23 November 2010

Klabu Bingwa Ulaya kuendelea leo.

LONDON, England

MICHUANO ya Klabu Bingwa Ulaya, inaendelea leo katika viwanja mbalimbali kwa kuikutanisha miamba 12 kati ya 28, inayoshiriki michuano hiyo.Katika mechi za leo kila
timu itashuka uwanjani, ikiwa katika mazingira tofauti kutokana na kuwa kuna baadhi ya timu ambazo tayari zimeshakata tiketi ya kucheza hatua ya mtoano, huku nyingine zikipigania roho ili kubaki katika ligi hiyo kubwa barani Ulaya.

Kwa mujibu wa ratiba ya michuano hiyo, mechi ya kwanza itaikutanisha timu ya Spartak Moscow ya Russia ambayo itakuwa ikiikaribisha  Marseille mjini Moscow, huku Ajax ya Uholanzi ikaakaribisha Real Madrid ya Hispania.

Mbali na mechi hizo, nyingine itakuwa ni kati ya Auxerre na AC Milan, huku Basle ikipepetana na  CFR Cluj-Napoca wakati Braga wao wataikaribisha Arsenal na     Chelsea, ambayo tayari imeshajihakikishia kucheza hatua ya mtoano itaikaribisha MSK Zilina.

Hata hivyo macho na masikio ya mashabiki yanadaiwa yataelekezwa katika mchezo utakaozikutanisha timu za Auxerre na AC Milan na mechi kati ya Ajax ya Uholanzi, itakayokuwa ikiikakaribisha Real Madrid

Inaelezwa kuwa utamu wa mechi hizo ni kutokana na baadhi ya timu kuwa katika mazingira magumu, ambapo kama AC Milan ili iweze kusonga mbele ni lazima iondoke na ushindi na si vinginevyo, lakini kama itapoteza mchezo huo dhidi ya Auxerre inaimaisha itakuwa imeyaaga mashindano hayo.

Msimu huu Auxerre imeshafanikiwa kupata ushindi wa mechi mbili, ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani kati ya mechi tatu ilizocheza kwenye uwanja huo, ikiwemo iliyoifunga  Zenit katika mechi ya mrudiano na ushindi iliyoibuka nao dhidi ya  Ajax.

Ligi hiyo inatarajia kuendelea kesho kwa kuzikutanisha timu za     Rubin Kazan na FC Copenhagen, Hapoel Tel-Aviv itacheza na Benfica, Inter Milan na FC Twente, Panathinaikos nayo itaumana na Barcelona, Rangers wao watacheza na Man Utd, Schalke 04 itakumbana na Lyon, Tottenham itapepetana na Werder Bremen na Valencia itambana na Bursaspor.

No comments:

Post a Comment