BAGHDAD,Irak.
INARIPOTIWA kuwa makubaliano ya kugawana madaraka nchini Irak yanaashiria kusafiri kwa nguvu za ushawishi kutoka kwa Wamarekani kwenda kwa Wakurdi na Wairani
Kwamujhibu wa duru za kimataifa hatua hiyo ni kutokana na kitendo cha siku chache, Wakurdi kufanikiwa kuandaa mazungumzokufanikiwa kufanya lile ambalo Marekani na Iran na marafiki wengine majirani wa Irak walishindwa kufanya katika kipindi cha miezi nane ya majadiliano ya kidiplomasia.
Inaelezwa kuwa walifanikiwa kuwashawishi viongozi wa vyama karibu vyote vya bunge nchini humo kukaa kwa pamoja kwa mara ya kwanza tangu uchaguzi uliofanyika mwezi Machi.
Indaiwa kwamba makubaliano yaliyopatikana katika mazungumzo hayo yanaonekana kuutatua mzozo wa kisiasa nchini humo ijapokuwa kwa muda mfupi.
Lakini hata hivyo chama kilicho na idadi kubwa ya wafuasi nchini humo Al-Iraqiya kilicho na idadi kubwa ya watu wa dhehebu la kisunni, kinaonekana bado hakijafurahishwa na mamlaka kinachopewa katika makubaliano hayo mapya.
Chama hicho cha Al Iraqiya kinachoongozwa na aliyekuwa Waziri Mkuu,Bw. Ayad Allawi kiliibuka cha kwanza katika uchaguzi huo wa Machi wa bunge kikijinyakulia viti 91 lakini kikapata upungufu wa idadi ya viti vinavyohitajika 163 ili kuweza kuunda serikali.
Wakati haya yote yakiendelea ukumbusho mkubwa wa kupungua kwa ushawishi wa Marekani nchini Irak umejitokeza kutoka kwa Wakurdi ambao wametajwa kuwa marafiki wa karibu wa Marekani.
Licha ya kile viongozi wakikurdi wametaja kuwa shinikizo kubwa kutoka kwa Marekani na marafiki wake wa nchi za kiarabu walio karibu kama vile Uturuki, kutaka Bw. Allawi awe rais, mwishowe kiongozi wa Kikurdi Bw. Jalal Talabani alichaguliwa kuwarais wa nchi hiyo kwa miaka mingine minne.
Wakati palikuwa na shaka baada ya uchaguzi huo iwapo Wakurdi watafanikiwa kuchukuwa uongozi tena, wameamua sio tu ni nani atakayeiongoza Irak, bali pia wamefanikiwa kuimarisha siasa za nchi hiyo.
Hii inakwenda kinyume na fikra ya kale zilizokuwepo kwa vyama vya kiarabu nchini humo, kwamba nia kuu ya Wakurdi ni kutaka kujitenga na kuwa hawajali kuhusu vurugu zilizopo katika maeneo yasio na wakurdi nchini humo.
Marekani ina wanajeshi wasiofika 50,000 hivi sasa nchini humo na ni katika kiwango cha kutoa ushauri na mafunzo na inatarajiwa kuondoa kikosi chake kizima ifikapo mwishoni mwa mwaka ujao.
No comments:
Post a Comment