CAIRO, Misri
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limesema nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), imejitoa katika kinyang'anyiro cha kwania kuandaa fainali za Matifa ya
Afrika za mwaka 2015 ama 2017 na kuziacha mbio hizo, kushindaniwa kati ya Morocco na Afrika Kusini.
Shirikisho hilo lilisema kuwa hata hivyo Januari, ndipo litakaa na kuamua nchi ambayo itaandaa michuano hiyo.
Michuano ijayo ya fainali za Matifa ya Afrika 2012, inatarajiwa kuandaliwa kwa ushirikiano kati ya nchi za Equatorial Guinea na Gabon ikiwa ni baada ya michuano kuamuliwa kufanyika kila baada ya miaka miwili, huku michuano ya mwaka 2013 ikiwa tayari imekabidhiwa kwa Libya.
Morocco na Afrika Kusini, zimewahi kuwa na ushindani mkubwa wa kuandaa fainali za Kombe la Dunia 2010 na nafasi hiyo ikaangukia kwa Afrika Kusini na pia nchi zote mbili, zimewahi kuandaa fainali hizo za Mataifa ya Afrika ambapo, Morocco iliandaa michuano hiyo mwaka 1988 huku Afrika Kusini, ikiandaa michunao hiyo mwaka 1996.
No comments:
Post a Comment