22 November 2010

CHADEMA Kilimanjaro yaunga mkono wabunge wake.

Na Gift Mongi, Moshi.

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Kilimanjaro kimetoa tamko la kuunga mkono kitendo cha wabunge wa chama hicho kutoka bungeni wakati
Rais Jakaya Kikwete akizindua bunge.

Kwa mujibu wa tamko lililotolewa na kusainiwa Katibu  wa chama hicho Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Basil Lema kwa niaba ya wanachama wa chama hicho, kitendo kilichofanywa na wabunge hao kamwe kisiangaliwe katika misingi ya kisiasa na badala yake CCM wajiulize kwa nini imekuwa hivyo.

taarifa hiyo ilifafanua kuwa kutokana na hali ambayo wabunge hao wameionesha serikali pamoja na umma wa Watanzania kwa ujumla, tayri wamekwishaanza kufuatwa fuatwa na mamlaka mbalimbali zikiwemo usalama wa
taifa, polisi na makachero.

“Tunajua kuwa baada ya wabunge wetu hawa kuukwaa ubunge hawakuwa na sababu yoyote ya kuanza jambo la aina hii, hasa ikizingatiwa kuwa wanajiweka katika hatari ya kufuatwafuatwa na serikali, usalama wa taifa, na kwa hakika lolote linaweza kuwakuta,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Bw. Lema alisema kuwa kitendo cha wabunge kutoka nje ya ukumbi wa bunge kina lengo la kuiambia jamii ya  Tanzania kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu ulijaa dosari
nyingi zilizofanywa kwa makusudi ili kuipendelea CCM, na pia utoaji wa elimu ya uraia kwamba mfumo wa siasa wa vyama vingi hauwezekani bila katiba inayoendana na mfumo huo.

"Sisi wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro tunapenda kuwaomba wabunge na wanachama wa CCM nchini kote kufungua macho yao ili waone kile ambacho wabunge wa CHADEMA wanachokipigania,” alisema katika taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilisisitiza kuwa wabunge wao hawana uadui
binafsi na Rais Kikwete bali wanachokikataa ni kuendelea kwa mfumo huu kandamizi unaomhakikishia kila mgombea
atakayetokana na chama tawala kushinda.

Aliwataka wanaCCM wajue kuwa mfumo huu unaokilinda chama chao kujihakikishia ushindi kabla ya uchaguzi una malengo ya kiuchumi yanayofaidisha kundi dogo la la mafisadi ndani ya chama.

Tamko hilo liliwataka Watanzania wote kwa ujumla bila kujali itikadi zao kuhakikisha kuwa wanaendelea kuwaombea wabunge wa CHADEMA ili mpango huu 'mtakatifu' ufanikiwe na jamii iweze kujua ni nini kilio cha CHADEMA.

"Tafadhalini sana wapeni moyo wabunge hawa ambao ni wapiganaji na hakikisheni kuwa mnabeba mzigo wa kuona  mabadiliko ya kweli yanatokea Tanzania na tuacheni kuburuzwa bila kujau haki zetu," ilisema sehemu ya tamko hilo.

Tamko hilo linawataka viongozi wa CCM kutunza amani na
upendo uliopo na kusikiliza kilio cha CHADEMA ili kuepusha chuki na machafuko na wasipofanya hilo basi Watanzania na ulimwengu mzima utajua kwamba hawaitakii nchi amani.

4 comments:

  1. WATU WANATAKA KUJIKOSHA KIAINA IONEKANE RAISI HAWANA UADUI NAE!! HIVI UNAPODAI KUWA HUTAMBUI MATOKEO MAANA YAKE KUWA NA RAISI HUMTAMBUI, NA PIA WALISEMA KUWA HATA MAWAZIRI WATAKAOCHAGULIWA NA RAISI HAWAWATAMBUA KWANI KAINGIA MADARAKANI SI HALALI!! WAO KAMA WALIKUWA NIA YAO KUPINGA MATOKEO ILI JAMII IJUWE WANGEFANYA MAANDAMO YA AMANI KWENDA KTK TUME YA UCHAGUZI ILI KILIO CHAO KISIKIKE MAANA WAO NDIO WALIOTANGAZA MATOKEO,IWEJE KTK VIYUO MAWAKALA WALIKUWEPO, KURA ZA WABUNGE MNAKUBALIANA NAZO, LAKINI ZA URAISI HAPANA INAINGIA AKILINI? ACHENI KUJIDANGANYA SASA LEO RAISI ANA KOSA GANI?NA INAONYESHA MTAENDELEA HATA KTK MIKUTANO HUKO MIKOANI MTATAKA KUJARIBU KUFANYA HIVYO WKT RAISI ANAHUTUBIA, NI BORA MUACHE KUHUDHURIA KAMA ALIVYOFANYA ZITTO KULE BUNGENI, JARIBUNI MUONE!!

