23 August 2013

LAAC YAZIDI KUBAINI WIZI WA FEDHA



Na Mariam Mziwanda
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), imesema aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro, Bi. Sarah Linuma na Mweka Hazina wake, Bw. Stima Kabikike, wanapaswa kutafutwa ili waweze kujibu tuhuma ya hesabu hewa sh. bilioni 1.2 za halmashauri hiyo.

Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Bw. Selemani Zedi, aliyasema hayo Dar es Salaam jana katika kikao chao na kusisitiza kuwa, pamoja na Bi. Linuma kuomba kustaafu na Bw. Kabikike kuhamishiwa Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam, ukweli utabainika juu ya matumizi hewa ya fedha hizo za umma.Alisema ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imebaini matumizi ya fedha hizo hayajathibitishwa na haijulikani zimefanyia kitu gani.
“Tunafanya taratibu za kumsaka Bi. Linuma ambaye ameomba kustaafu na Bw. Kabikike waje kutuambia kwanini matumizi ya sh. bilioni 1.2 hazina nyaraka kwa CAG na haijulikani zipo wapi.“Pia kamati hii imebaini katika halmashauri hiyo, kuna ujenzi wa ofisi hewa ya Mkurugenzi kutokana na CAG kutokuwa na taarifa ya malipo sh. milioni 39 alizolipwa mkandarasi ambazo ni zaidi ya fedha zilizoainishwa katika mkataba,” alisema.
Aliongeza kuwa, kumekuwa na ubadhirifu katika ulipaji malipo ya Hifadhi ya Jamii kwa wafanyakazi hivyo kuitaka halmashauri hiyo kuhakikisha fedha zote zinapelekwa ili wafanyakazi hao wanapofikia umri wa kustaafu waweze kupata viinua mgongo vyao.Kamati hiyo iliiagiza halmashauri hiyo kupeleka zaidi ya sh. milioni 94 za miradi ya vijijini ambazo hazikufikishwa na uhakiki ufanyike ili fedha halali zijulikane na kupelekwa kabla mwaka huu wa fedha haujamalizika.
Akizunguzia matumizi hewa ya fedha za miradi ya wanawake na watoto katika halmashauri hiyo, Bw. Zedi alisema ni kinyume na sheria kutumia fedha hizo katika matumizi mengine.
Matumizi hayo ni pamoja na kulipana posho na kuitaka h a l m a s h a u r i k u h a k i k i s h a watakapokutana tena na kamati hiyo wawe na ripoti inayoonesha uwezo wa kujitegemea kwa asilimia 10 na kuamuru malipo yote sasa kufanyika kwa mashine za elektroniki

No comments:

Post a Comment