaidi na kuongeza hasira za wapenzi wa chama husika. Nashauri chama kimuadabishe. nadhani huyu zitto anatafuta makosa makusudi ili apate kisingizio cha kuhamia ccm. hafai tena kuwa chadema.

    ReplyDelete
  5. Ni hatari sana kuwa na mtu kama ZITTO KABWE. Huyu bwana ni kweli anapenda sifa na sijui kama huwa ana uwezo wa kufikiri sana kabla hajatenda. ZITTO kwa siasa za Tanzania anajiona anafaa ila kwa siasa za wenzetu kule ULAYA au Marekani wangeshamtimua siku nyingi. ZITTO ni mshamba kisiasa na CHADEMA wamuonye na akirudia tena ATIMULIWE, CHADEMA itabaki yeye ataondoka. Kama RAIS amepeleka maendeleo jimboni kwake, hiyo si kupendelewa ni wajibu wake RAIS kufanya hivyo maana yeye si RAIS wa mkoa au wilaya fulani ni wa WATANZANIA WOTE. Nawashauri CHADEMA wamtimue haraka, maana yeye si Mungu wala malaika wa CHADEMA.

    ReplyDelete
  6. WANACHAMA WOTE WA CHADEMA MNAOMPONDA NA KUMKEJELI MHESHIMIWA ZITTO KABWE NI WANAAFIKI NA MNAFANYA HIVYO KWA SABABU ZITTO AMEWEKA NIA YA KUGOMBEA URAIS MWAKA 2015. CHADEMA HAWAKO TAYARI KUMPA NAFASI MGOMBEA ASIYE MKIRISTO KUGOMBEA NAFASI YA JUU KWENYE UONGOZI WA NCHI KUPITIA CHAMA CHA WAKRISTO TANZANIA. NA HUU NI MWANZO, ZITTO ATAANDAMWA NA KUTUKANWA MATUSI YOTE ILIMRADI AONEKANE HAFAI NA HASTAHILI HESHIMA YOYOTE NDANI NA NJE YA CHAGGA DEVELOPMENT MANIFESTO(CHADEMA)
    WATANZANIA TUSIPOJIHADHARI NA CHADEMA, HATUNA NCHI!!! NI CHAMA HATARI CHENYE MALENGO YA HATARI SANA YA KULIGAWA TAIFA KWA MISINGI YA DINI NA UKABILA, WACHAGA NA WAKRISTO NDIO WENYE CHAMA , WENGINE WOTE NI SHUWAINI, MAMLUKI, N.K. TUAMKE WATANZANIA!!!!

    ReplyDelete
  7. pETRO eUSEBIUS mSELEWANovember 23, 2010 at 10:09 AM

    Nilishasema kwamba kitendo alichokifanya Zitto ni ukosefu wa adabu kwa viongozi wake wakuu wa chama Bungeni na nje ya Bunge.Pia ni alama ya kutokuwa na siri,'kujaa misifa',kimbelembele,majivuno na nini sijui.Sasa Bwana Zitto tunakutaka usirudie tena...siri zinabaki kuwa siri.Au ndo umechukua maneno ya Mrisho Mpoto yaliyo kwenye wimbo wake wa Asanteni'siri tunasema na bayana tunaficha'? Kama huwezi toka CHADEMA..usitupotezee 'apetaiti' yetu ya kuchukua kadi za uanachama wa CHADEMA bure!

    ReplyDelete
  8. Zitto uko strong sn umekataa kuburuzwa na Mbowe, umekataa kugoma na kulalamikia pembeni km wengine walivyofanya. kwa kuwa hujabebwa na mtu ndio maana unajiamini. Unauelewa, mkubwa umesoma,usiburuzwe na CHAGA DEVT MANIFESTO.

