24 November 2010

Shahidi wa Mramba abanwa mahakamani.

Na Peter Mwenda.

SHAHIDI wa 13 katika kesi ya matumizi mabaya ya madaraka inayomkabili Waziri wa Zamani wa Fedha, Bw. Basil Mramba jana alipata wakati mgumu baada ya kubabaika mara kwa mara kujibu maswali ya
Wakili Hubert Nyange anayemtetea mshitakiwa.

Bi. Christile Shelukindo ambaye ni Kaimu Kamishna wa Kodi wa Manispaa ya Kinondoni alieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa kiasi cha bil. 11.7 kilitokana na hesabu zilitakiwa zilipwe serikalini.

"Kiasi hiki sh. il. 11,752,350,114 ndicho Kampuni ya Alex Stewart ilitakiwa ilipe serikali, tuliwajibu PCCB barua yao ya kutaka mahesabu halisi waliyotakiwa kulipa," alisema Bi. Christile.

Wakili: Hizo Financial statement ambazo uliletewa na PCCB zilikuwa zimesainiwa na nani?

Shahidi: Sikuziona

Wakili: Kwanza ulisema nyaraka hizo ulizipokea wewe na kuzifanyia kazi na sasa unasema hukuziona je, ukweli ni upi?

Jopo la Mahakimu watatu wanaosikiliza kesi hiyo akiwemo Jaji John Utamwa walishtuka kusikia shahidi huyo kukiri kuziona hesabu hizo na baadaye kukataa kuwa hakuziona.

Ndipo Jaji Utumwa alipiomuuliza je, unafuta usemi wa kwanza kuwa hesabu hizo hukuziona?"

Shahidi alikaa kimya na baadaye kujibu ndiyo. Ndipo wakili Nyange alipotaka aeleze mahakama nyaraka zilizotumika kubaini msamaha wa kodi wa sh bil. 11.7 ulitokana na mahesabu kutoka TRA au kampuni ya Alex Stewart.

"Unasema ulipokea barua kutoka PCCB ikikutaka upige mahesabu je, alikuwepo Ofisa wa Kampuni ya Alex Stewart? au mmepiga mahesabu kutoka mahesabu ya TRA, je, huoni kuwa hizo si hesabu halali?

Shahidi: Hapana.

Katika kesi hiyo ambayo shahidi huyo anaendelea kutoa ushahidi leo Bw. Mramba, Waziri wa zamani wa Madini Bw.Daniel Yona na Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha Bw. Gray Mgonja wanakabiliwa na kesi ya kusababisha serikali hasara ya sh. bil. 11.7 wakati wakiwa madarakani.

3 comments:

  1. pETRO eUSEBIUS mSELEWANovember 24, 2010 at 12:15 PM

    Shahidi ameshanunuliwa huyo...hana lolote.Y jana tu ndo asahau kama alisema aliziona,leo akatae?! Mramba huyoooooooooo uraiani huru!

    ReplyDelete
  2. Makamba acha ufisadi, siunaona jinsi shahidi wako anavyoshindwa kujieleza inaonyesha jinsi gani mlivyogawana hizo fedha?

    Hizo fedha zingeweza kusaidia miradi mingi sana lakini kutokana na huyu Makamba na wenzako wasio na uchungu na nchi yetu wameamua kuzichakachua.

    Lakini lazima kieleweke tu wakili nakuomba kuwa makini sana wabane hao mashahidi maana wanachaoonge ni uongo tupu, nadhani wamepewa nao hizo pesa.

    Jamani viongozi wetu tunawaomba muwe makini sana katika kuulinda uchumi na kutumia vizuri mali ya Taifa letu. oya Makamba na wenzako lazima mrudishe hizo fedha. Na haufai kabisa kushika nyadhifa yoyote ya uongozi hapa Tz.
    God bless Africa,God bless Tz, Amin BIG UP SANA WAKILI

    ReplyDelete
  3. Mhando Antony.

    Kesi hizi dhidi ya hawa wenye fedha ni Kiinimacho tu. Mwenye pesa siku zote ana haki na ushahidi hautoshi kumtia hatiani. We iba kuku uone hukumu itakavyotoka baada ya siku 2. Muda wote huo bado kesi ya Mrambaaaaaaa, kesi ya Mrambaaaaa! Mwachieni huru tu, kwani tunajua serikali ni ufisadi mtupu. Kesi ya fisadi,isikilizwe na fisadi; haki itapatikana?

    ReplyDelete