22 November 2010

Jiji la Mbeya kugawiwa vyandarua.

Na Esther Macha, Mbeya

KATA 36 za Jiji la Mbeya zimepatiwa vyandarua kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa malaria ambavyo vitagawiwa kwa kila kaya.Akizungumza na mwandishi wa habari Kaimu Mratibu wa
Malaria wa Jiji la Mbeya, Bw. Vincent Mwanga alisema tayari vyandarua hivyo vimepatikana kilichobakia ni kuvisambaza kwa wananchi.

Aliongeza kuwa wananchi wanapaswa kuvitumia vizuri vyandarua hivyo ili lengo la serikali litimie kwa kuwa hiyo ni njia moja wapo ya kutokomeza ugonjwa wa malaria nchini.

Alisema kuwabaadhi ya watu ambao wakipata vyandarua vya misaada huvitumia katika matumizi mengine kama vile kuvulia samaki na kuweka katika uzio wa bustani ili kuku wasiingie kwenye bustani hizo.

“Ningependa kuwajulisha wananchi kuwa baada ya kutoa vyandarua hivyo kutakuwepo na utaratibu wa kufuatilia kwa umakini suala hilo ili kubaini wale watakaovitumia katika mambo mengine,” alisema.

“Hii tabia ya wananchi kufanya mambo yao tofauti na matarajio ya serikali ni jambo baya sana kwa kuwa serikali imekuwa ikijitahidi kushirikiana na
mashirika mbalimbali ili kutokomeza malaria.

No comments:

Post a Comment