03 October 2013

MBINU KUONDOA UMASKINI NCHINI ZAANDALIWA CHINANa Mwandishi Wetu, Aliyekuwa Beijing, China
Wawakilishi mbalimbali wa asasi zisizo za kiserikali kutoka nchi za Afrika ikiwemo Tanzania, wamependekeza mbinu mpya za kuhakikisha umaskini unapungua Afrika hususan Tanzania kama si kuondoka kabisa ili kuharakisha maendeleo ya bara hilo.

Aidha, wamependekeza kutenga fungu maalumu la fedha kwa ajili ya kukuza biashara za ubia baina ya watu wa China na Afrika ili kuinua watu wenye kipato cha chini na maskini. Mapendekezo mengine ni pamoja na kuwa na utaratibu wa kubadilishana watu hususani wataalamu mbalimbali ili kukuza mahusiano ikiwemo tamaduni za nchi hizo. 
Wawakilishi hao kutoka nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Tanzania, walitoa mapendekezo hayo hivi karibuni katika kongamano la siku moja lililoandaliwa na Taasisi Inayosimamia Shughuli Zote za Taasisi Zisizo za Kiserikali nchini China (CNIE), katika Chuo Kikuu cha Masomo ya Kimataifa cha Beijing (BFSU) mjini Beiging, China.
  Kongamano hilo la wanazuoni lilihudhuriwa na wawakilishi wa vyombo vya habari kutoka nchi za Afrika na Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ili kujadiliana namna ya kufikia maendeleo ya pamoja na kuondokana na umaskini katika ushirikiano baina ya nchi za Afrika na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China.
  Mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania waliosoma nchini China, Fred Maiga aliishauri Serikali ya China kuweka mkakati utakaohakikisha watu wa Afrika na Wachina wanashirikiana ili kufikia maendeleo. "Maendeleo ya mahusiano yalenge watu zaidi. Maendeleo katika mahusiano ya China na Afrika yamewaleta watu wa mataifa hayo karibu. Mahusiano hayo yanapaswa kuangalia zaidi uhusiano wa kibiashara na uelewa wa tamaduni za nchi hizo," alisisitiza Maiga katika hotuba yake.
  Mbali na hayo walipendekeza kubadilishana wataalamu pamoja na kutumia Umoja wa Watanzania waliosoma nchini China katika kukuza na kutangaza umuhimu wa uhusiano baina ya China na Tanzania ili kulenga kukuza ushirikiano.
"Wachina ni wachapakazi sana ili kufikia ndoto yao ya 'Chinese Dream' (Ndoto ya Wachina). Wachina wanaweza kushirikiana na Waafrika katika kukamilisha ndoto ya Afrika ya umoja kwa kuungana, kushirikiana na kusaidiana ili kukamilisha ndoto hizo," aliongeza Maiga.
  Ndoto ya China ni dira iliyozinduliwa na Rais wa China, Xi Jinping ambaye alitembelea Tanzania ikiwa ni nchi ya kwanza Afrika na ya pili duniani wiki chache baada ya kuteuliwa kuwa rais wa taifa hilo mwezi Machi, mwaka hu

No comments:

Post a Comment