    ReplyDelete
  9. CHADEMA MNASUBIRI NINI KUMFUKUZIA MBALIHUYU MSALITI ALIYETUMWA KUWAVURUGIA CHAMA CHENU MAKINI? ZITTO SIO MWANACHAMA WA CHADEMA ILA NI MAMLUKI KUOKA .... HAFAI KUPEWA MUDA ZAIDI WA KUISAMBARATISHA CHADEMA KUMBUKA KINGA NI BORA KULIKO TIBA. WAHI ADUI YAKO KABLA HAJAKUWAHI. ZITTO AFUKUZWE CHADEMA MARA MOJA

    ReplyDelete
  10. naishangaa chadema chama makini lakini kinaonekana kama haki idara ya inteligence kwani taarifa za zitto kufanya vikao vya siri na chama wapinzani wenu hamzifahamu? acheni kulala jamaa ametumwa kufanya kazi ya kuwamaliza.msipo mchukulia hatu safari hii msishangae kadi zenu zikianza kurudishwa wanachama wamechoka.mnapewa siku saba kutoa tamko kuhusu hatua mlizochukua dhidi ya zitto.

    ReplyDelete
  11. Wakufukuzwa ni bowe na Slaa ndio walioandaa mpango wote musilaumu zitto anajua anachofanya si mtu wa kuburuzwa

    ReplyDelete
  12. Kwa hili, Zitto amepotoka. Kutoa siri za CHADEMA tena akiwa mmoja wa viongozi wa juu ndani ya chama chake ni uhaini. Hivi CHADEMA mnayafumbia macho mpaka lini? Zitto aliwahi kumsubiri JK Nairobi wakaja wote na ndege moja hadi Dar. Baada ya hapo tulimsikia JK akimchagua Zitto kuingia katika tume fulani kuhusu madini. JK alipokwenda Kigoma, pamoja na kuwa Zitto ni mbunge wa sehemu aliyozuru JK, sifa alizopewa JK na Zitto zilitosha kabisa kuonyesha aina ya urafiki ambao Zitto alikuwa amejenga kwa JK. Tumwombe Zitto afanye uamuzi bayana wa kujiunga na CCM kuliko kufanya siri hilo, na badala yake kuanika siri za CHADEMA nje.

    ReplyDelete
  13. Mi naona kama zito anatumiwa kuidhoofisha chadema, kama anauchukia uongozi wa juu si akihame chama mara nyingi misimamo yake inatia shaka!! ndio maana hata umaarufu wake umeporomoka haeleweki anamtumikia bwana yupi umuch now mwingi!!

    ReplyDelete
  14. kwa maoni yangu Zitto hana tena mvuto ule uliomfanya akafika hapo, hana ushawishi tena kwa watanzania, binafsi alikuwa mtu aliyenigusa sana kipindi kile hata alipofukuzwa bungeni nilienda kuandamana, leo hii hata akifanywa kitu gani sitajisumbua, wala simsikilizi tena, keshachakachuliwa huyu, aondoke tu chadema asituletee makundi yasiyo na maana, kama kura zilionesha wengi walisema wasuse sasa anataka nini, kwani Jk alipata ushindi wa asilimia 100?? mbona sasa anamweshimu kama Rais, hata yeye jimboni kwake hakushinda kwa 100% ndo maana sasa wote hata waliompinga anawatumikia, asituchezee aende tu ccm. Tushamchoka.

    ReplyDelete
  15. KABWE KAMUA BABA, NA HAPO HAKUA ZITO PEKE YAKE HATA KINA MPENDAZOE NAO HAWAKUHUDHURIA NA PIA WALITOA SABABU KWANINI HAWAKWENDA BUNGENI. MWENYE AKILI HAWEZI KUBURUZWA NA CHUKI BINAFSI, MBONA MPENDAZOE ALIPIGWA MPAKA PICHA AKIONGEA NA JK NA MAGAZETI HAYAKUSEMA NI MHAINI? WAPENZI WENZANGU WA CHADEMA WAKATI MWINGINE TUWE WAKWELI SI KILA ANACHO KISEMA SLAA NA MBOWE NI KITAKATIFU TUTAUMIA.

