25 July 2013

AGIZO LA DKT. MAGUFULI KUTEKELEZWA JANGWANI



 Na Goodluck Hongo
AGIZO l a Wa z i r i wa Uj e n z i Dk t . John Magufuli la kujengwa Barabara ya Jangwani-Kigogo jijini Dar es Salaam litaanza kutekelezwa kuanzia Agosti 6 mwaka huu licha ya kuwepo kwa kesi mahakamani.Kesi ambayo ilifunguliwa na wamiliki wa nyumba wapatao sita katika eneo hilo
. A k i z u n g u m z a n a mwandishi wa habari hizi jana jijini Dar es Salaam, Mkurungenzi wa Kampuni ya Heri Sigh tawi la Dar es Salaam ambayo ndiyo ilipata tenda ya ujenzi wa barabara hiyo, Jospal Sigh alisema ujenzi wa kipande hicho kilichobaki kitaanza kujengwa rasmi mwezi huo.
Awali Waziri wa Ujenzi Dkt.Magufuli alifanya ziara katika Mkoa wa Dar es Salaam kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Barabara ya Jangwani hadi Ubungo ambapo licha ya kukamilika sehemu kubwa ya barabara hiyo lakini hakukuwa na lami katika kipande cha kuanzia Jangwani hadi Njiapanda ya Daraja kuelekea Kigogo.
Baada ya kukagua barabara hiyo, Waziri Dkt. Magufuli ndipo alipotaka kujua sababu za kushindikana kukamilika kwa barabara hiyo na mkandarasi kukaa eneo la mradi kwa zaidi ya miaka miwili bila kazi.Akitoa maelezo mbele ya Waziri Magufuli mhandisi mshauri wa kampuni hiyo, Musa Ally alisema sababu za kushindwa kumalizika kwa kipande hicho ni kutokana na wananchi sita kufungua kesi mahakamani hivyo hadi kesi hiyo itakapokwisha ndipo wataendelea na ujenzi wa kipande hicho.
B a a d a y a k u p a t a maelezo hayo ndipo Waziri Ma g u f u l i a l i p o i a g i z a kampuni hiyo kuendelea na ujenzi wa barabara hiyo kama ulivyopangwa lakini wasibomoe nyumba hizo hata kama lami itapita pembeni mwa nyumba hizo
"Fidia wamechukua lakini hapo hapo wamefungua tena kesi mahakamani na ujenzi ulitakiwa kukamilika siku nyingi zilizopita sasa Watanzania wajue kuwa wanaochelewesha maendeleo ni baadhi ya watu wachache kwani fedha zipo za utekelezaji wa miradi hiyo, nakuagiza mkandarasi ujenge barabara hii mara moja hata kama lami itapita pembeni mwa nyumba hizo wewe weka lami, lakini usibomoe nyumba hata moja na pia mtendaji mkuu wa TANROADS nakuagiza ukafungue kesi kwa watu hawa kwa kuitia hasara serikali kwani hilo linawezekana,"alisema Dkt. Magufuli.
Katika ziara hiyo Dkt. Magufuli alikagua barabara zote zinazojengwa Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam ikiwemo mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi wa (DART).

No comments:

Post a Comment