19 November 2010

Pinda aapa, CHADEMA wasusa.

Na John Daniel, Dodoma

RAIS Jakaya Kikwete, amemwapisha Waziri Mkuu Mizengo pinda kwa kumkabidhi rasmi Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ikulu ya Chamwino mjini hapa tayari kuanza
kazi.

Jumanne wiki hii baada ya kuteuliwa na kuthibitishwa na bunge mjini hapa, Waziri Mkuu Pinda aliweka wazi changamoto kubwa inayomkabili kama kiongozi wa shughuli za kila siku za serikali kuwa ni kushughulikia vikwazo na kero za wakulima, wafugaji na
wavuvi walioko vijijini ambao bado wanakabiliwa na umasikini zaidi.

Licha ya umati mkubwa uliohudhuria hafla hiyo, wabunge na viongozi kutoka vyama vyote vyenye uwakilishi bungeni na visivyo na
uwakilishi, wale wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambao tayari wametangaza kutomtambua Rais Jakaya Kikwete kama rais, hawakuonekana.

Vyanzo vya habari vya Majira vilieleza kuwa sababu ya wabunge wa CHADEMA kutokwepo katika hafla hiyo ulitokana na msimamo wao wa kutoitambua serikali huku baadhi yao wakishinikiza wasitishe msimamo huo, hivyo kuwalazimu kuwa na kikao cha dharura kujadili suala hilo.

Ilielezwa kwamba wakati wa hafla ya kumwapisha Waziri Mkuu wabunge hao walikuwa na mvutano wao kwa wao katika ukumbi namba 219 maarufu kama ukumbi wa Chief Kasusura, pamoja na mambo mengine wakipanga ama watoke nje wakati Rais Kikwete atakapoingia bungeni kuzindua bunge la 10 au la.

Kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni Bw. Freeman Mbowe hakuwa tayari kutoa ufafanuzi wa kina juu ya taarifa hizo za mvutano kati yao kuhusu msimamo wao wa kutoka nje Rais akiingia ukumbini.

"Sisi tulikuwa kwenye kikao kweli, tulikuwa tukijadili mambo ya mustakabali wa taifa hili, kama hilo nalo ni mojawapo ya masuala muhimu katika mustakabili wa Taifa basi tulilijadili," alisema Bw. Mbowe kwa kifupi bila kutoa ufafanuzi wa kina.

Wakati hayo yakiendelea, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Bw. Edward Lowassa, alikosoa mpango wa Kilimo Kwanza na kueleza kuwa mkakati huo hauwezi kuleta tija inayokusudiwa bila elimu na kusisitiza kuwa sekta ya elimu ndiyo inayoapaswa kupewa kipaumbele cha kwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya Bw. Pinda kuapishwa, Bw. Lowassa alisema nchi nyingi zilizokuwa masikini kama Tanzania zimepiga hatua ya kimaendeleo haraka baada ya serikali kuamua kuwekeza na kutoa kipaumbele katika sekta ya elimu.

Kwa upande wake aliyekuwa Spika wa Bunge wa tisa Bw. Samuel Sitta, aliweka wazi matumaini yake makubwa kwa Bw. Pinda na kusisitiza kuwa uteuzi wake hauna dosari kwa kuwa kazi aliyofanya katika kipindi cha miaka miwili na nusu ni nzuri.

"Nilishasema katika bunge lililopita mkutano wa 20 kuwa katika uteuzi wa Waziri Mkuu Mhe. Rais hana sababu ya kuumiza kichwa, kazi aliyoifanya ni nzuri na ni kiongozi makini, kikubwa sasa ahakikishe tu nguvu nyingi zinaelekezwa kwa wakulina na sekta ya elimu, na hilo nina hakika atalifanya," alisema Bw. Sitta.

Kwa upande wake Waziri Mkuu mstaafu Bw. John Malecela, alimpongeza Bw. Pinda na kumtaka aangalie namna ya kushughulikia tatizo la ongezeko kubwa la vijana mijini huku wengi wao wakikosa shughuli za kufanya kutokana na ukosefu wa ajira.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba alisema licha ya kumpongeza Bw. Pinda, anaiomba serikali kuangalia upya uundwaji wa Tume huru ya Uchaguzi ili kutoa nafasi kwa demokrasia kufanya kazi nchini.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Makamu wa Rais, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Pili, Balozi Seif Ali Iddi, mabalozi, makatibu wakuu, wakuu wa mikoa na viongozi wengine wa serikali.