    ReplyDelete
  16. kwa mtazamo wa wahafla tu mtasema amekosea,siasa hakujifunza leo au jana anajua anachofanya tuvute subra tutaona nini kitatokea baadae

    ReplyDelete
  17. Mh.zito yupo wrong.Kunauwezekano akawa kibaraka coz alipokuwa chaguliwa kuwa miongoni mwa wanakamati ya hao wanaofuatilia maswala ya mikataba ya madini bungeni ndo imempunguzia ujasiri wa kutetea mambo ya msingi kwenye chama chake kwa maslahi ya taifa.
    kinachotafutwa sana na chadema ni haki itendeke na wala hawana uroho wa madaraka coz wanasema hata mtu angeshida kwa asilimia 20 basi iwe kwa haki na hamna mtu angelalamika.
    na kama serikali ipo makini wanapata kigugumizi gani kwa swala la katiba kama sio uroho wa madaraka wasiotaka wengine waongoze kwa lengo la kuleta maendeleo. wenzangu tujaribu kuchambua baadhi ya mambo kwa makini sana.
    mary

    ReplyDelete
  18. Sawa ni demokrasia kutohudhuria kwa zito, lakini kwa nini atoe siri za ndani, kwa nini kila mara anajitofautisha? Kama chadema cha wachaga CUF ya nani ya dini gani? Ni unafiki kusema chadema ya wachaga. Wengi wa watanzania ni waoga sababu ya umaskini. Wachaga wengi wemejikomboa kielimu hata kifedha. Hawasikilizi porojo za chaka cha Mapema

    ReplyDelete
  19. mbona wapenzi wa CHADEMA tusiwe na subira? kwa nini tunakuwa na haraka wa kulaumu? siasa inahitaji uvumilivu hata Zitto naye amekuwa na haraka wa kuropoka,Watanzania wanapunguza imani kwake heri angenyamazwa kwanza kama wabunge wengine kwani wote waliridhia kitendo hicho?. suala la kitaifa halihitaji kuropoka bali umakini yeye kama hakuwepo Bungeni angesema hakuwepo siku hiyo,.Spika wa bunge au majaji na wanasheria hawajatueleza kama wabunge wa CHADEMA walikiuka sheria ya nchi, sasa uropokaji kwamba fulani kaburuzwa kumetoka wapi kama sio kujimaliza kisiasa.kwa mwendo huu kila siku tutakuwa tunahama vyama kwabila sababu za muhimu kwa maslahi yetu binafsi.Eti mtu akivunja maadili ya chama akikemewa anakihama chama na kukimbilia chama kingine,kuhama kwetu vyama viwe kwa msingi wa kuwatetea wanyonge lakini sio kwa uropokaji hata kanisani kuna kanuni za kufuatwa kila mtu hawezi kuwa msemaji kwenye chama.
    ninawaomba msimlaumu Zitto, tusubiri kwanza mambo yawe dhairi ndipo tutamjua shujaa katika suala la wabunge wa CHADEMA kutoka nje ya ukumbi.tumvumilie hata kama kile ambacho amekisema si kweli tumpime kwanza kwa sababu inawezekana ni uharaka wa kutafuta makuu.hata Kikwete Baba wa taifa alimkataa japo wengi walimwona kuwa anafaa, leo ndio wamethibitisha baada ya kumpa madaraka.wanaomlaumu Mbowe wakae na kutafakari kwa kuona ni wapi Mbowe amekitoa CHADEMA kwani chadema kinazidi kusonga mbele tofauti na vyama vingine vya upinzani huko Bara, halafu suala la udini wekeni mbali jambo hilo halipo kwa watanzania bali kwa Wakubwa hao wanaotafuta madaraka ndio wanaowachonganisha wananchi kwa udini.

    ReplyDelete
  20. Zito nimekukubali kwa busara zako.

    ReplyDelete
  21. Zitto ni mwanasiasa anajua nini kitatokea baadae,Kitendo walichofanya chadema wameitia aibu Tanzania kitaifa na kimataifa kuwa T'zania hakuna democrasia ya kweli na hilo ndio lengo lao tu hakuna lengine na kama wanayo hoja ya kudai katiba mpya na mengi mengineyo si wanao wabunge 47 si wanatosha kupeleka hoja zao bungeni,Kumsusia Raisi sio suluhisho bali ni kundeleza migogoro isiyo na maana yoyote katika nchi yetu.Hayo ndio yamesha tokea sasa ninaamini CCM watajibu mapigo ambayo yatakiasiri chama cha chadema ,Tunasubiri nini kitatokea bado ni mapema mno kujua.Lakini tufahamu kuwa siasa si ugomvi,simatusi,si fitna bali fikra ambazo zinaweza kutuletea mabadikiliko ya kweli katika nchi yetu

    ReplyDelete
  22. Mimi ni yule yule Hafidh kutoka visiwa vya amani- Zanzibar.

