Na Mwandishi Wetu, Dodoma
MAMIA ya wanachuo kutoka vyuo vikuu na taasisi mbalimbali za elimu ya juu mkoani Dodoma, walifurika kwa wingi kuhudhuria tamasha la muziki la Str8Muzik Festival Inter-College
Special 2010, lililofanyika juzi usiku kwenye Ukumbi wa Royal Village mjini hapa.
Tamasha hilo hufanyika kila mwaka ambalo linalenga kuwakutanisha wanachuo kubadilishana mawazo na kuburudika pamoja hudhamini na Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC), kupitia sigara yake ya Sweet Menthol (SM).
Katika tamasha hilo msanii wa kizazi kipya Hamisi Mwinyijuma 'Mwana FA', Joh Makini 'Mwamba wa Kaskazini' na Michael Ross wa Uganda walikuwa kivutio kutokana kutawala vyema jukwaa.
Msanii Mwana FA aliwapagawisha mashabiki kwa nyimbo zake za Vile ‘Naongea na wewe’, ‘Usije mjini’, ‘Alikufa kwa ngoma’, ‘Mabinti’ na ‘Unanitega’.
Tamasha hilo linatarajiwa kuhitimishwa Jumamosi jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Posta Kijitonyama, Dar es Salaam ambapo wasanii kutoka Marekani T-Pain, Mims, Elephant Man na Gyptian wanatarajiwa kutumbuiza.
No comments:
Post a Comment