11 September 2013

BALAA JINGINE



  •  MWALIMU ALIYEMBAKA MWANAFUNZI 'MTEGONI'
  • MAHAKAMA YAMPELEKA GEREZANI MIAKA 30


 Na Nickson Mahundi, Ludewa

MAHAKAMA ya Wilaya ya Ludewa, mkoani Njombe, imemhukumu kifungo cha miaka 30 gerezani na kuchapwa viboko 30 mwalimu wa Shuile ya Msingi Ingwachanya.


Mwalimu huyo, Bw. Romanus Msango, mkazi wa Lupembe, wilayani Njombe, alitiwa hatiani kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa miaka 14 (jina linahifadhiwa) na kumuumiza vibaya sehemu za siri.

Akisoma hukumu hiyo Septemba 6 mwaka huu, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ludewa, Bw.

Fredrick Lukuna, alisema mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka ambao haukuwa na shaka yoyote.

Alisema mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 1309(1) na 31(1) cha kanuni ya adhabu ya mwaka 2002 hivyo adhabu hiyo ni fundisho kwa wengine.

"Natoa adhabu hii ili kukomesha vitendo hivi kwenye jamii

kwani vinaleta madhara makubwa kwa watoto na wanawake pamoja na kusababisha magonjwa ya kuambukiza," alisema.

Awali ilidaiwa na Mwendesha Mashtaka, Edison Kasekwa kuwa, mshtakiwa alitenda ukatili huo wa kinyama Agosti 20,2012 katika Kijiji cha Masimbwe, Kata ya Mlangali.

Alisema kabla mshtakiwa hajatenda kosa hilo, alimshambulia mwanafunzi huyo, kumbaka na kumlawiti jambo ambalo lilimsababishia maumivu makali.

"Serikali ilimpa mshtakiwa dhamana kubwa ya kulea watoto ambao ni nguvukazi ya Taifa la kesho lakini amewageuka na kutenda kitendo ambacho ni kinyume na maadili ya kazi yake, kuidharirisha taaluma hivyo naomba mahakama itoe adhabu kali iwe fundisho kwa walimu wengine," alisema.

Bw. Kasekwa aliongeza kuwa, mshtakiwa alikusudia kutenda makosa hayo kwa sababu alimfuata mwanafunzi huyo shambani wakati akivuna mahindi na wenzake ambao walikimbia kwenda kijijini kutoa taarifa baada ya mshtakiwa kumkamata mwenzao na kumpeleka kichakani.

Wa k a t i h u o h u o , wa t u wawili Bahati Mtega na Flowin Mtweve, wote wakazi wa Milo, wamehukumiwa kifungo cha maisha gerezani na kuchapwa viboko 12 kila mmoja kwa kosa la kumbaka mke wa mtu na kumsababishia maumivu makali

3 comments:

  1. Mwalimu kupewa dhamana ya kulea watoto kielimu na kisha kuwageuka ni kwaida kwa TZ KTK fani zingine.

    Mara ngapi tumeona manesi wakinyanyasa wagonjwa? Mara ngapi viongozi wakipewa dhamana ya kulindamali ya umma wanaifisadi?

    Ni mara ngapi viomgozi wa dini tena hao ndo kabisa.Mie nimeshuhudia sista mmoja kijijini kwetu akimsingizia mama yake kuwa ni mchawi, na kumpa pesa za kutosha mdogo wake ili amnyanyase mama yao kwa kusudio la kuharakisha kifo chake kwa manyanyaso.

    Kwa hiyo bunge letu liache mapigano , badal yake liangalie upya sheria za kulinda wananchi wake kikatiba

    ReplyDelete
  2. watu wa mwogope Mungu,watoto wetu tuwafiche wapi? Watanzani? hata wazee ,viongozi wa serikali,dini wafanya biashara ngono imekuwa ni km pombe kwao,watoto wa kike hawajiamini ,hata ktk kazi kwa mapokeo mabaya wanayo ya ona kwa walimu,lecture,profesor ,huwezi kuona mwanamke anasumbuliwa Amerika km nyumbani watu wote wako chini ya sheria,nchi yenye kila kitu lakini hata utamaduni wetu tunashidwa kuuenzi Mungu tusaidie.

    ReplyDelete
  3. vitendo vya ubakaji nchi hii vinatisha sana hii ni kutokana na kukosa maadili. je mtoto wake wa kumzaa angelifanyiwa hivi angejisikaje? watu wenye tabia kama hii wanastahili kufungwa maisha kwani ameharibu maisha ya huyo mtoto na hicho kitendo kitamuathiri huyo mtoto katika maisha yake yote.

    ReplyDelete