NEW YORK, Marekani
MWANAMUZIKI nguli nchini hapa, Jay-Z amekana tetesi za kwamba mkewe Beyonce ni mjamzito.Hatua hiyo imekuja baada ya tetesi kusambaa tangu mwezi uliopita, zikidai
kuwa mwanamuziki huyo anajiandaa kupata mtoto wake wa kwanza hivi karibuni.
Hata hivyo baadhi ya watu wanadai kuwa Jay-Z, alimwambia DJ Howard Stern kwamba hakuna ukweli wowote katika taarifa zinazoeleza kwamba wanandoa hao, wanatarajia kupata mtoto katika siku za hivi karibuni.
Akikanusha habari hizo, Jay-Z alisema: "Nilirudi nyuma na kupigwa na butwaa wakati watu waliposimama na kuanza kusema kuwa Beyonce ni mjamzito, sidhani vyombo vya habari kama vinaweza kufahamu jambo hilo, kabla ya bibi yangu.
Rapa huyo aliongeza kuwa kila mmoja anafahamu ameoa, hivyo hataki kulijadili suala hilo kwa sababu ni sehemu yake ya maisha na anataka kuliacha kuwa suala binafsi.
No comments:
Post a Comment