Na Mhaiki Andrew, Songea
WANAMGAMBO 714 mkoani Ruvuma wamehitimu mafunzo ya awali ya miezi mitatu ya kijeshi katika masuala ya ulinzi wa nchi pamoja na usalama wa raia na mali zao kwa wilaya zote
mkoani hapa mwaka huu.
Akizungumza ofisini kwake jana, Kaimu Mshauri wa Mgambo Mkoa wa Ruvuma, Kapteni Nassoro alisema kuwa programu ya ulinzi mwaka huu ililenga kutoa mafunzo kwa vijiji vya mipakani ili kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo hayo.
Akibainisha alisema katika Wilaya ya Mbinga wameweza kuhitimu mafunzo hayo ya mgambo vijana 125, Wilaya ya Namtumbo vijana 397, wilaya ya Songea vijana 162 na Wilaya ya
Tunduru wameweza kuhitimu mafunzo hayo vijana 60, idadi ambayo alisema imekuwa ndogo ikilinganishwa na wilaya nyingine.
Alisema idadi ndogo ya wahitimu wa mafunzo hayo ya mgambo katika Wilaya ya Tunduru kila mwaka inatokana na wilaya hiyo kutawaliwa na mambo ya umwinyi na usultani kwa maeneo mengi ya vijijini na hata kusababisha vijana wenmgi kukwepa kujiunga na mafunzo hayo.
Alisema licha ya kumwezesha kumpatia ajira katika
kampuni za ulinzi pia kiapo chao kitawawezesha kutoa habari za siri, kwa vyombo husika ambazo zitasaidia kuwezesha kukamatwa kwa watuhumiwa, kuhojiwa, kuweza kuwabaini na kuwafikisha mahakamani.
Alisema serikali ya mkoa kwa kuona umuhimu wa mafunzo hayo ya mgambo ambayo yamekuwa yakiendeshwa kila mwaka,
tayari wameweza kuziagiza halmashauri zote kuhakikisha kila kijana anahudhuria mafunzo ya awali ya miezi mitatu kama njia moja wapo ya kuweza kumpatia elimu na utimamu wa mwili katika maisha yake.
Hata hivyo kapteni Nassoro alishindwa kubainisha katika kipindi cha miaka mitatu ya nyuma idadi ya vijana waliohudhuria mafunzo hayo ya awali na kuhitimu akisema hawezi kutoa takwimy hizo kwa kuwa ni za kiusalama zaidi.
No comments:
Post a Comment