14 November 2013

FUTURE TAIFA STARS YAWAADHIRI KAKA ZAO 1-0


  Timu ya Future Taifa Stars jana imewaadhiri Taifa Stars katika mechi ya kirafiki iliyochezwa Uwanja wa Karume Dar es Salaam, anaripoti Fatuma Rashid .

  Mechi hiyo ni maalumu kwa Kocha Mkuu wa Stars, Kim Poulsen kwa ajili ya kuchagua wachezaji wengine 10 watakaoungana na timu hiyo ambayo itakwenda jijini Arusha kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Kenya 'Harambee Stars', ambayo ipo kwenye kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (F IFA).
  Katika mchezo huo Future ndiyo walioanza kupata bao dakika ya 40 kupitia kwa mchezaji wao Elias Mguli baada ya kutumia udhaifu wa beki wa Stars,Kelvin Yondan.
  Katika mechi hiyo Future walionekana kuutawala mchezo zaidi na kukosa nafasi nyingi za kufunga , ambapo dakika ya 26, Ramadhani Singano 'Messi'aliachia shuti kali lililotoka nje ya lango.
 Taifa Stars ilionekana kupotea na kutokana na kasi ya vijana wa Future kufanya mashambulizi mfululizo huku kiungo wake, Salum Abubakari akipoteza mipira mingi na kuwafanya Future kuendelea kutawala mchezo huo.
  Dakika ya 31 Taifa Stars ilizinduka na kufanya shambulizi kali langoni mwa Future lakini shuti la beki wake Erasto Nyoni liliokolewa na mabeki wa Future Taifa Stars. 
  Kipindi cha pili timu zote ziliingia uwanjani zikiwa na uchu wa kutak a kufunga mabao lakini mabeki wa pande zote walikaa imara ya kuon doa hatari zote zilizoelekezwa langoni.No comments:

Post a Comment