20 August 2013

SHERIA ZA MAZINGIRA KUPITIWA UPYA



SERIKALI imesema kuwa ni wakati mwafaka wa kuangalia sheria zilizopo zinazohusu uchafuzi wa mazingira kutokana na hali halisi kuonesha kuwa asilimia 90 ya uchafu unaoenda baharini unasababishwa na wananchi, anaripoti Anneth Kagenda.

Hayo yalisema Dar es Salaam jana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, John Mngodo wakati akifungua mkutano wa wadau ulioandaliwa na Mamlaka ya Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA), ambao unalenga kujadili mambo mbalimbali likiwemo hilo la jinsi ya kuzuia uchafuzi wa mazingira ya baharini kutokana na vyombo vya baharini na ziwani.
Pia kujadili juu ya sheria na kanuni za uchafuzi wa mazingira baharini.
Alisema, suala la uchafuzi huo kwa asilimia 90 limekuwa likisababishwa na wananchi hivyo sheria zilizopo zikitumika na zingine kuibuliwa suala hilo linaweza kupatiwa ufumbuzi.
“Asilimia 10 ndiyo inayotokana na vyombo vyenyewe vya majini, mfano meli kuzama na mafuta kumwagika bahari inachafuka, lakini uchafuzi mkubwa unatokana na shughuli za kibinadamu ikiwemo kutiririsha maji machafu,”alisema.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA, Ahmed Kilima, alisema lengo la semina hiyo ni kujadili mambo mbalimbali likiwemo watu kufahamu juu ya suala hilo na watu kujua sheria ambazo tayari zipo wazifahamu na kuzifanyia kazi pamoja na kupata utaalamu

No comments:

Post a Comment