23 November 2010

Sitta: Namshukuru Mungu kwa yote.

*Waumini wa KKKT Kinondoni wabubujikwa machozi.

Na Mwandishi Wetu.

SPIKA mstaafu wa Bunge, Bw. Samuel Sitta amesema yote yaliyotokea juu yake anamwachia Mwenyezi Mungu na hakuna sababu ya kutafuta mlolongo mrefu.
Bw. Sitta alitoa kauli hiyo juzi kwenye ibada ya Jumapili katika kanisa KKKT Kinondoni, alipopata nafasi ya kuwasalimia waumini, naye akagusia kinamna masaibu yaliyompata Dodoma, jambo ambalo liliwafanya baadhi ya waumini wabubujikwe na machozi.

Mchungaji Mwaipile wa kanisa hilo, aliwatambulisha wageni waliokuwa kanisani hapo akiwamo Bw. Sitta, mkewe, Bi. Magareth Sitta pamoja na mbunge wa Lupa, Bw. Victor Mwambalasa.

Kabla ya mahubiri, Mchungaji Mwaipile aliwaomba waumini hao kutoa neno la skukrani, ndipo aliposimama Bw. Sitta na kusema alikuwa katika mapambano lakini sasa amerejea kujiunga nao.

"Msitafute mlolongo mrefu, sisi katika imani yetu huamini kwamba kila kitokeacho tunapaswa kumshukuru bwana. Hivyo naomba tumshukuru bwana," alisema Bw. Sitta

Bw. Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki, alieleza kufurahishwa na upendo uliooneshwa kwake na waumini hao ambao kila hatua ya mchakato wa uchaguzi wa uspika walikuwa wakimpa moyo.

"Mmenipa faraja sana, wengi wenu mlikuwa mkinifariji sana kwa kunitumia ujumbe mfupi na kunipigia simu. Nawaombeni tumshukuru bwana kwa kila kilichotokea," alisema Bw. Sitta ambaye alikuwa anatoa baada ya kukosekana kanisani kwa miezi mitatu ambayo amekuwa kwenye mapambano.

Aliwaomba waumini hao waendelee kumpa nguvu kwa kuwa  ataendelea kutumikia umma kwa uadlifu kwa uwakilishi wake wa ubunge wa Jimbo la Urambo Mashariki, kwani unampa nafasi tosha ya kufanya hivyo.

Bw. Sitta alitoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache baada ya kuenguliwa na Kamati Kuu ya CCM kuwania uspika kwa kile kilichoitwa kujali usawa wa kijinsia na kufanya muhimili huo kuongozwa na mwanamke kwa mara ya kwanza tangu uhuru.

Bw. Sitta anakumbukwa kwa rekodi yake ya kuendesha bunge la tisa kwa kasi na viwango na kulifanya liwe mwiba mkali kwa watuhumiwa wa ufisadi serikalini.

12 comments:

  1. Hayo aliyoyapata Samweli Sitta ni kazi ya mikono yake. Yeye alipewa dhamana ya Uspika akaitumia kwa maslahi yake. Pia Sitta ashauriwe asitumie makanisa kama majukwaa ya kisiasa.

    ReplyDelete
  2. HONGERA MZEE SITTA WAKATI UKUTA!! INABIDI UKUBALIANE NA NYAKATI UKIZIDI KUNG'ANG'ANIA ITASHUSHA HESHIMA YAKO, WEWE MZEE NI MMOJA KTK WAHIMILI WA CHAMA UNATEGEMEWA UMETOKA MBALI NA HESHIMA YAKO IKO JUU, STAHMILI HAYA NI MAWIMBI NI BORA UWAPE NGUVU VIJANA WALIO CHINI YAKO NA USITAKE KUHAMA CHAMA AU KUANZISHA MAKUNDI MAPYA NI KWA FAIDA YAKO NA CHAMA PIA, FIKIRIA ULIKOTOKA NA ULIPO NA UENDAKO KTK KULA PENSHENI YAKO

    ReplyDelete
  3. Kwani nani alimwambia kuwa atakuwa spika milele,anaweka maslahi mbele ndio maana kaomba aendelee kulipiwa pango la nyumba na umeme na serikali.Amepoteza fedha nyingi kujenga ofisi ya kifahari urambo heti yenye hadhi ya spika ,nani alimuambia kuwa atafia kwenye uspika.Tufikie wakati tuwe wa wazi,hizo fedha alizotumia kujengea ofisi ya spika kwao nani atazilipa,je spika mpya ataamishia ofisi yake urambo,another white elephant project by the hounourable sitta,conspicous consumption of resources.Takukuru mpo?

