20 August 2013

UZALISHAJI MAJI WAPUNGUA DAWASCO



Na Aneth Kagenda
SHIRIKA la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO), limesema uzalishaji maji katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani umepungua kutoka lita 80,000,000 hadi lita 50,000,000 kwa siku.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na DAWASCO makao makuu na ofisa uhusiani Bi. Irene Makene imesema kuwa, hali hiyo imetokana na pampu mbili za kuchotea maji (pre-lift pump) kwenye Mto Ruvu kuharibika na hivyo kubaki kwa Pampu mbili zinazofanya kazi kati ya nne
"Kutokana na tatizo hilo DAWASCO inawaomba radhi wananchi wa Dar es Salaam, Kibaha na Mlanzidi na Pwani kutokana na kukosa maji katika baadhi ya maeneo hadi hapo huduma zitakaporejea kama kawaaida," alisema.Bi.Makene alisema kuwa kutokana na hali hiyo imesababisha uzalishaji kupungua na kuathiri upatikanaji wa maji katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.Alisema kutokana na hitilafu hiyo mafundi wanaendelea na jitihada za matengenezo ili kuhakikisha upatikanaji wa maji unarejea katika hali yake ya awali kama kawaida. Alisema maeneo yatakayoathirika ni Mlandizi, Kibaha, Kibamba, Mbezi, Kimara, Ubungo, Chuo Kikuu, Kibangu, Riverside, Barabara ya Mandelea, Tabata na Segerea.

No comments:

Post a Comment