    Mimi maoni yangu ni kua inapaswa watu wawe na uelewa kwanza badala ya Jazba ya kutoa maoni ambayo hayana hoja za msingi.

    Kutofautiana katika Chama cha Siasa au Serikali haina maana ya mtu Kuonekana katenda Dhambi kubwa!! Lazima tuelewe kua ni haki ya msingi na kikatiba pia mtu kutoa maoni yake ili mradi asivunje haki ya mwenziwe tu. Ni mara ngapi Viongozi wanatofautiana mawazo katika nchi hii jamani mbona haijawa issue?! kwa mfano mh. Mizengo pinda alitafautiana kimawazo na wana CCM Wenzake pia kwa suala la Zanzibar kua nchi au si nchi? ushahidi wa hili CCM (Viongozi)Zanzibar walikua wanapinga wazi wazi kua Mh. mtoto wa mkulima alipitikiwa ilhali mwenyewe anajiamni na kusema yupo sawa.Mbona hapa haijaonekana issue.
    2) Katika Chama cha CUF - Mh.mmoja(Jina kapuni) alitofautina wakati ule Wawakilishi wa CUF kugoma katika Baraza na Mbona haikuwa issue kubwa na mpaka leo Mheshimiwa huyo anaendelea kupiga siasa kama kawaida na anaendelea kua mwakilishi.

    Mimi naona Zitto kutofautiana na wakuu wake ni kukomaa kidemokrasia pia ,kua na uhuru wa kuongea tusiwe kama wenzetu kwa wakati ule wa mfumo wa chama kimoja.Huwezi kusema lolote una hofu au labda uachie ngazi.

    Wanachadema nawaomba mutulie musiwe na jazba bado Zitto ni kiongozi na mwananachama hai wa chadema. msihukumu ikiwa hamjawa na ushahidi na mkipata ushahidi ndio mtoe hukumu.

    Igeni CUF na msimamo wa kuondoa viongozi wake amabao wanapatikana na ushahidi kua wasaliti.mara nyingi hua wanajiondoa wenyewe katika chama badala ya kuona wamebanwa sana.

    TANZANIA ILIOJAA NEEMA YA MALIASILI BADO INAKUA OMBA OMBA! TANZANIA YENYE NEEMA INAWEZEKANA- TUNAHITAJI MABABADILIKO- WE NEED CHANGE -YES WE CAN.

    ReplyDelete
  23. Zitto kitendo ulicho kifanya siokabisa, unaonyesha jinsi gani haupendi kushirikiana na wenzako,huu ni mwanzo tu, hata kama ulipingana nao ukachukua uamuzi wa kutoenda bungeni usingejipendekeza kutoa siri za chama kwa waandishi wa habiri basi ungewafichulia hata siri za chumbani kwako.

    Hata kama Jk amekufanyia mambo makubwa jimboni kwako, lakini heshimu katiba ya chama chako nakuilinda au unatakakwenda ccm.
    Tunakuomba ujerekebishe kijana mwakajana ulikuja kwa kasi nzuri sana mpaka ukashirikiana na wenzako kufichua mafisadi. Waite viongozi wenzako waombe msamaha kama vipi waambie niilingiliwa na ibilisi.

    ReplyDelete
  24. Mh. Zito dalili za mvua ni mawingu. Usipokuwa makini sifa yako itaporomoka. Hata kama una uwezo wa kupanga maneno kushawishi watu. UKIHAMA CHADEMA...utahama peke yako..Tunashukuru kwa kukitumikia Chadema. Tunaomba uwe muwazi,uweleweke, Kwani tendo la kuamia CCM basi ujuwe umekwisha...! hata udiwani hautapata! Una ndoto za urais..! atakupa nani kura!!! Tunakupenda ni kijana mwenzetu na muda fulani huwa una hoja za msingi lakini kwa ndoto ya urais hapo unachemsha..!Pole kwa kutamka haya,ni we mwenyewe umewahi kutamka. Dalili zako za kupenda madaraka ya juu zipo wazi...Acha kusingizia DEMOKRASIA..! Demokrasi isipolindwa madhara yake ni makubwa. Tulia kijana! jenga nchi, watumikie wanyonge.Waombe radhi watanzania (wanachedema)kuwa umekosa na ukili kuwa we si ndumila kuwili. WATANZANIA TUMECHOKA...! OH..! Chama PINZANI kilichobaki Tanzania
    ni CHADEMA tu!! Wananchi tunaanza kukiamini. Wanaoimba ndani ya chadema kuna ukabila, hawana akili nzuri.Chadema ni chama kichanga, msingi wa chimbuko la walioanzisha chama ndio panazaa tatizo.Wana mtwara ndie wangekuwa waasisi, mngekiita chama cha wamakonde...! Yamkiniki jibu ingekuwa................!