21 comments:

  1. Kama kura zilichakachuliwa ni haki yao kuwaonyesha watanzania kwa maana Chadema ni chama kinachopenda amani na ndio maana wameamua kuchukua hatua za kistaarabu kama hizo za kutoka nje ya ukumbi wa Bunge. CHADEMA OYEEEEE

    ReplyDelete
  2. CHADEMA mmeonyesha jinsi mlivyo na uchungu na inchi hii, maana CCM wamekuwa wakifanya mombo yote kiwizi na kibabe. Lakini wjue hawatatawala milele inchi hii, mwisho wao umekwisha wajiandae kung'oka kwa vyovyote vile. CCM wamelazimisha kutawala inchi baada ya kuiba/kuchakachua kura za watanzania ambao hawakuwachagua.Lakini wajue ya kuwa mwenye fikra nzuri na anaye elewa mambo haya yote hatawaliki hata kidogo nisawa na kutawala kumtawala simba porini.

    ReplyDelete
  3. inanishangza Rais wetu Kitwete kulivalia kibwebwe suala la udini wakati halipo, anatupeleka wapi watanzannia

    ReplyDelete
  4. Huyo siyo rais wetu ni rais wa mafisadi labda na wanyama wa porini maana hatukumchagua sisi htumjui.

    ReplyDelete
  5. suala la udini liko wapi nchini! mbona ccm chini ya mwenyekiti wao wanalikuza sana? kuna nini tunaomba watuambue watanzania,kwani walizusha sana suala la umwagaji damu wakati wa kampeni wakati hakuna aliyekuwa na mkakati huo, mbona CCM wanapenda kutumia lugha ambazo zinataka kuwafanya watanzania wasidai haki zao?kwa nini wanapeleka mawazo ya watu kuanza kuchokonoa suala ambalo ni dhana ya wanasiasa kutaka kuwagawa watanzania ili CCM wadumu madarakani hivi wanayo hati miliki ya nchi hii? kila wakitaka kukoselewa wanazua kutokea kwa vita na udini, jamani siyo hivyo achane kutumia njia hiyo kuwaadaa wananchi ambao hawajawa na upevu katika mambo ya siasa. mimi nadhani suala la udini linataka kukuzwa na CCM ili watanzania wasiwaamini walioko mstari wa mbele kuwatetea .Tunawaomba CHADEMA wasonge mbele ila wapunguze migomo isiwe mingi sana badala yake watumie hoja kama walivyofanya katika Bunge lililopita ambalo liliibua zaidi uovu wa CCM na kufanya baadhi ya mawaziri kujiuzulu, tumia njia hiyo jamani kuwaelimisha wananchi watawaamini zaidi kuliko migomo.

    ReplyDelete
  6. nasikitishwa na kitendo cha mkuu wa nchi kuwa mbeya, mnafiki na mchonganishi. NAOMBA AJE ATUELEZE WATANZANIA KWA UNDANI SANA SUALA LA UDINI. MIMI LINANIU MA SANA

    ReplyDelete
  7. chadema wamefanya jambo la kijasiri na kama watanzania wote tungekuwa na uchungu kama hawa jamaa tungekuwa mbali sana kwa mtazamo wangu chadema wamefanya la msingi ili kuumbua mabaya ya chama cha mafisadi.