    ReplyDelete
  2. mzee anonymous huna jipya,kwenye maoni huko nyuma umempamba sana Zito ukasema amekomaa kisiasa huenda watu wakamwita mamluki wa CCm,ila hata kabla ya jogoo kuwika ktk mtiririko wako wa maoni umemwita mamliki wa ccm!Wanachofanya hao Chadema ni kutumia mbinu yeyote inayokubalika kikatiba kuwasilisha madai yao.Sio lazima waandamane kuelekea tume kama njia mojawapo ya kuwasilisha wanachodai,ingawaje hiyo ni njia mojawapo pia mbonA UNATAKA KUWACHAGULIA NJIA YA KUWASILISHA UJUMBE WAO.Hao tume unaosema walalamikiwe si maajenti wa hao CCM?nani kakwambia wamekubaliana na matokeo ya ubunge kama wewe si mbumbumbu!Hujasikia wamefungua kesi tyr mahakamani na bado zitaendelea kufunguliwa.hATA KAMA WAMEPINGA MATOKEO YA RAISI PEKEE WAKAACHA YA UBUNGE PIA NI HAKI YAO KUAMUA WALALAMIKIE LIPI WAACHE LIPI HATA WEWE UKIPIGANA NA MTU UNAWEZA KUMSAMEHE ILA MWINGINE MKAFIKISHANA KUBAYA HAYO YANATOKEA BWANA USITUPOTOSHE

    ReplyDelete
  3. KWA KWELI WA-tz TUNA SAFARI NDEFU KUFIKIA UPEO WA UELEWA JUU YA SIASA ZA VYAMA NA UPINZANI. wENGI NI KIZAZI CHA ENZI ZA CHMA KUSHIKA HATAMU.
    Tatizo liko pia kwa waandishi wetu wa habari.Hawa wanatazamwa na wengi na kuaminiwa kama waelimisha jamii. Wanapaswa kuwa weledi wa kiwango cha juu wa mambo na masuala mengi ya nchi na dunia kwa jumla. Kwa hapa nchini wanapaswa kuzielewa kwa undani kanuni na taratibu za bunge na haki na wajibu wa kila mbunge.Wanapaswa kuelewa kuwa kususia (kikao au msemaji wa serikali)ni mojawapo ya njia za kisatarabu ambazo mbunge (au hata diwani) anazitumia kuonesha kutoridhishwa kwake na jambo, mbinu au hata mtu binafsi. Wabunge wana njia nyingi za kuonesha kupinga au kutoridhishwa kwao na jinsi upotoshaji wa matokeo ya uchanguzi wa rais ulivyofanyika. Wangeweza kubaki ndani ya jengo lakini ama wakaamua kujifanya wamelala, au wakawa wanafanya mambo yao mengine tu, au hata kuamua kumshangilia rais bila mpangilio, na hata kuwa wanaguna mfululizo almradi tu rais asisikike. Hizo ni mbinu zinazoruhusiwa na kanuni za bunge kama tunavyoshuhudia kwenye mabunge menghine yanayofuata mfumo wa Westminster huko INdia, Kenya, Uganda, Zimbabwe hata SA pia. Wenzetu wanafikia kuoneshana ubabe ndani ya bunge kwa kupigana na kurushiana vitu. Je hao wanaowashangaa CHADEMA kwa kuamua kuonesha msimamo wao dhidi ya Kikwete kama Rais (taasisi) na sio kama JMK binafsi, walitaka wabunge wetu hawa nao wawe vigorous?
    WaTZ tunapaswa kuelimishana kila mara kuwa siasa za ushabiki wa vyama hazitatupeleka kwenye maendeleo kamwe.Moja ya madhara ya wazi ya ushabiki wa vyama bila kujali maslahi ya jimbo au nchi kimaendeleo ni kuona kuwa ndani ya bunge la milenia hii kuna wabunge wenye elimu chini ya darasa la saba toka Kilombero, Njombe Kasikazini na Korogwe kupitia CCM. Hivi tujiulize, watu hawa watasaidiaje kusukuma gurudumu la maendeleo katika karne na milenia hii ya www.com?
    Inasikitisha pia unaposikia kuwa nguvu zetu za kiutendaji katika vyombo vyetu wa ulinzi na usalama zinaelekezwa kukiangamiza CHADEMA kwa kujidanganya kuwa tunaondoa wakorofi wa kisiasa, huku ni kujitia kitanzi wenyewe.

