16 November 2010

CCM, CUF wapata majimbo matatu, CHADEMA moja.

Na Waandishi Wetu

MATOKEO ya uchaguzi katika majimbo saba ambayo uchaguzi uliahirishwa yametangazwa na vyama vya CCM na CUF kuibuka ma matatu kila moja na moja kubaki mikononi mwa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Katika Jimbo la Nkenge wilayani Missenyi, mkoani Kagera Bi. Asumpta Mshama wa CCM amechaguliwa kwa 23,772 dhidi ya mpinzani wake wa karibu wa CUF, Alhaji Amri Sadik aliyepata kura 606 na Bw. William Kweyamba wa TLP kuibuka na kura 597.

Jumla ya kura zilizopigwa ni 25, 091, zilizoharibika ni 116 na kura halali zilikuwa 24,975. Waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 90,631.

Kutoka wilayani Mpanda mkoani Rukwa, Bw. Said Amour Arfi, aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Mpanda Kati kupitia CHADEMA amefanikiwa kutetea kiti chake katika Jimbo jipya la Mpanda Mjini baada ya kuwazidi wapinzani wake wawili kwa kura 49.

Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Mpanda Mjini, Bw Henry Haule alimtangaza Arfi kuwa mshindi baada ya kupa kura 8,075 huku Sebastian Kapufi wa CCM akipata kura 8,020 na nafasi ya tatu ikienda kwa Aram Ndimubenya wa CUF aliyeambulia kura 39.

Waliojiandikisha kkupiga kura kuwa ni watu 42,215 lakini waliojitokeza ni 16,276. Kura halali zilikuwa 16,140 na zilizoharibika ni 135.

Naye Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mpanda Vijijini, Mhandisi Emmanuel Kalobelo alimtangaza Bw. Moshi Kakoso wa CCM kuwa mshindi kwa kupata kura 5,693 akifuatiwa na Bw. Masanja Mussa wa CHADEMA aliyepata kura 3,260 huku nafasi ya tatu ikienda kwa Bw. Shaban Kisabo wa CUF aliyepata kura 74 na Makofila wa NCCR-MAGEUZI aliambulia kura 22.

Watu waliojiandikisha katika jim,bo hilo ni 35,928 lakini waliojitokeza kupiga kura ni 9,138. Kura halali zilikiua 9,049 na zilizoharibika 89.

Kabla ya matokeo hayo kutangaza wafuasi wa vyama vya CHADEMA na CCM walionekana mitaani wakishangilia ushindi huo, na baada ya matokeo hayo kutangazwa walitawanyika wenyewe, licha ya vyombo vya doka kujipanga kudhibiti fujo ambazo zingetokea.

Katika majimbo ya Zanzibar, CUF imeshinda majimbo ya Wete, Pemba, Magogoni na Mtoni yote ya Unguja, huku CCM ikiambulia jimbo moja la Mwanakwerekwe lililoko Unguja.

Katika Jimbo la Magogoni walioandikishwa walikuwa 10, 155, waliopiga kura ni 7,484. Hamadi Ali Hamad 4,033 na Issa Abeid 3,264. Jimbo la Mtoni waliojiandikishwa ni 9,671, waliopiga kura 7,395 kura halali 7, 301, na Faki Haji Makame (CUF) aliibuka msindi kwa kura 4,097 wakati mgombea wa CCM Ussi Ame alipata kura 2, 738.

Katika jimbo la Mwanakwerekwe walioandikishwa ni 8,061, halali 5,083, 71 ziliharibika. Mgombea wa CCM, Haji Juma Sereweji alishinda kwa kura 2,975 na Usi Juma Hassan wa CUF 1,971.

Kwa matokeo hayo CUF imefikisha ya majimbo 22 ya Zanzibar, ukiongeza mawili ya Tanzania bara yanafika 24.

Imeandaaliwa na Juddy Ngonyani, Mpanda; Livinus Feruzi
Missenyi, na Mwajuma Juma, Zanzibar

1 comment:

  1. Petro Eusebius MselewaNovember 16, 2010 at 10:06 AM

    Hongereni wote mliochaguliwa.Wahini kwenye kiapo Dodoma ili muwatumikie wananchi.Hta kama mmechelewa kumchagua Spika,Naibu Spika na hata kumuidhinisha Waziri Mkuu,songeni mbele kiutendaji.Hayo ni matunda ya Tume ya Uchaguzi Mbovu.Mungu awatangulie....

    ReplyDelete