    ReplyDelete
  8. Hili swala la udini, ni dnganya toto tufanye kama wenzetu wa zanzibar.nasahangaa wabunge wa chama tawala wanshangilia uovu.ipo siku chama cha mapinduzi kitakuwa ni chama cha upinzani, mwisho wa uchaguzi huu, mwanzo wa kampeni 2015. Hongera chadema jengeni hoja za nguvu kupambana na hao mafisadi." dont give up"

    ReplyDelete
  9. Mh Rais kweli ulikolipeleka hili taifa au unakolipeleka sio kuzuri kwa sababu hao wapambe wako watakufanya CCM ikufie mikononi, mh kaa chini ufikirie tena, hii kauli yako ya udini wengi wanakuangalia na wanakupima unalengo gani kila kukicha dini dini. Unajua mchuwa anapokula ni lazima ajifungie ndani ili adui yake asimuone. Sasa hatujui una lengo nzuri au baya au nini umekiona wewe kuhusu hii dini tupe mfano sehemu yenye matatizo ya dini. Viongozi wa dini hasa ukristo kuweni macho na huyu mtu. Sijasikia mkristo analiongelea hilo suala ila ni yeye na wanzake tu kwa nini? Ndugu zangu watazania tuombe mungu tuvuke hili daraja vizuri tusije fika katikati likavunjika tukaanguka kwenye mto mamba wapo midomo wazi, mate yanawashuka. MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.

    ReplyDelete
  10. kikwete mwenyewe ni mtu anae endekeza udini kwani katika hatua za mwanzo za uteuzi wa wabunge 3 wote ni watu wa imani moja.je huo si udini au tusemeje?

    ReplyDelete
  11. KWeli kikwete umekwisha

    ReplyDelete
  12. watanzania msiwe wepesi wa kusahau mwaka 1995 mwalimu alimkataa kikwete,hakuwa akimaanisha kuwa wakati wake bado ila si mtu wa kufaa kuiongoza nchi hii,ndio maana kipindi chake amekuwa ni mtu wa matumizi makubwa na kuendeleza serikali ya kivikundi kmv.kuigeuza CCM kuwa mali ya familia yake,kwani hata mfumo mzima wa kampeni ziliratibiwa na familia bila kujali masilahi ya wengi.hivyo tz imemua kuchezea miaka 10 hii bure.tumuombe nungu amalize haraka aende zake tujaribu kutafuta kiongozi mwingine

    ReplyDelete
  13. CCM na Kikwete ndio wanaoendekeza udini,sijasikia chama kingine chochote au hata dini yeyote ikisema eti mtu fulani anafaha kuliko wa dini nyingine ila nimesikia kwa kikwete,kwa ccm,kwa Gazeti la mtanzania ambalo linamilikiwa na mafisadi.Hao ndio wanaosema udini,laakini pia tusitishwe na kauli hizo wala tusivurugwe kwa kigezo cha udini kwani hakipo hizo ni fikra za kujilinda kwa ccm na JK.ebu angalia safu ya ccm,ebu angalia wabunge watatu wa kwanza wa kuteuliwa,si tunaona,si tuna akili ya kutambua.Mbona watu hajalalamika??angalia magazeti yanayoandika mambo ya udini udini wamiliki wao ni nani si wale wale,ambao kwa miaka 5 hawakutoa mchango wo wote bungeni ila wanaamrisha magazeti yao kutunga hoja za uongo ili kulinda maslahi yao.Je kama wanawasemea wananchi kwa nini mtu ukae bungeni miaka 5 bila hoja yeyote,au hata kuchangia hoja za wenzako.Tuwe makini ccm inataka kuvuruga jitihada za wananchi kupambania haki zao.na tumewagundua pamoja na wafuasi wao wenye kumiliki vyombo mbalimbali vya habari.Mwisho wenu umefika lakini hata kama hamtaki kuondoka kwa demokrasia lakini umri utawaondoa tuuuu.Hamtaishi milele kutoonea watanzania na kutuvuruga.

