22 August 2013

WANANCHI WACHOMA MOTO BASI



 Na Damiano Mkumbo, Singida
.KUNDI la watu wanaodaiwa kuwa wenye hasira wamechoma moto basi la Kampuni ya Turu la mjini Singida katika tukio lililotokea katika Kijiji cha Singa Wilaya ya Mkalama Mkoa wa Singida.Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela, tukio hilo lilitokea juzi Agosti 20, mwaka huu mchana wakati basi hilo likitoka mjini Singida kwenda Hydom kijijini.

Basi hilo lilipofika kijijini hapo lilisimamishwa na abiria kutakiwa kushuka pamoja na kuteremka na mizigo yao.Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini hapa jana, Kamwela alibaini kuwa basi hilo nambari T438AHJ lilikuwa likiendeshwa na dereva, Yusufu Lema (36) na kwamba baada ya kufika kijijini hapo wananchi walilizuia na kuanza kulipiga mawe.
Alisema basi hilo lilipasuliwa vioo kwa mawe na kisha kuchomwa moto na kusababisha hasara inayokadiriwa kufikia sh. milioni 40.Kamanda Kamwela alisema kuwa uchunguzi ulibaini chanzo cha tukio hilo, mgogoro kati ya wananchi wa Vijiji vya Singa, Mudida na Nkungi vilivyo kwenye barabara hiyo kutokana na mtu mmoja, Daudi Songelael (40) kukanyagwa na gari na kusababisha kifo chake.
Inadaiwa kuwa basi la Kampuni hiyo T922ALQ lilisababisha kifo cha marehemu Agosti 6, mwaka huu. Alisema kulikuwa na mvutano kiasi cha kusababisha kuchomwa moto basi hilo.Alisema Jeshi la Polisi liliwashauri wamiliki wa Mabasi ya Kampuni ya Turu kusitisha safari zake kwa muda ili kutafuta suluhisho la mgogoro huo.
Aliongeza kuwa wamiliki hao walikwenda kijijini hapo Agosti mwezi huu kuomba msamaha bila kulijulisha Jeshi hilo; na kuanzisha tena safari zake Agosti 20, mwaka huu wakidhani mgogoro umekwisha.Alisema basi hilo lilipofika kijiji cha Singa lilikutana na kizuizi na wananchi wakalichoma moto kisha kukimbia

No comments:

Post a Comment