26 August 2013

UDA KUINGIZA MABASI MAPYA 2000



Na Reuben Kagaruki
SHIRIKA la Usafirishaji Mkoa wa Dar es Salaam (UDA) linatarajia kuingiza mabasi 2,000 kwa ajili ya kutoa huduma za usafiri jijini ifikapo Juni mwaka 2014.Haya yalisemwa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Saimon Group, Robert Kisena, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mageuzi makubwa ambayo yanaendelea kufanyika ndani ya UDA kuhusiana na uwekezaji.

Alisema hadi sasa wameingia ubia na kampuni ya kutengeneza mabasi ya Eicher pamoja na wasambazaji wa mabasi ya kampuni hiyo ya Africarries kwa ajili ya kufanikisha uwekezaji huo.
"Tumeanza mpango mkubwa wa uwekezaji na tumeingia ubia na Eicher na Africarries ambapo ifikapo Juni, 2014 mabasi 2,000 yatakuwa yamefika nchini na ifikapo Septemba na Oktoba mabasi mengine 100 itakuwa yamefika na hayo ni mbali na yale 2,000," alisema Kisena.
Alisema katika awamu ya kwanza walianza na mabasi 30 na sasa mabasi mengine 40 yapo tayari na yataanza kutoa huduma hivyo kufanya jumla ya mabasi ya UDA kufikia 70. Aliongeza kuwa ifikapo mwaka 2017 UDA itakuwa na mabasi yanayotoa huduma ya usafiri yapatayo 7,000 na mipango ya kufanikisha uwekezaji huo inaenda vizuri.
"Uwekezaji huu utakuwa na manufaa kwa wakazi wa Dar es Salaam...uwekezaji wa UDA nia yake ni kugusa maisha ya wananchi, tutaleta mabasi ambayo yatasaidia wananchi wa rika zote, wanawake na wanafunzi," alisema Kisena na kuongeza kuwa;
"Hii sio mipango wa ubabaishaji v i n g i n e v y o h a t a h a w a wasingekuwepo (maofisa wa Africarriers." Alisema uwekezaji huo wa mabasi 2,000 utakapoanza zitazalishwa ajira za watu 8,000, hivyo watu wengi wataweza kupata kazi," alisema na kuongeza kuwa;"Nauli za mabasi yetu zitakuwa hazipandi hovyo hovyo, kwani sisi tupo kwa ajili ya wananchi na hata kama kutakuwa na hali ya kupanda kwa mafuta, nauli haitakuba inabadilika mara kwa mara.
Alifafanua kuwa ununuzi wa mabasi 2,000 ni maandalizi ya kuingia na kutoa huduma kupitia Mradi wa Mabasi yaendayo Kasi Dar es Salaam (DART), kwani mabasi yanayoagizwa na UDA ni yale yanayokidhi masharti yanayotakiwa ikiwa ni pamoja na kuwa na milango miwili ya kutumiwa na abiria.
Aliongeza kuwa sehemu kubwa ya faida itaelekezwa kwa jamii hasa kwa upande wa elimu na sekta ya afya. Alibainisha kwamba baada ya UDA kuwa imara hisa zake zitaingizwa kwenye Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE ) ili watu wapate fursa ya kununua hisa hizo baada ya kutengeneza minzania yake mwakani.
Wakati huo huo, Kisena alisema wao wapo tayari kununua hisa ndani ya UDA iwapo itafanyika hivyo. "Na sisi tumesikia kwenye vyombo vya habari kuwa Jiji la Dar es Salaam litauza hisa zake, endapo watafanya hivyo sisi tutakuwa tayari kuzinunua, lakini hatukatazi mtu mwingine kujitokeza kuzinunua,"alisisitiza
 

2 comments:

  1. KWA HILO NAWAPONGEZA SANA.BIGUP.

    ReplyDelete
  2. Ni jambo jema lakini ni vema pia kuwa makini katika kusimamia mabasi hayo ili yatoe huduma bora zaidi.

    ReplyDelete