    ReplyDelete
  4. Hongera mzee Sita ,watanzania tuko na wewe daima,na bado tunaimani na wewe nimalizie kwa kusema"OLEMGOSHA WA KAPANGA"(WEWE NI MWANAUME WA SHOKA) ndiyo maana hata adui zako wa kisiasa wanakukimbia ,na pia wanakuogopa

    ReplyDelete
  5. Tuna kila sababu ya kukupongeza. Mafisadi wako tuone kama na wao wataupata huo uspika si wameukosa. Duniani usimfanyie mtu roho mbaya. Hao wanaosema Ofisi ya Urambo hiyo ni kwa faida ya wana Urambo na watanzania pia. Wasingelitoa jina lako Bw. Sitta mbona ungerudi katika miaka mitano tena lakini" TUMSHUKURU MUNGU KWA KILA JAMBO" hao mafisadi waliokuandama huyo mwingine anayo keshi ya RADA na Mungu atamlaani, ni kwa nini ameuwa watu wawili na bado anatamba na visenti vyake kwa nini asiwekwe lupango? Alaaniwe mtu huyu tena hana aibu ameropoka mengi lakini tunamshukuru Mungu kwa ajili ya Mzee Sitta. Si vizuri kumshukutumu mwenzako vijisenti alikuwa na tuhuma nyingi hivyo Mungu atamuadhibu hapa duniani asidhani ameua na yupo huru adhabu ya Rada itakuwa mikononi mwake hafai kupewa uongozi katika serikali hii ana majivuno sana hafai, muuaji kwa nini asifungwe apate habari zake hafai, tena hafai.

    ReplyDelete
  6. pETRO eUSEBIUS mSELEWANovember 23, 2010 at 10:59 AM

    Mi nauliza hivi:ile Ofisi ya Spika kule Urambo ya nani? Makinda atahamia kule au naye atajenga yake Njombe? Mh.Sitta tunakuomba ukaiuze ile ofisi ya Spika kule Urambo halafu tuje kujenga kitu kingine ambacho ni cha kudumu.Maneno yako ya simanzi kanisani hayasaidii kitu.Sisi tulikuambia usiizike Richmond....hukusikia.Ulikuwa na utaendelea kuwa kama 'CHICHIDODO'.Subiri wakuzuge na uwaziri ukajenge na Ofisi ya Waziri Urambo...Kila mja.........

    ReplyDelete
  7. Ndio salama yako baba! ule unga wa kichawi aliomwaga Chenge ukianza kufanya kazi ungekutoa roho kabisa! Likuepukalo lina kheri nawe, Shukuru Mungu kweli

    ReplyDelete
  8. WACHAWI, WAAGUZI NA WAONAJI NA WAPUNGA PEPO, nao walitupa fimbo zikageuka nyoka mbele ya Mussa, lakini fimbo ya Musaa ilipotupwa iligeuka nyoka wa shamba, na kuanza kuzimeza nyoka za wachawi, waaguzi, waonaji, na wapunga pepo, na mashuhuda na mfalme walipofika, waliona mikia ikiishia mdomoni mwa nyoka wa Mussa. Kusaja Kusaja.

    ReplyDelete
  9. Mh. Sitta wewe ulikuwa mfano wa kuigwa na hao waliopata sasa hivi kuliongoza bunge kwakuwa ulikuwa muwazi na mkweli na uliruhusu hoja binafsi ambazo zilikuwa ni nyeti na kali kwa taifa hili ambazo sidhani kama bunge hili la sasa zitapata nafasi maana ziliwaondoa mawaziri pamoja na waziri mkuu madarakani na kubaki kuwa wabunge, nionavyo mimi hii ilikuwa mbinu imesukwa ndani ya chama chako usipate tena nafasi kwakuwa uliruhusu serikali kukosolewa ambapo wao hawakupenda kukosolewa walitaka kuambiwa kila kitu NDIO MZEE kama vile wao ni malaika. Nakutakia uwakilishi mzuri katika Jimbo lako la Urambo na Mwenyezi Mungu akutangulie na usisite kusema ukweli pale wapinzani watakapokuwa wanagandamizwa bungeni kwakuwa ccm wana wabunge wengi.

    ReplyDelete
  10. Mzee sita hongera sana kwa kazi nzuri ulioifanyia Tanzania ili usisahau ule usemi usemao tenda mema nenda zako usingoje shukrani. Mungu atakulipa kwa wema wako wananchi tunakuombea na usikate tamaa ya kupinga rushwa. Ila mafisadi wakumbuke malipo ni hapahapa duniani na hao makatibu wakuu wa ccm wasisahau kuwa wanatakiwa kutumikia wananchi na sio ccm. Mungu ibariki TANZANIA, Mungu mbariki mzee sitta

    ReplyDelete
  11. Mi nadhani huyu bwana ni mdini. Ana kamchezo ka kukimbilia kanisani au kwa waumini wenzake wamwonee huruma.

    ReplyDelete