01 December 2010

Tibaijuka awavaa mafisadi wa ardhi

*Ataka wajisalimishe haraka kabla hajachukua hatua
*Asema hababaiki na fedha zao, maana za mboga anazo


Na Gladness Mboma.

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka amemwaga cheche kuhusiana na ufisadi wa ardhi na kuagiza kama kuna
watu wamepora ardhi kwa jeuri ya fedha wajisalimishe mapema.

Prof. Tibaijuka aliyasema hayo jana Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na shughuli mbalimbali za wizara yake, ikiwa ni siku chache baada ya kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete.

"Kama kuna mtu wamepora ardhi kwa jeuri ya fedha, naomba ajisalimishe mapema ili angalau tuweze kuzungumza naye kabla hatujachukua hatua dhidi yake.

"Iwapo anataka kuleta jeuri ya fedha sisi hatubabaiki na wala hatutahangaika naye kwani fedha za mboga tunazo," alisema.

Vile vile aliwataka wananchi wenye taarifa zozote kuhusu uporwaji wa ardhi wazipeleke wizarani ambako zitafanyiwa kazi, na ikibainika ni za kweli sheria itachukua mkondo wake.

"Itabidi tufanye kazi na wananchi, kwani wananchi wasipotusaidia maendeleo shirikishi hatutafika popote," alisema. Ninataka kufanya kazi shirikishi kwani wataalamu pekee hawataweza kumaliza matatizo ya ardhi, bado tunahitaji maoni ya wananchi ili kutekeleza majukumu ya ardhi," alisizitiza.

Prof. Tibaijuka ambaye alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa (UN-Habitat) kwa miaka nane, alionya kuwa kama kazi hazitafanywa kwa udhabiti katika masuala ya ardhi, maendeleo ya nchi hayatafika mbali.

Alisema kuwa kwamba ardhi ni muhimu kuliko fedha na sekta hiyo ni nyeti na mtambuka, hivyo masuala yake yasipofanyiwa kazi kwa umakini, sekta nyingine nchini zitadorora.

Katika moja ya maeneo anayotaka kufanyia kazi ni upimaji wa viwanja na maeneo, kwa kuwa kati ya hekta 900,000 ziliozopo nchini ni asilimia mbili tu zimepimwa.

Kwa mujibu wa Profesa Tibaijuka, upimaji wa ardhi ni hatua muhimu katika kurasimisha mali kama hatua ya kukuza uchumi.

Naye Naibu Waziri, Bw. Godluck ole Medeye alisema kuwa uhuru wa binadamu ni kuishi katika paa lake mwenyewe na kuwataka wananchi kushirikiana na wizara hiyo katika masuala ya ardhi.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Patrick Rutabanzibwa alisema kuwa matatizo ya ardhi ambayo yamekuwa yakilalamikiwa na wananchi Dar es Salaam ni ya kweli na kwamba ndio maana alianza kupangua wafanyakazi baada ya kujua ukweli huo.

Alisema kuwa mambo yaliyokuwa yanafanywa ni kinyume na maadili na kanuni za sheria ya ardhi na kwamba wale aliowabaini kuwa wamepora ardhi aliwataka warudishe.

Alidokeza kitendo hicho ndicho kilichosababisha kuanza kuandikwa vibaya katika baadhi ya vyombo vya habari na kudai kwamba yeye anatekeleza kazi yake na wala si vinginevyo.

Wakati huo huo, wakuu wa idara mbalimbali pamoja na taasisi za Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wametakiwa kukaa vikao vyenye maneno machache, lakini utendaji wa kazi zao uwe juu.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Emmanuel Mchimbi aliyasema hayo jana alipokutana na watumishi wa Wizara hiyo Dar es Salaam.

"Mimi ni kama vile nimeshaharibika, kwani wizara niliyokuwa ninaitumikia ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa nikiwa naibu waziri sikuona maneno

Yaani kule maneno kidogo kazi zaidi, kwani wanajeshi ndivyo walivyo, hivyo ninataka na hapa maneno yawe kidogo utendaji kazi uwe juu," alisisitiza.

