Na Mwali Ibrahim
BENDI ya muziki wa dansi ya African Stars 'Twanga Pepeta', imekamilisha nyimbo tatu zitakazokuwepo katika albamu ya 11, inayotarajiwa kuzinduliwa hivi
karibuni, Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja wa bendi hiyo, Abuu Semhando 'Baba Diana' alisema muda si mrefu wanatarajia kukamilisha nyimbo zilizobaki kwa ajili ya kuzindua albamu hiyo.
"Lazima tuzindue albamu hii hivi karibuni, kwani ni nyimbo chache tu zilizobaki na kutunga nyimbo si kitu cha kuchukua miezi, bali hata siku moja unaweza kukamilisha hivyo tunamalizia nyimbo zetu na baadhi zipo katika hatua ya mwisho kukamilika," alisema Semhando.
Alizitaja nyimbo zilizokamilika kuwa ni Kauli, Mapenzi hayana kiapo na Mida ya majeruhi ambazo zimeishaanza kuimbwa katika kumbi mbalimbali wanazotoa burudani.
Alisema licha ya nyimbo hizo, pia mitindo mipya ya uchezaji imeshatungwa na imeshaanza kutambulishwa kwa mashabiki katika kumbi mbalimbali za burudani.
No comments:
Post a Comment