01 December 2010

Kamati Kuu yasogezwa mbele

Na John Daniel

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimelazimika kuahirisha Kikao cha Kamati Kuu (CC) iliyotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam leo kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kupata
nafasi zaidi kushughulikia suala la Katibu Mkuu wa chama hicho.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu suala la Katibu Mkuu wa chama hicho imekuwa ni mtihani mzito huku, Bw. John Chiligati aliyeripotiwa kuandaliwa kurithi mikoba ya Bw. Yusuf Makamba kudaiwa kutopenda nafasi hiyo.

Ilielezwa kwamba baadhi ya wazee wa chama hicho walimtaka Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, kumshawishi aliyekuwa Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Bw. Abdulrahman Kinana kushika nafasi hiyo.

Ilielezwa kwamba Bw. Kinana anatakiwa kushika wadhifa huo kutokana na uwezo wake mkubwa na upeo wake kuhusu hali ya kisiasa huku yeye mwenyewe akidaiwa kukataa nafasi hiyo kutokana na sababu mbalimbali.

Sababu kubwa iliyotajwa kumfanya Bw. Kinana kukataa kushika wadhifa huo ni kutokana na mwenendo wa baadhi ya wanachama wa chama hicho kuunda makundi kwa ajili ya kusaka urais mwaka 2015 huku wakiwa hawana sifa za uzalendo na uaminifu.

Ilielezwa kwamba Bw. Kinana anao uwezo mkubwa wa kuendesha chama hicho na kuvunja makundi na kwamba hayuko tayari kuona baadhi ya watu wakiendesha kampeni chafu za kujiimarisha kinyume cha maadili, hivyo kukubali nafasi hiyo itampa wakati mgumu zaidi.

Majira imekuwa katika harakati za kumtafuta Bw. Kinana kwa siku tatu sasa bila mafanikio huku simu yake ya mkononi ikiwa imezimwa.

"Mheshimiwa Kinana alisafiri nje ya nchi baada ya uchaguzi, hayupo hata nyumbani kwake, lakini pia alishakataa ukatibu mkuu, uenda mwenyekiti mwenyewe (Rais Kikwete) amshawishi sana ila alionesha wazi kukerwa na baadhi ya vitu ndani ya chama," kilisema chanzo chetu.

Majira ilipomtafuta Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi, Bw. Chiligati ili kupata ufafanuzi wa taarifa hizo, alisema Kikao cha Kamati kuu sasa utafanyika baada ya maadhimisho ya sherehe za Uhuru wa Tanzania Desemba 9.

"Ninachojua ni kuwa uenda Kamati Kuu itakutana baada ya sherehe za Uhuru Desemba 9," alisema Bw. Chiligati.

Alipoulizwa sababu za kuahirishwa kwa kikao cha leo alisema hakukuwa na taarifa rasmi kuhusu kikao hicho na kwamba suala la mabadiliko ya uongozi, hususan Katibu Mkuu halipo kwenye agenda wala halijafikiriwa.

7 comments:

  1. pETRO eUSEBIUS mSELEWADecember 1, 2010 at 9:47 AM

    Kunaweza kufanyika uchakachuaji hapa.Kwa maana kila unapotokea usogezwaji mbele wa tukio ambapo CCM wapo,tumeshazoea kuona au kusikia uchakachuaji.Hapa pia kuna harufu ya hilo.CCM jamani,uchakachuaji hadi ndani kwenu wenyewe?!

    ReplyDelete
  2. Majira ni gazeti zuri sana halichakachui maoni. Nawaomba Watz wawe makini wanapojadili jambo,huyo pETRO hapo juu hata haeleweki au haelewi maana ya kuchakachua,inaelekea kaimbishwa na yeye anaimba

    ReplyDelete
  3. Kuchakachua maana yake ni kuondosha uhalisia, kama maziwa kuyatia maji, au ku-dilute juice na maji kwa maana hiyo Petro umekusudia kusema CCM wana haribu mambo yao wenyewe au vipi? au ndio neno tu la mjini limeingia basi na wewe unafuata mkumbo? toa ufafanuzi tusikuone juha!

    ReplyDelete
  4. Ni zuzu tu huyo Petro! Cha msingi ni habari iliopo! Nafasi ya Katibu Mkuu ni muhimu kwa CCM lakini Makamba hafai, nawapongeza CCM kwa kuliona hilo! lakini nashangaa kuona wanahangaika juu ya substitution yake wakati wana hazina kubwa viongozi! suala la raisi 2015 haliepukiki, lazima tu mchakato utakuepo! sasa hofu ni ya nini? hicho kiti si cha mfalme kama akifa atarithiwa na Ridhiwani, CCM itapiga kura kumchagua competitive candidate mwisho wa siku!

    ReplyDelete
  5. Nafasi ya ukatibu mkuu wa CCM ni muhimu sana kwa sasa,kwa sababu Makamba hafai hata kuwa katibu wa shina,Yeye ndiyo analeta mgawanyiko CCM,yeye amechangia CCM kupoteza majimbo kwa Chadema na sio spika Samuel Sita,Amesahau katibu mkuu wa CCM taifa lazima uwe na STAHA,UTU,HESHIMA,UVUMILIVU,BUSARA,HEKIMA NA MUELLEWA WA MAMBO(KUSOMA NYAKATI)yeye Makamba hana hata kitu kimoja kati ya hivyo! Watu walishindwa kwenye kura za maoni yeye anawarudisha wagombee ubunge na matokeo ndiyo tumeyaona!

    ReplyDelete
  6. Mnamshambulia Petro bure.CCM walijua kuwa makamba hafai kabla ya uchaguzi.Lakini kwa vile kuna kundi la watu lilitaka kuchakachua matokeo ya kura za maoni,likalazimisha makamba abaki.Sasa kundi hilo hilo linavuta subira kumtafuta mtu wao atakayepitisha mambo yao 2015.Ndio maana Petro anasema kuna uchakachuaji wa nafasi hiyo.SIKIO LA KUFA HALISIKII DAWA NA NDIO MAANA WOOTE WENYE AKILI HAWAITAKI NAFASI HIYO MWAFIKIRI WANAOGOPA NINI???MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA

    ReplyDelete