    ReplyDelete
  4. Kama judge Mkuu alivyosema kuwa haoni kosa la wabunge hao katika kanuni za bunge wala katika sheria za kawaida za nchi na mimi niseme kuwa watanzania tujifunze kuendesha siasa za kuvumiliana hata pale ambapo unaona kabisa kitendo alichofanya mpinzani wako kisiasa kimekudhalilisha. Ile ilikuwa nafasi ya Chadema kumjulisha Rais wao kuwa pamoja na katiba tuliyoapa kuilinda kukuweka madarakani lakini sisi kama wadau muhimu bado tuna kilio cha kutofurahishwa na utaratibu mzima wa upatikanaji haki ya kweli katika uchaguzi ndani ya nchi yetu. Kwa hili chadema wamefanikiwa kwa kuanzisha kwa nguvu kubwa ya kuhimiza watanzania kuanza kufikiria matatizo yaliyopo katika mchakato wa uchaguzi Tanzania kwa kujiuliza kwa maswali ambayo yalikuwa hayauliziki wala kujadilika katika viunga vya kawaida kabisa miongoni mwa makundi mbalimbali ya watanzania. Pili kurasimisha kauli za waangalizi wa kimataifa ambao kwa kauli zao uchanguzi ulikuwa huru lakini si haki. Hata hivyo kauli ya baadhi ya wabunge wa chadema kutoa maoni binafsi nje ya kikao chao huo ni utovu wa nidhamu na ni kinyume cha "philosophy' ya collective responsbility ambayo imetuasisi kuwa pale ambapo tunakuwa na maoni yetu na tukapewa fursa ya kuyaeleza tukawa sehemu ya majadiliano na hatima ikafikiwa kwa kufanya maamuzi ya kikundi basi sote tutafungwa na uamuzi huo bila kujali maoni yetu, ni unafiki mbele ya jamii kujaribu kujitofautisha na uamuzi wa chama au kikundi chako kwa sababu tu eti unataka kufurahisha wapiga kura wako katika jimbo. Kwa maana hiyo wapo baadhi ya wabunge wa CHADEMA ambao wanaweza kufadhiliwa kwa njia ya kupewa miradi ili wakiuke maamuzi ya Chama. Enzi za Mwalimu Nyerere Tanzania kama nchi ilitupilia mbali msaada kutoka ujerumani Magharibi na Uingereza kwa sababu nchi moja kutaka kutuchagulia rafiki au adui(Wajerumani Magharibi) na Wingereza kwa kuitambua serikali ya Smith Zimbabwe ya leo wakati huo Rhodesia. Serikali kusimamia maendeleo ya wananchi wake sio chaguo ni lazima "it is a crime for parliamentarians to do lobbying to Government officials or to the President himself for development purposes" they can when it comes to soliciting foreign support. Kufanya vizuri kwa Serikali katika maendeleo kwa watu wake hakutoi mwanya/ruhusa ya kuvuruga uchaguzi na kusamehewa, kwamba wananchi wako wanatambua mazuri ya serikali yao hakutoi nafasi ya Mbunge kunyamazia uovu mwingine wa taasisi hiyo. Nina wasamehe wabunge hao kwa leo safari nyingine hao lazima wahesabike kama wasaliti wa umma wa watanzania ambao umewekeza kwenye ushujaa na umakini wao. nimesikiliza hoja za Mhe Shibuda na Mhes. Zito zote ni dhaifu na ni za kukemewa na watu wote wapenda haki hawakukitendea vema chama chao na nafsi zao wenyewe, lazima wakubali gharama ya demokrasia kuwa ndani inafungua milango ya majadiliano lakini maamuzi yakishafikiwa wengi wanapewa na wachache lazima wakubali kifo cha mtizamo wao. Aluta continua Nawapenda sana Wabunge Wachadema kuweni timu moja vinginevyo kifo cha chama chenu kipo njiani

    ReplyDelete