Dkt. Mchimbi aliwataka wakuu wa idara kuakikisha wanasimamia vilivyo makujumu yao huku wakishirikiana vyema na wafanyakazi wa wizara hiyo kufikia malengo yaliyojipangia na hatimaye tija ya kazi ionekane.

Alisema kuwa kila mtu anatakiwa kutekeleza majuku yake aliyopewa ili wizara hiyo iweze kusonga mbele.

4 comments:

  1. pETRO eUSEBIUS mSELEWADecember 1, 2010 at 9:42 AM

    Prof.Tibaijuka unaanza kukosea.Huo mtindo wa kuwaomba watu wajisalimishe amekupa nani? Tumeshawazoea nyinyi CCM..mnapenda sana kuhadaa watu kwa mambo ya kusadikika.Kwani nani hajui mlipotuambia kuwa kuna Kampuni zimesajiliwa lakini wamiliki hawajulikani? Sasa kujisalimisha wenyewe maana yake ni kuwa walifisadi ardhi hawajulikani Serikalini? Mazungumzo ya nini kufanyika kati ya mafisadi na Serikali wakati Serikali yatakiwa tu kuwashughulikia wahusika? Kujisalimisha hakumaanishi kuwa anayetakiwa hajulikani? Sasa kama wahusika hawajulikani,ufisadi wa ardhi unaosemwa na Serikali umegunduliwaje? Kwa heshima kubwa kwako Prof.Tibaijuka na nikitambua uwepo wa tambo za kihaya,nalazimika kukupinga kwa hili na utaratibu unaotaka kuutumia.Kama unaamua kufanya kazi(ambazo wewe waziweza) basi fanya bila kutumia mikwara ya kipolisi.Hiyo waachie akina Afande Said Mwema na Kova.Usipojirekebisha,nitakuongeza kwenye orodha yangu ya wasanii mahiri wa hapa Tanzania katika tasnia ya Siasa.Subiri uone.

    ReplyDelete
  2. Katibu Mkuu wizara ya Ardhi anaongoza kwa uporaji wa viwanja akishirikiana na wenzake. Tunaomba ukabila usitumike kumlinda. tutawasilisha ushahidi kwako mama.

    ReplyDelete
  3. Mselewa. Kwa mara nyingine umekosea.Prof Tibaijuka anatumia mkakati wa kimataifa wakati ambapo ufisadi ukiwa mwingi sana basi mwanzo unawashauri wahalifu kusalimu amri. Hii husaidia kwa njia mbili: kwanza, huondoa haja ya kwenda mahakamani kwani kesi huchukua muda mrefu. Kama mhalifu aliyepora mali ya taifa akirejesha basio sawa - ardhi inatejea katika mikono ya taifa.Kwa mfano kama watu 1,000 wameiba mali ya taifa itabidi kufungua mashtaka idadi hiyo ! Pili, wale ambao wanatamani kuiba upya watakuwa na hofu kuwa sasa serikali iko macho. Watakuwa na wasiwasi. Muhimu ni kuona Waziri atachukua hatua gani dhidi ya wale watakaodharau matamshi yake.Tusubiri kuona hatua atakazochukua. La kushangaza nikuwa waziri hakutoa muda maalumu:mfano, wasiporudisha ardhi baada ya mwezi mmoja tutawachukulia hatua. Lazima pawepo deadline. Ndugu, hata hivyo ingekuwa bora tuwe na subira huku macho yetu yakiangalia kwa makini. Baada ya mwezi moja hivi uliza waziri wangapi wamo katika mikono ya vyombo vya usalama. Kwa ufupi, wape mawaziri hawa kamba ndefu ambayo baadaye itatumika kuwasakama. MA

    ReplyDelete
  4. Mama prof, tibaijuka umewatisha vizuru lakini hujawapa mda au mpaka uwajue? ni akina nani wengine wanaweza kuwa ndugu zako utafanyaje? swala ni kwamba hakuna mazungumzo hapo ni kurudisha tu au kunyang,nywa kabisaa. lakini isiwe nguvu ya cocacola kesho na keshokutwa kimyaa, tunakutoa.

    ReplyDelete