15 November 2010

'Makinda amechaguliwa kulisafisha bunge'

Na Charles Mwakipesile, Mbeya

KATIBU mkuu wa Kanisa la Moravian Tanzania, Jimbo la Kusini Magharibi, Mchungaji Daud Nsweve amesema kuwa spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Bi. Anne Makinda amechaguliwa na Mungu kwenda kufanya kazi maalumu kulisafisha bung  hilo.

Akizungumza na Majira katika mahojiano maalumu alisema kuwa   kutokana na Tanzania kupita katika kipindi cha mpito chenye changamoto kubwa wakati wa uchaguzi mkuu, sanjali na siasa za kupakana matope kwa ajili ya watu kusaka uongozi, palihitajika spika mwenye hofu ya Mungu asiyelaumiwa.

“Unajua nafasi ya spika ni sawa ya askofu na hivyo hata Biblia inasema imempasa Askofu asiye mtu mwenye kulaumika na hivyo baada ya Mungu kuona makundi ya wenye nguvu, aliona awawekee pembeni na kumpa nafasi mnyonge,” alisema.

Alisema kuwa kati ya walioomba kuteuliwa kiwa tiketi ya CCM   walikuwepo waombaji wenye nguvu kubwa ya ushawishi wa makundi waliyo nayo laini Mungu aliamua kuwaonesha kuwa yeye haangalii majina, bali anaaangalia mtu anayefaa kuongoza kwa wakati husika.

Mchungaji Nsweve alisema kuwa Bi. Makinda hakutegemewa kama angeibuka kuwa mshindi wa nafasi hiyo kutokana aliokuwa anapambana nao kuwa na nguvu kubwa ya ushawishi wa namna zote ikiwa ni pamoja na nguvu ya fedha, hata hivyo  yeye pamoja na unyonge wake aliwashinda kwenye vikao na kuibuka mshindi.

Alisema kuwa sifa kubwa aliyo nayo mama huyo ni uadilifu katika kazi zote alizowahi kupewa na serikali ikiwa ni pamoja na ukuu wa wilaya, ukuu wa mkoa, uwaziri na nyazifa nyingine ambazo  zimemjengea heshima kubwa ndani na nje ya nchi.

"Huyu mama mimi ninamlinganisha na Magreth Thacher wa Uingereza  ambaye aliongoza wanaume kwa mafanikio na ujasiri mkubwa, hali ambayo alisema ndiyo itakayotokea kwa Bi. Makinda ambaye ni shupavu, asiyekubali kuyumbishwa, msimamo mkali wa kuchukia ufisadi.

9 comments:

  1. Kauli za aina hii hazistahili kutolewa na viongozi wa dini; hazina uvuvio wa Roho Mtakatifu. Mungu hachagulii watu viongozi wa kisiasa kama ilivyokuwa tangu mwanzo, hujichagulia weneyewe. Kwenye Biblia ameandikwa; mpe Kaisari iliyo ya Kaisari na Mungu iliyo ya Mungu. Kazi ya siasa ni ya utashi na utqawala wa wanadamu tofauti na kazi ya injili ambayo maongozi yake yanatokana na Roho wa Mungu. Huyu amekosa ufunuo,asiendelee kutuchanganya na viongozi wa siasa ambao WENGI wamepata kwa njia za uganga. au tumwuulize, mbunge wa Korogwe, Maji Marefu aliye mganga wa jadi ni chaguo la Mungu au la wanaKorogwe? Askofu!!! Ukristo ni tofauti na haya unayosema, Mungu akurehemu kwa upofu huu.

    ReplyDelete
  2. THATCHER MWENYEWE ALIONDOLEWA KABLA HAJAMALIZA MUHULA. MAKINDA ALIWAHI KUPOTEZA UMAARUFU PIA LEO UNATOKA WAPI WEE BISHOP KUMSEMEA HAYA! MUNGU HAJKUPA HUO UJUMBE, USITUFUMBE KAMA JK NA KUNDI LAKE WANAVYOWAFUMBA MASKINI WA TZ ILI KUJIPATI UONGOZI. TUNAKUKEMEA KWA JINA LIPITALO MAJINA YOTE KWA UPOFU HUU; WOTE TUNAJUA VIONGOZI WETU HUJIPAITIA USHINDI KWA WAGANGA YAANI WACHAWI UNAMTAJAJE MUNGU KWENYE CHAGUZI KAMA HIZI?? JK ANALINDWA NA MAJIN, MAKAMBA NI KM MWEHU, CHILIGATI MUNGU TU AMHURUMIE HAJIJUI NI ANATUMIKA KM MSUKULE. ASKOFU TUBU, TUBU, NA TUBU.

