Na Amina Athumani
KLABU za kuogelea za Tanzania Bara, zimeendelea kushikilia rekodi za ubingwa wa Muungano za mchezo huo, ambapo klabu ya Talis ya Dar es Salaam juzi imetawazwa kuwa
mabingwa wapya wa michuano hiyo.
Michuano hiyo ya Muungano ilianza, mwaka 2006 na tangu kuanzishwa kwake klabu za Tanzania Bara, ndizo zimefululiza kuchukua ubingwa huo na kuiacha Zanzibar ikiwa nyuma yao.
Awali ubingwa huo ulikuwa ukishikiliwa na Klabu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Nafasi ya pili ya katika mashindano hayo ilichukuliwa na Stingrays A na ya tatu nayo imekwenda kwa Stingrays B, ambayo hivi karibuni ilinyakua medali 74 katika mashindano ya wazi ya kimataifa yaliyofanyika nchini Malawi.
Katika mashindano hayo, Anna Mart wa Stingrays alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa kike anayechipukia na Lewis Mcara wa Talis alichukuwa mchezaji bora kwa wanaume.
Pia michuano hiyo ilitoa wachezaji bora mbalimbali kwa wanawake na wanaume ambao walipewa makombe. Mashindano hayo yalishirikisha timu kumi.
No comments:
Post a Comment