    ReplyDelete
  25. Mbona siyo siri Zitto Kabwe amekuwa anaonyesha dalili za umamluki muda mrefu tu.
    Kwanza wakati wa kampeni alitamka anataka kugombea urais 2015. Badala ya kutilia mkazo uchaguzi uliopo yeye anatangaza nia ya 2015 kinyume na utaratibu. Pili ukaribu wa JK kwa Zitto una agenda ya siri. Tatu Zitto anafikiria yuko juu zaidi ya alivyo. Kama anataka kurudi CCM aende tu. Wanachadema tuko wengi na Chadema ni chama Imara na Makini.

    Wale mamluki wote wataanza kujitokeza kipindi hiki cha kudai haki za msingi kwa watanzania. Kipindi cha kujitolea muhanga kama wabunge wa chadema badala ya kutoa hotuba za uongo na kweli kule bungeni.

    ReplyDelete
  26. Mimi si Mchaga lakini nawasifia ndugu zetu hawa kwa misimamo wanayoweza kushikilia na kutetea mambo muhimu. Watu wa Kaskazini wanajitahidi sana kuwa na msimamo. Angalia watu wa Arusha, Kigoma, Mwanza, Shinyanga, Musoma, bila kuwasahau watu wa Mbeya, watu hawa wana misimamo. Ni mtazamo tu wala siyo ukabila. Zanzibar pia wamo

    ReplyDelete
  27. Mh ZITTO angalia wenzako akina Lamwai, Makongoro hawapo tena katika ramani Tanzania. Na usaliti ndio huohuo. Kama unakerwa kwa nini usijisogeze chama kingine hapo pembeni kinachoweza kukusikiliza, kwa nini ukae na watu wanao kukwaza. Na kauli ndio hiyo hiyo ya wachaga ina maana hawa wachaga wananuka au wananini tujiulize. Basi kama hili kabala la wachaga linawakwaza wengi na hawataki umoja nao basi wajitenge wafanye shughuli zao za kimaendeleo kwa sababu wanawakwaza. CCM mnambinu chafu sana na mlimwaga sumu kali sana kuhusu hawa wajamaa lakini yana mwisho. Ni kijiji gani utakwenda usimkute mchaga kama wangekuwa hawana umoja na wanaipenda TZ yao, na wanapenda kuishi maisha ya kila hali. Yaani ukishakuwa mamluki wa madaraka ukiona haiwezekani mnatupa huko wachaga kinaniuma sana japo sio mchagaaaaaaaaaaaa.

    ReplyDelete
  28. Mimi binafsi nilianza kutokumwelewa huyu Zitto wakati wa sakata la mitambo ya umeme wa
    ya Dowans, alikuwa anashauri eti serikali inunue mitambo ile! hivi kweli hata kama ni kwa manufaa ya taifa mitambo ile ilikuwa ni ya kununuliwa kweli? pamoja na wingu zito lililokuwa limetanda kuhusu mitambo ile yeye bila hata aibu akawa anashauri mitambo ile inunuliwe! hapo ni wazi kabisa alishachakachuliwa tayari, na kwa sababu alishajiona yeye ni super star watu watakubali tu! kwa hiyo hata hili la kupingana na uamuzi wa chama chake kwa sasa hivi sioni ajabu tena, cha msingi ni kumshikisha adabu mapema asijione kwamba bila yeye hakuna Chadema na hii inatakiwa ifanyike haraka kabla hajaharibu chama, Bravo Peoples power!

