02 April 2013

Wamaliza kufukua kifusi cha ghorofa 16


Na Peter Mwenda

KAZI ya ukoaji watu waliofunikwa na kifusi cha ghorofa 16, ambalo limeanguka mwishoni mwa wiki kwenye Mtaa wa Indira Ghandi, Barabara ya Morogoro, Dar es Salaam, imemalizika jana ambapo miili mitatu ilipatikana na kufikisha idadi ya watu 26 ambao wamepoteza maisha katika tukio hilo.


Maiti zilizopatikana zilifahamika kwa majina ya Hamad Mirambo (50), mkazi wa Tandare, mtoto Zahir Mohamed Ganji (8), Salim Haliko, mkazi wa Handeni, mkoani Tanga, Kata ya Kwidiboma.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema jeshi hilo linamshikilia mmliki wa jengo hilo Bw. Raza Hussein Damji, mwanaye Bw. Ali Raza Damji na Mhandisi Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Bw. Ogare Sallu.

Alisema wengine wanaoshikiliwa ni Mhandisi wa Majengo wa Manispaa ya Ilala, Bw. Goodluck Mmbanga, Mkaguzi wa Majengo Manispaa ya Ilala, Bw. Willibroad Mliagusu, Bw. Ibrahim Kisoka, Mkandarasi wa jengo, Bw. Ibrahim Kisoka na Zona Ussi.

Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Bw. James Mbatia, ambaye alishiriki katika uokoaji huo, alisema Serikali inapaswa kujiweka tayari kwa kununua vifaa vya kisasa kwa ajili ya
majanga kama hayo.

No comments:

Post a Comment