12 November 2010

Mgaya ataka wafanyakazi kuishtaki serikali.

Cresensia Kapinga na Joseph Mwambije, Songea

NAIBU Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya wa Wafanyakazi (TUCTA) nchini, Bw. Nicholas Mgaya amesema wanapanga kuifikisha serikali mahakamani kwa
kulipa mishahara ya wafanyakazi kinyume na makubaliano.

Bw. Mgaya aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa CWT mkoani Ruvum, kuwa Waziri wa Wizara ya Kazi na Maendeleo ya Kazi alitangaza mishahara tofauti na makubalianao yao.

Alisema kuwa wameshakwenda Mahakama ya Kazi na kutoa notisi ya siku 30 ya kutekelezwa kwa makubaliano yao kwenye vikao kati ya viongozi wa TUCTA na serikali kuwa mambo yao matatu ambayo ni kuongezwa mishahara, kupunguzwa kwa kodi na kuhusu madai ya mfuko wa hifadhi ya jamii, yatekelezwe

"Tutaishitaki serikali kwenye mahakama ya kazi na tayari tumeshatoa notisi ya siku thelathini na kinachosubiriwa kwa sasa ni serikali kutujibu notisi hiyo," alisema Bw. Mgaya.

Alisisitiza kuwa watadai madai yao wakiwa ndani ya misingi ya sheria na kanuni na taratibu za nchi zinavyosema bila kuvunja sheria zilizowekwa na kwamba bado wataendelea na madai yao kama walivyopanga mpaka kieleweke.

Akizungumzia utendaji kazi wa Wizara ya Kazi katika awamu iliyopita alisema haukuridhisha, hivyo wanamshauri rais kumteua waziri ambaye atakuwa mchapakazi na mwenye majibu mazuri kwa wafanyakazi.

No comments:

Post a Comment