    ReplyDelete
  29. zitto sikukubali. ulichofanya sio kabisa, naona ile kamati ya madini imekupotezea dira na kama una wazo la kuwa rais ktk hali unayojijengea sahau, Vijana wapenda mabadiliko hatuwezi kumpa mamluki rungu

    ReplyDelete
  30. Kwa mtu asiyekuwa wa kawaida hata akiwa na akili kama ya kuku anafahami fika kwamba Tanzania haiana katiba. nashangaa maoni ya wavivu wa kufikiri wanaona madai ya katiba sio sahihi. watanzania amkeni jamani mambo mengine hayahitaji digrii kuyang'amua angalia ilianza celtel mara ikabadilishwa ikawa zein muda mfupi imebadilishwa imekuwa Airtel, kuna nini tanzania? Tax holday?????????????????. bakini na ujinga wenu hivyo hivyo.ZITO MAMLUKI AFUKUZWE CHADEMA ISONGE MBELE.

    ReplyDelete
  31. zito hauna jipya ktk siasa za bongo na za kimataifa. tanzania tunahitaji mabadiliko ya katiba na tume ya uchaguzi

    ReplyDelete
  32. Kutofautiana ni jambo la kawaida hata ktk siasa. Powell hakukubaliana na siasa za Bush kuhusu Irq. Na akasema hadharani hatakichagua chama chake katika uchaguzi. Powell bado ni mwana Republican na hakuna aliyemwona msaliti. Zito yuko sahihi kueleza msimamo wake hata kama ni hadharani. Unaweza ukatofautiana na hoja yake lakini siyo kumhukumu kwamba ni makosa yeye kuwa na mtazamo tofauti.

    Maoni mengine yanayotolewa yanaonesha watu wanaoyatoa WAMEFILISIKA kuwaza. Zitto hajasema kuwa alikataa kuburuzwa na wala hajasema kuwa ambao waliunga mkono maamuzi ya kikao waliburuzwa. na wala hajasema kuwa msimamo wake ni kwakuwa yeye ni dini fulani au alikuwa anapinga msimamo wa watu wenye dini au wanaotoka mahala fulani. Sasa wewe unayehusisha uamuzi wa Kabwe na dini yake, au sehemu anayotoka au usaliti katika chama ujue kuwa UMEFILISIKA KUWAZA. Acha kuweka sumu katika jamii na ndani ya chama. wakwanza kuumia mambo yakiharibika unaweza kuwa wewe mwenyewe. Tuache kufanya MASIHARA na mambo tete yanayoweza kuliangamiza taifa.
    A.M.BAKARI

    ReplyDelete
  33. CHADEMA tumia busara, fanya maamuzi magumu kama mliyofanya ya kususia (walk out) hotuba ya JK kwa sababu zinazoeleweka vizuri sana kwa watu wenye welewa, ONDOA hii sumu mapema. Hii ni bahati Bw mdogo huyu ameshindwa kuficha hisia zake na hivyo kuwapa nafasi ya kuamua mapema. Zitto aondoke kama Kabolou alivyoondoka na CHADEMA itaendelea kuwepo. Mimi nimeshindwa kumwelewa alitaka nini. Msimwonee aibu ye yote yule anayejikomba kwa mafisadi. Vita mliyoanzisha na mnayoiongoza ni ngumu, inahitaji watu wasio wanafiki. Hata hao wabunge waliokataa kuingia ukumbini wapeni elimu juu ya mapambano dhidi ya ufisadi (adui namba wani wa watanzania), wakishindwa mtihani msiwaonee aibu, fukuza. Mhariri tafadhali nifikishie ujumbe huu kwa Uongozi wa CHADEMA. Tunakosa mahali pa kuwapitishia moja kwa moja maoni yetu.

    ReplyDelete
  34. Nawapongeza majira kwa blogu hii nzuri na isiyona upendeleo. Tumemchoka Michuzi blog kwani yeye anapendelea CCM na JK. Tukipeleka maoni yetu anayatupa kapuni anaweka yale ya JK na CCM tu.

    Mkiendelea hivi tutakuwa tumepata mkombozi wa kutoa maoni yetu kwa uhuru. Issa michuzi abaki na mambo ya burudani tu

    ReplyDelete
  35. Hivi kumbe ilikuwa siri hayo mambo? Eti vikao vya siri, hakuna siri ya zaidi ya mtu mmoja. Na siri ni ya mtu mmoja tu si chama wala kikundi. Kama mngekuwa mnajua kuna mambo ya siri msingekuwa mnabeba mafile ya serikali na kumpelekea Dr wenu ayatangaze hadharani.

