24 November 2010

Mancini: Sina presha Manchester City.

LONDON, England

KOCHA Roberto Mancini, amesema kazi yake katika timu ya Manchester City, haina kashikashi ikilinganishwa na alivyokuwa Inter Milan.Muitaliano huyo ndiye anayetarajia kuleta
mafanikio makubwa ndani ya kikosi hicho cha Eastlands, ambacho kimekuwa ghali barani Ulaya lakini hali hiyo kwa Mancini inaonekana kuwa bado tangu awasili.

Mancini aliichukua timu hiyo, baada aliyekuwa akiifunza, Mark Hughes kutimuliwa mwishoni mwa mwaka jana.

Licha ya kuwepo na matarajio makubwa kutoka kwa mmiliki tajiri wa klabu hiyo na makelele kutoka kwa mashabiki, Mancini anaonekana kutosumbuliwa na presha hizo na badala yake anasisitiza kuwa alifanya kazi Inter kwa kipindi cha miaka minne, akaleta mafanikio kwa vinara hao wa Italia na kama anavyoweza kufanya Manchester City.

"Waandishi wa habari wanaendelea kusema kuwa nipo chini ya shinikizo, lakini sipo chini ya shinikizo," alisema Mancini.

"Endapo utakuwa umefanya miaka minne Inter Milan, huwezi kupata shinikizo kutokana na kuwa ni moja ya timu kubwa Italia na moja ya klabu kubwa ulimwenguni," alisema kocha huyo.

Alisema wakati anatinga katika klabu hiyo, ilikuwa haijatwaa ubingwa wowote kwa zaidi ya miaka 25 na alikuwa chini ya presha kila siku,  huku watu wakitaka kufahamu ni lini Inter itatwaa ubingwa.

Lakini akasema kuwa pamoja na presha hizo aliweza kubaki ndani ya klabu hiyo kwa muda wa miaka minne na kuweka rekodi akiwa kama Kocha Mkuu.

Mancini alisema anafahamu haiwezekani kufikia mafanikio kwa usiku mmoja hivyo, Manchester City inabidi wasubiri aijenge taratibu na kujenga msingi mzito utakaowafikisha kwenye mafanikio.

No comments:

Post a Comment