26 August 2013

MASHABIKI WA LIVERPOOL WANYAKUA UBINGWA



Na Mwandishi Wetu, Singida

TIMU ya soka ya mashabiki wa Li v e r p o o l n c h i n i Uingereza wa mjini Singida, juzi imenyakua ubingwa wa bonanza la Serengeti Fiesta mkoani hapa, baada ya kuichapa Bayern Munich ya Majengo mabao 2-0.Kwa ushindi huo, Liverpool imejinyakulia kombe na sh. 300,000 taslimu. Mshindi wa pili Bayern Munich, wao walizawadiwa sh. 200,000.


Mashabiki wa Liverpool wamewavua ubingwa huo wenzao wa Arsenal wa mjini Kigoma, ambapo Arsenal walinyakua ubingwa huo kwa kuichapa Manchester United.Mchezo huo mkali na wa kusisimua, ulifanyika kwenye Uwanja wa Klabu ya Peoples uliopo Utemini mjini Singida na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa mji huo na vitongoji vyake.

Mabao ya Liverpool yalifungwa na Mohammad Said na Saidi Saidi katika dakika za 58 na 71.Bayern Munich itabidi wajilaumu wenyewe kwa kukosa nafasi nyingi za kufunga kwani walikosa mabao ya wazi dakika za 61, 69 na 81 kutokana na safu yake ya ushambuliaji kutokuwa makini walipokuwa wakilikaribia lango la wapinzani wao Liverpool.

Ak i z u n g umz a b a a d a y a kumalizika mchezo huo, Meneja Biashara wa Kampuni ya bia ya Serengeti Kanda ya Ziwa, Octavian Migire alisema wameamua kudhamini bonanza la Serengeti Fiesta Soccer Bonanza kwani ni shamrashamra za awali, kabla ya tamasha kubwa la Serengeti Fiesta mjini Singida kwa kuwa mchezo wa soka unajumuisha watu mbalimbali ambao ni wateja wao.

Alisema kupitia michezo, vipaji huibuka, kwani ni fursa kwao kuonekana na wadau wa soka ili wahusika waweze kujiajiri na kuajiriwa."Kama unavyojua, ajira kupitia michezo nafasi ni nyingi na hazina masharti magumu kama zilivyo kwa kazi zingine. "Pia zinalipa mapato makubwa kuliko kazi zingine zozote hapa duniani," alisema Migire


No comments:

Post a Comment