    SIONI LOLOTE LA AJABU ALILOLITENDA ZITTO KWA KUSEMA WAZI KUWA HAKUUNGA MKONO HUO UAMUZI. NA HATA SHIBUDA ALISEMA HAYO NA PICHA AKAPIGWA AKIMPA MKONO JK MBONA HAMUMSHAMBULII KUWA NI MAMLUKI TENA HUYU AMEINGIA CHAMANI HIVI MAJUZI TU SEUZE ZITTO?

    Mwisho mtakufa vibaya kwa roho zenu mbaya, kilichowauma sio Zitto kutokugoma au kukubaliana na wenziwe bali ni ule ukweli aliousema kuwa JK AMEWANYIA WANANCHI WA KIGOMA MAMBO AMBAYO HAKUNA RAIS ALIYEPITA AMEYAFANYA. Kama wakweli mngemuuliza ni mambo gani hayo? Maana kutwa kwenye vijigazeti vyenu hamwishi kusema kuwa hakuna lolote alilolifanya JK ndani ya miaka mitano maana nyie ni wezi wa fadhila, hamuoni wala hamuthamini nguvu ya mtu.

    Bwana Mhariri hawa bwana ni hilo neno la Zitto kumsifia JK kuwa kafanya mengi Kigoma kuliko marais wote ndilo linalowauma na kuwatoa roho wananchama wa Chadema. Tena hili linaonyesha kuwa kumbe basi JK kashinda kihalali maana kama huko Kigoma watu wameona matunda yake watakuwa wamempigia kura JK ili aendelee kuyaendeleza yale aliyoanza kuwapa ambayo pengine tangu uhuru wa nchi hii walikuwa hawajayapata. Na kweli mwaka 2005 kabla ya uchaguzi nilikwenda Kigoma barabara za mitaani nyasi tupu, barabara za vijijini hazieleweki kama zinapita magari au matrekta, na umeme na maji vilikuwa ni msamiati wa kujifunzia maneno mapya watoto!

    Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, JK kachaguliwa na watanzania kwa yale aliyowafanyia, na kuna maeneo ambayo hakuna rais aliwahi kufika JK kafika kwanini watu wasimpe kura? Kwanza hao watu magazeti yenu na mitandao kwao ni lugha za kigeni kwa hiyo Chadema acheni utoto concede defeat na mjipange upya na mwaka 2015 hampati kitu na mnaweza hata kupoteza hivyo viti vyenu msipoangalia kwa ubabe wa usio na mantiki!

    ReplyDelete
  36. NAMMULIZA MSEMAKWELI HAPO JUU: KAMA CHADEMA NI CHAMA CHA WAKRISTO NA WACHAGA, CHAMA CHA WAISLAMU NA WAZARAMO NI KIPI - CCM AU CUF? WATU WAJIFUNZE KUTOA HOJA INAYOJITOSHELEZA NA SIYO KUKIMBILIA KAULI RAHISIS RAHISI. KUTUMIA UKABILA NA UDINI KUKISEMA CHAMA KIMOJA NA KUVIACHA VINGINE NI KUKOSA UWEZO WA KUCHAMBUA MAMBO KISOMI. KWA NINI WATU HAO WANAONA DINI TU AU UKABILA TU KATIKA KILA ISSUE ZA KITAIFA. KWA NINI HAWAONI USIASA, UBABE, UJINGA, UDIKITETA, UFISADI, UBWANYENYE, KUTOKUWA NA MAADILI, NA MAPUNGUFU MENGI AMBAYO TANZANIA INAYO?? KAMA MNATAKA KUZUNGUMZIA HOJA, BASI ANZENI NA ZILE ZA MSINGI KWANZA, YAANI MIZIZI NA SIO MATAWI MADOGOMADOGO. TANZANIA BADO INA ELEMENT YA UDIKITETA WA CHAMA KIMOJA, ELEMENT ILEILE ILIYOSUMBUA ULAYA MASHARIKI KWA MIAKA MINGI. KWA NINI HAMUONGEI HAYO??

    ReplyDelete