26 July 2013

WMA KUDHIBITI WEZI WA VIPIMO



 Na Jazila Mrutu
WA K A L A w a Vi p i m o ( W M A ) wamegundua vifaa maalumu ambavyo vinaratibu mifumo ya ukaguzi na kupunguza tozo kwa wafanyabiashara kutokana na kurahisisha utendaji kazi. Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Meneja Mawasiliano wa Vipimo Tanzania, Irene John alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya vifaa vinavyotumika kurahisisha kazi zao katika ukaguzi
. Alisema, vifaa hivyo vitatumika katika magari ya mafuta na malori ya mchanga kwa ajili ya kupima uzito na ujazo, pia alieleza kuwa wafanyabiashara ndogondogo wanaowaibia wananchi kwa kutumia mizani isiyokidhi viwango walivyoviweka nao watadhibitiwa.
"Tunajitahidi kuhudhuria kwenye maonyesho mbalimbali na kuelimisha wajasiriamali juu ya utumiaji wa mizani na kuhakikiwa ili kuepusha wizi unaoendelea kwa baadhi ya wafanyabiashara," alisema Irene.
Mwanasheria kutoka katika wakala huo, Moses Mbunda alisema, utekelezaji wa ukaguzi kwa upande wa gesi za majumbani ulianza Julai 19, mwaka huu na kuahidi kuanza ukaguzi kuanzia bandarini hadi kwa wasambazaji. Naye Meneja wa Upimaji Wakala wa Vipimo, Richard Kadege aliwaomba wananchi kushirikiana vizuri na Wakala wa Vipimo ili kudhibiti wizi huo unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara wadogo wadogo.

No comments:

Post a Comment