    ReplyDelete
  3. Mchungaji Nsweve wacha kujifanya wewe ni msemaji wa Mungu, hayo ni mawazo na maneno ya kujipendekeza. Ebu tuambie, hapo mtu unayempigia debe kwa kumsingizia Mungu, atakapo shindwa kukidhi haja utasemaje? Waulize wenzako waliowahi kusema watu fulani walikuwa machaguo ya Mungu mwisho wake wakaduwaa.

    ReplyDelete
  4. Ndugu mhariri hapa watu wataongea mengi lakini mpira unachezwa dakika 90. Itakapofika dakika ya 30 tu tutajua kuwa anafaa au hafai. Kama ni uspika ameshapewa na CHAMA TAWALA. Kwa hiyo hapa tutaumiza vichwa. Yeye ndio mwenye kisu chenye makali ataamua atumie kisu kwa umakini au AKICHEZEE na akikichezea kitamkata yeye mwenye. Anatakiwa kuwa makini katika jukumu hilo zito alilopewa asifikirie kuwa ni kazi ndogo. Afanye kazi na kujituma ili kuliendeleza bunge katika misingi ya haki sawa. Akisikiliza mafisadi ajue kuwa atakuwa anatwanga maji kwenye kinu.

    ReplyDelete
  5. Watz kwa kelele hamjambo. Mchungaji uko juu na kwa kweli tunahitaji viomngozi wa dini walio wazi kiasi hiki. Wanaopinga ni walewale wasiojua na wanaotaka wanavyotaka wao ndio, viwe, haiwezekani. na nyie mkagombee tuone kama mtashinda muwe spika. Wivu tu ,tangu Makinda amekuwa kiongozi mbona hamjakosoa alishindwa wapi ,kwenye uspika tu ndo mnachonga kwa sababu mzee aliyejenga ofisi ya spika jimbnoni kweake hajapata? na niulilze ile ofisi itakuwaje? au makinda atahamia urambo?

    ReplyDelete
  6. Moja na moja ni mbili, sema usiseme. Hatujasikia tuhuma za kujenga ofisi jimboni kuwa tatizo kuliko ufisadi uliopo tz, wee usiongee km mtoto. Tatizo la huyu askofu ni kuzungumza lisilotoka kwa Mungu. Tunarudia, viongozi wengi wameenda kwa wachawi kaupata vyeo, Mungu anahusika? Dini si kivuli; kama uanpenda kusikia ukweli, usijifiche kwenye hili, Makinda kawekwa na mafisadi hana ch kujitahidi, uwezo na msimamo wake vinaeleweka waTZ tuumie tu. Hivi wewe hufikirii? Mhagama aliomba unaibu wakaongeza muda, hiyo si dhuluma? Na sera ya spika mwanmke ilianzaje usiku mmoja? Hakuna nchi inayoongozwa hivyo ni TZ tu.

    ReplyDelete
  7. Nyie WATZ, mwasema Mungu! Acheni huyo Mungu asipate hasira akawamaliza. Mpaka sasa hamjaandamana kwa sbb ni makondoo, nchi imetekwa si siri. utajiri wote umewekwa kwa manyang'au waliowadhamini wa viongozi, eti ni mungu kawapa madaraka! Wachache wanoonekana kukerwa na dhuluma kwa raia anatupwa nje; ccm ni mafia, mbinu zao zote ni za kiuhaini. OLE WAKO JK HUTAKWEPA HASIRA YA HAKI KWA DHULUMA UNAZOENDELEZA

    ReplyDelete
  8. Mchungaji declare interest kwanza halafu uyaweke mawazo yako. Usipende kulitumia jina la MUNGU kwa ajili ya maslai yenu.
    Lakini hizi ni nyakati za mwisho msishangae watu kuwa vibaraka wa wanasiasa. Siasa inawanunua wengi mno

    ReplyDelete
  9. Hawa viongozi wa dini siku hizi wamechanganyikiwa kabisa. Lakini kinachowapa nguvu ni umbumbumbu wa waumini wao.

    ReplyDelete