    ReplyDelete
  14. RAIS KIKWETE AWE MKWELI AACHE KUSEMA MANENO YA KWENYE KHANGA AU TAARABU NI WAPI WATU WAMEPIGA KURA KWA IMANI ZA DINI YEYE NDIYE ANAYECHOCHEA MAMBO HAYO ANAENDEKEZA UDINI HASA UISLAAM UNA HATA UTEUZI WAKE WA WABUNGE WATATU WA AWALI WOTE WAISLAMU HALAFU HUYO MEGHJI WA NINI AU KULIPA FADHILA KWA MTOTO WAKE AMBAYE ANAMAHUSIANO NAYE?KWANZA ALIONDOLEWA KWA UFISADI WA FEDHA ZA EPA SASA ANAMTAFUTIA NAFASI YA ULAJI HUO NDIYO UDHAIFU WA RAIS KIKWETE.WABUNGE WA CHADEMA KUSUSIA SHEREHE SI KOSA HAWAKUTUMWA NA WANANCHI KUHUDHURIA SHEREHE BALI KUPELEKA KERO ZAO SERIKALI HASA KATIKA VIKAO VYA BUNGE WANGEKOSA KUHUDHURIA VIKAO VYA BUNGE HAPO SAWA TUNGEWAHOJI,SHEREHE HATA KAMA UMECHANGIA HUKUCHANGIA MCHANGO UKINIALIKA NIKASHINDWA KUJA HASARA YAKO NINI?ACHENI MBWEBWE CHANBUENI MAMBO KWA VIGEZO NA SIYO USHABIKI.TUMSIFU WA MASWA,SHINYANGA.

    ReplyDelete
  15. Kiwete ni mdini wa kupindukia aache unafiki autafute huo udini wa wenzake auanike kama atakosekanamo, ni mnafiki sana huyu rais wa ccm. Chadema kutoka bungenii endeleeni mpaka huyu rais wa ccm aharishie mlango wa Bunge.Chadema oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee,People's powerrrrrrrrrrrrrrr.

    ReplyDelete
  16. Tatizo la nchi yetu si hotuba murua na maridadi bali utekelezaji wa hoja. Mh. Rais punguza safari tatua matatizo ya wananchi kwanza. Iga kwa Mwai, Kagame na Chaves. Tulia fuatilia masahibu ya wanyonge. Ukisafiri tu Mafisadi wanachanga karata. Chadema tunawapa support kwa sana tumechoka kuwa mabwana ndiyo mzee!

    ReplyDelete
  17. Suala la udini lipo. aliyelianzisha suala la udini ni JK. Ndiyo maana Mwalimu alimkataa. Mpaka sasa viongozi wote wajuu kutoka zanzibar na huku bara wote ni Waisilamu. vyeo vidogo vidogo ndiyo wanapewa kina Pinda kama watu wa kutumwa tu.

    Wizara zote nyeti watu wa dini hiyo hiyo. Mdini ni Kikwete!

    ReplyDelete
  18. mdini ni JK JUZI KATEUA WABUNGE 3 WAISILAMU NA HAO ANAWAPA MADARAKA YA UWAZIRI. SUBIRINI MTAONA.

    ReplyDelete
  19. Jk viongozi wengi anachagua waislamic anaacha wakristo, ukiangalia zanzibar wamejazana waislam, Kwa kweli swala la udini ni Jk analiendekeza na hili lipo kwake. jamani watanznia tunaangamia sasa Taifa hili likianza kuongozwa na dini moja na hao ndio mafisadi wanao turubuni sisi wanachi.

    Naomba hili jambo liangaliwe sn, wapeni wakristo nafasi za uongozi wote ni wa Tz hakuna Mkenya Au Mzambia kwanini dini moja ijazane katika serikali moja? na huku wote ni Taifa Moja?

    ReplyDelete
  20. Baadhi ya waandishi wanamlaumu JK kwa kuanzisha hoja ya udini. Lakini hapo hapo wanamshambulia JK kwa kuwateua wabunge watatu ambao wanasema ni waislamu. Hawasemi ni watanzania! Mbona darubini yenu ina misingi ya kidini! Pia hawataji majina ya wateuzi wengine wa JK - ikiwa pamoja na Waziri Mkuu,Spika, Mkuu wa Uchaguzi, pamoja na wateuzi wengine wa bunge. Tatizo la dini na ukabila limeleta hasara kubwa Afrika na pia ulimwengu. CCM ni mashuhuri kwa sababu tangu awali ( Hata Tanu) ilitambua hatari hiyo na ikachukua hatua.Ndiyo maana Tanzania inasifika.Tuache unafiki: baadhi ya vyama vyama vya upinzani vilitumia mbinu hizo mbovu.
    MPENDA AMANI - London

    ReplyDelete