Na Goodluck Hongo
CHAMA cha Demokrasia
na Ma e n d e l e o ( CHADEMA) kimepanga kuzunguka nchi nzima kwa usafiri wa
anga, majini na nchi kavu, kufanya mikutano ya hadhara ambayo itakuwa ni
mabaraza yake ya katiba ili kuwapa fursa wananchi kujadili rasimu ya katiba
mpya na kutoa maoni yao.Akizungumza
juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Stendi ya Malori,
Majengo, mjini Songea mkoani Ru v uma , Mwe n y e k i t i wa CHADEMA, Freeman
Mbowe, alisema utaratibu mzima wa namna mabaraza ya katiba ya chama hicho
yatakavyoendeshwa kwa nia ya wananchi kutoa maoni yao na namna ya kuboresha
rasimu ya katiba mpya, utatolewa hivi karibuni.
Alisisitiza
kuwa wanataka katiba mpya inayotokana na mwafaka wa Watanzania wote.Alisema
tangu chama hicho kianzishe ajenda ya katiba mpya, kimekuwa na dhamira ya kuona
Watanzania wakijipatia katiba inayotokana na matakwa yao
kwa ajili ya kusimamia na kulinda masilahi yao."Ndugu
zangu, Watanzania wenzangu wa Songea, mtakumbuka kuwa ajenda hii ya katiba
ilikuwa ni ajenda ya CHADEMA, na tuliisimamia kwa miguu yote, mnajua hilo na haikuwa agenda
wala haijawahi kuwa ajenda ya CCM, ndiyo maana sasa chama hicho kinafanya
juhudi za kupingana na maoni ya Watanzania katika masuala ya msingi yaliyomo
ndani ya rasimu.
Alisema
hadi sasa tayari mabaraza ya katiba yameanza kukutana, lakini asilimia kubwa
yametawaliwa na CCM, lakini wao pia na Watanzania wengine wote wanaoipenda nchi
yao, wana fursa ya kuunda mabaraza yao."Tutakuwa
na mabaraza ya katiba nchi nzima, ambayo tutayafanya kwenye mikutano ya wazi ya
hadhara. Hatutajifungia ndani kama
wanavyofanya wao," alisema.Mbowe
aliongeza kusema kuwa katika rasimu ya katiba mpya pamoja na kuwepo kwa masuala
mengi, kuna mambo manne ambayo Mtanzania yeyote makini na anayeipenda nchi yake
atalazimika kukubaliana na mapendekezo ya Tume ya Jaji Joseph Warioba.
"Sasa
jiandaeni kwa mabaraza ya katiba ya CHADEMA, tutazunguka nchi hii ikibidi kwa
ndege, yatakuwa yakifanyika kwenye sehemu za wazi, ambayo siku nzima wananchi
wa eneo husika watajadili rasimu ya katiba mpya wakitoa maoni yao, kisha tutayachukua pamoja na saini
zao...nchi nzima tutafanya, viongozi wote, wabunge wote watasambaa nchi
nzima," alisema Mbowe.Al
i b a i n i s h a k uwa y e y e h a t amu o g o p a r a i s , l a k i n i
atamheshimu, hataogopa polisi lakini atawaheshimu, hataogopa jeshi lakini
ataliheshimu jeshi na hatamheshimu mtu yeyote asiye heshimu ubinadamu au mtu
mwingine.Alisema uchaguzi wa kata nne mkoani Arusha wameshinda kwa mapambano ya
damu ambapo watu wao walipigwa kila mahali na kukatwa mapanga na mashoka na
vijana wa CCM.
No comments:
Post a Comment